Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Umepotea kwa kuyakataa maarifa. Mungu hapangi ndoa, bali amekupa utashi (free will). Usije kumshutumu Mungu kwa matatizo yako ya kwenye ndoa, Yeye ni shahidi tu wa MKE WA UJANA. Ndoa pekee zilizo kwenye rekodi ambazo Mungu alizipanga mwenyewe ni ya Adam vs Hawa na nabii Hosea vs Gomer.

Kuzaa nje ya ndoa kunamwathiri zaidi mwanamke hata kama utapinga mno, na mwanamume anayejitambua hawezi kuoa single mother bali aweza kuoa mjane. Tunza sifa yako njema, epuka kujiingiza huko, uwe mwanamke mwenye kutakiwa na wote.
Sawa lakini haibadilishi ukweli kwamba Mungu ni wa wote wanaume na wanawake

La sivyo tusingeona single mothers wanaolewa kila iitwapo leo kama ambavyo tunaona single fathers wanaoa kila iitwapo leo ifike mahali tuite chepeo chepeo tu na siyo kijiko kikubwa
 
Nilikuwa najiuliza mbona humu JF wanawananga sana single mothers kuwa hawaachani na baba wa watoto wao, nikafikiria kwa msimamo tulionao wanawake tukiacha tunaacha kweli, wanatusingizia.

Lakini kwa nilichoshuhudia kwa macho na masikio yangu, sijui wanakwama wapi hawa wanawake wenzangu jamani.

Ni mama wa watoto wawili aliyezaa wakati anasoma chuo fulani na mwanaume fulani kipindi hicho akiwa chuo, mtoto wa kwanza alimzaa akiwa mwaka wa kwanza na wa pili alimzaa wakati anahitimu chuo.

Kwa bahati nzuri akapata kazi kwenye kampuni fulani na kwa jeuri yule mwanaume aliyekuwa naye chuo alimuacha katika mazingira ya kutatanisha na mawasiliano yakawa yamekatika kipindi wamehitimu chuo.

Baada ya mwaka 1 huyu mdada akawa amepata mwanaume mwingine akamuoa tu vizuri kwa harusi kubwa. Cha ajabu wiki kama 4 zimepita yule kaka aliyezaa naye watoto wawili akaibuka, akamtafuta, wakagombana na wakabembelezana wakakubaliana huyo kaka atakuwa anamtumia hela mdada ya kuwahudumia watoto, muda huo akijiandaa kumwambia mume wake kuhusu hao watoto awarudishe kwa baba yao.

Wakakubaliana kuwa siku fulani watakutana hoteli fulani atawapeleka watoto wakamsalimie baba yao, bila mume wake kujua.

Siku ya siku mdada akawapeleka hoteli nje kidogo ya mji, basi wakakutana, ila mdada akawa na msimamo kuwa endapo ex atajaribu kuleta ushawishi hatakubali hata siku moja, bahati mbaya mtoto wao wa kwanza akawa anaongea maneno kwa baba na mama ya kuwaleta pamoja hadi mdada akawa na huruma kwa ex wake akajikuta anataka avunje ndoa arudi kwa ex wake na huku ex wake ana mke na mtoto 1.

Juzi mume wa ndoa anapata mchezo mzima anamuuliza mke wake anasema ni kweli anadai talaka arudi kwa baba watoto wake.

Nimeamini wanawake muda mwingine hatutumii akili. Alikutelekeza, akakuacha mwenyewe ukatunza watoto mwenyewe from nowhere mnarudiana kisa maneno ya mtoto wao wa kwanza yamemfanya alie, amhurumie na amrudie ex wake.
Je, 7,800 zinatosha?
 
Watakuwa wako kipindi ambacho hawajapata ufahamu, lakini baada ya hapo si wako tena. Watoto wako ni wale waliotoka viunoni mwako tu, mengine ni kujifariji na kujipoteza. Time will tell.

Kama naweza mlea Mtoto akiwa hana akili na akiwa nayo anaenda pia ni sawa, maana hata mie ningeweza kuwa huyo mtoto!

Humu duniani twaishi mda mfupi Sioni sababu ya kupiganq vita
 
Nimewauliza hivyo ili nijue kwamba ninyi mkisema single mothers wasiolewe mnawaongezea nini au mnawapunguzia nini kwenye maisha yao ilihali wapo wanaume wenzenu wengi wanaojitambua wanawaoa kila iitwapo leo na ndoa zao zinadumu

Yaani ninyi wanaume wa humu JF na hizi kejeli zenu za kila siku kuhusu single mothers nilitegemea mkisema wanaume wasioe single mothers basi wanaume wote hapa bongo au kote duniani watafuata mitazamo yenu na pengine labda ipo siku single mothers wataacha kabisa kuolewa lakini wapi

Tatizo lenu wanaume huwa mnadhani Mungu ni wenu peke yenu na kwamba eti ndoa inapangwa na wanadamu!! Sasa kama anaruhusu wanaume wenye watoto waoe wanawake wasio na watoto kwanini asiruhusu wanawake wenye watoto waolewe na wanaume wasio na watoto??

Tena ukizingatia hao wala hawakujibebesha mimba wenyewe lakini mwanaume akizalisha bila ndoa anaoa vizuri tu ila mwanamke akizalishwa bila ndoa kuolewa ndiyo iwe kizaazaa?? Huwa nawaambia siku zote Mungu ni wa wote wanaume na wanawake na yeye ndiye anayepanga ndoa mtake msitake God is never unfair like humans na ndiyo maana haya malalamiko yenu hayajawahi kuisha humu mitandaoni wala huko mitaani na kamwe hayatakuja kuisha!!

Achakusema vitu ambavyo havipo,ujinga wao ndio unao wafanya kushindwa kuelewa uhalisia wa mambo Mungu hampangii binadamu ndoa ndio maana kampa utashi wa kufanya maamuzi. Jambo linalo ongelewa hapa nikama elimu tuu ya kumsaidia mwanaume na mwanamke asije akafeli kwenye utashi aliopewa kwa yale yanayo mkabili.. najua wanawake wanafikiri wanasimangwa ila kiukweli mnafeli pakubwa hata second chances mnazopata bado mnaziaribu its sad vry sad.
 
Daima nitabaki na msimamo wangu Thabiti, hasa baada ya kuwa na mahusiano kadhaa na hao watu.
 
Alipatwa na nini ?
The TRUE STORY na iwe ni USHUHUDA:

Kijana wa Mwl. Mwakasege alikuwa na uhusiano na mwanamke mzuri tu wa DSM ambaye aliwahi kugombea Ummiss wa wilaya maarufu Dsm na kushika nafasi nzuri.

Huyu binti alikuwa na Mtoto mmoja aliyezaa na Mwanaume mwingine.

Siku kijana anaenda kumwambia Mzee wake habari ya kumuoa huyu binti alimwambia Mzee ukweli kuwa binti ana mtoto ila hajamwona mwingine wa kumuoa isipokuwa huyo.

Mzee alichomwambia tu kuwa Kamwe hatuwezi kukuchagulia mke ili usije kutulaumu lakini akamuuliza

''Je unamfahamu vizuri huyu binti? Je aliyemