Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Haki waalimu wana kazi ngumu sana
Unataka walimu wafanye nini ili ninyi single mothers mkubalike? Haitatokea labda karne ijayo. Hata wazaliwa wa single mothers hawapendi single mothers.
Haohao single mothers hawataki kuletewa wakwe ambao ni single mothers. Mjue msivyotakiwa.
 
Umeishiwa hoja umeamua sasa utumie personal attack siyo?? Aise kazi kweli kweli!!
 
Umeishiwa hoja umeamua sasa utumie personal attack siyo?? Aise kazi kweli kweli!!
Nimeishiwa hoja ipi? Watu hawataki single mothers, na watu hao ni pamoja na single mothers wenyewe hawataki uchuro huo ujirudie kwenye familia zao wala za wapendwa wao. Clear.
 
Nimeishiwa hoja ipi? Watu hawataki single mothers, na watu hao ni pamoja na single mothers wenyewe hawataki uchuro huo ujirudie kwenye familia zao wala za wapendwa wao. Clear.
Uliposema kuwa mimi ni single mother ulikuwa na uhakika upi?? Wanaume wengi wa JF ndivyo mlivyo mkiishiwa hoja huwa mnakuja na personal attack kama defence mechanism maana huwa hamkubali kushindwa mbele ya wanawake hata kama mnajua kabisa kuwa mnachotetea siyo sahihi!!
 
Kwa hilo la kukutaja kama single mother naomba radhi, nimekosea.
Lakini hoja dhidi ya single mothers iko palepale, kwamba hata single mothers wenyewe hawakubali kuletewa mkwe ambaye ni single mother.
 
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
mkuu Nyenyere naomba kuuliza maswali machache kwenye sentesi nilizobold na kupigia mstari tukianza na hapa

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu

unamaanisha ni wanawake peke yao wanaopaswa kuwa katika hali ya bikira wao ili wanaume wahisi wamepata mke mwaminifu?unamaanisha wanaume peke yao ndio wenye haki ya kupata hisia hiyo ya usalama?wanawake hawastahili au hawana haki ya kuhisi kuwa wamepeta mtu mwaminifu?unaliongeleaje swala la mwanaume kujitunza mpaka ndoa yake?

pili Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati

single fathers ni matokeo ya nini? accident,kubakwa,kulazimishwa kubambikiziwa au unatafsiri vipi uasherati au uzinzi mkuu?

tatu Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo

unaweza kuniambia majestically ni single baba wangapi ambao wako radhi kuoa mwanamke bila kujali ikiwa mwanamke atampenda mtoto wake au la? unamaanisha ni kina mama peke yao ndio hujali sana watoto wao hivi kwamba wanataka sana mume apende mtoto aliye naye tayari?unamaanisha wanaume huwa hawajali vile mwanamke atamtreat mwanaye aliyemzaa kabla ya ndoa?

nne Mtoto si wako

ni kweli sio wako,lakini namna gani single babas wao watoto zao wa kabla ya ndoa wanakuwa wa wake zao wapya?wake zao wanapolea hao watoto wanakuwa wanalea watoto zao au watoto za mwanamke mwenzao aliyezini na mumewe kabla hajaolewa naye?

tano Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo

mkuu unataka kumaanisha na kutuaminisha kuwa single babas hawawatafuni baby mamys zao vile watakavyo wakishaoa ? unamaanisha hii tabia wanayo single mothers tu au point yako ni nini hapa?

nina maswali mengi sana mkuu kutokana na hoja zako tajwa katika mada hii,lakini kwa kuanzia em tuanze na hayo machache then tuendelee.

Asante.
 
Kwa hilo la kukutaja kama single mother naomba radhi, nimekosea.
Lakini hoja dhidi ya single mothers iko palepale, kwamba hata single mothers wenyewe hawakubali kuletewa mkwe ambaye ni single mother.
Siyo wote
 
mkuu Nyenyere naomba kuuliza maswali machache kwenye sentesi nilizobold na kupigia mstari tukianza na hapa

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu

unamaanisha ni wanawake peke yao wanaopaswa kuwa katika hali ya bikira wao ili wanaume wahisi wamepata mke mwaminifu?unamaanisha wanaume peke yao ndio wenye haki ya kupata hisia hiyo ya usalama?wanawake hawastahili au hawana haki ya kuhisi kuwa wamepeta mtu mwaminifu?unaliongeleaje swala la mwanaume kujitunza mpaka ndoa yake?

Kwanza mada ni kuhusu single mama. Pili anayeoa ni mwanamume, hilo halina haki sawa. Tatu chastity ni kwa wpte lakini mwisho wa siku wakianza uzinzi mapema, anayekuja kujutia KIMWILI ni mwanamke.Nne si vema kila kinachosemwa kiwekwe kwa kulinganisha, wewe pia waweza anzisha mada kuhusu wanaume, mimi sihubiri haki sawa hapa walasio muumini wake. Mimi ni muumini wa uasili wa mwanadamu
pili Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati

single fathers ni matokeo ya nini? accident,kubakwa,kulazimishwa kubambikiziwa au unatafsiri vipi uasherati au uzinzi mkuu?
Single father ni illusion tu, haina uhalisia. Ni yale mambo ya kutafuta haki sawa.Mwanamume hazalishwi, anazalisha tu. Mengine ni wishful thinking
tatu Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo

unaweza kuniambia majestically ni single baba wangapi ambao wako radhi kuoa mwanamke bila kujali ikiwa mwanamke atampenda mtoto wake au la? unamaanisha ni kina mama peke yao ndio hujali sana watoto wao hivi kwamba wanataka sana mume apende mtoto aliye naye tayari?unamaanisha wanaume huwa hawajali vile mwanamke atamtreat mwanaye aliyemzaa kabla ya ndoa?

Do your homework.

nne Mtoto si wako

ni kweli sio wako,lakini namna gani single babas wao watoto zao wa kabla ya ndoa wanakuwa wa wake zao wapya?wake zao wanapolea hao watoto wanakuwa wanalea watoto zao au watoto za mwanamke mwenzao aliyezini na mumewe kabla hajaolewa naye?

Mwenye ndoa ni mwanamume, wewe unatolewa posa unakwenda kujenga ukoo wa mwanamume. Mwanamke ni msaidizi wa mumewe, hivyo hakuna usawa unaoutaka kwenye ndoa mpaka maumbile. HAKUNA SINGLE BABA. Ngoja nikupe somo:

Mwanamume anatongoza mwanamke analala naye, akizaa mtoto nje ya mipango ya ndoa atahitaji kujiridhisha kuwa ni damu yake, hapo atamchukua kwenye nyumba yake kwa sababu huyu mwanamke aliyemzaa ametimiza jukumu la kumjengea ukoo. Kama hajaridhika kuw mtoto ni damu yake ama hkuwa tayari kujenga ukoo, ndipo sasa mtoto hubaki kwa mama yake na hapo tunampata single mama. Umewahi kujiuliza ni kwa nini mjane haitwi single mother? Sababu ni kuwa watoto wake wana ukoo wao!! Kwa hiyo hata mume akifariki, mama ya watoto hawezi kamwe kuwa single mother, watoto wana baba wala hawaitwi kwa majina ya wajomba zao,mama amezaa ndani ya mkataba wa ndoa. Single mama anazaa nje ya mkataba wa ndo mtoto anakataliwa na mwanamume. Hana ukoo tena, badala yake ana-retain ukoo wa mama,

tano Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo
mkuu unataka kumaanisha na kutuaminisha kuwa single babas hawawatafuni baby mamys zao vile watakavyo wakishaoa ? unamaanisha hii tabia wanayo single mothers tu au point yako ni nini hapa?

Haki sawa inakipotosha.Mume aweza kuoa hata wanawake ishirini kwa wakati mmoja lakini mwanamke ataolewa na mwanamume mmoja tu at a time. Pili anayeoa ni mwanamume sio mwanamke, hivyo si vema kuweka kada wa chama cha upinzani ndani.
nina maswali mengi sana mkuu kutokana na hoja zako tajwa katika mada hii,lakini kwa kuanzia em tuanze na hayo machache then tuendelee.

Asante.

Karibu
 
Back
Top Bottom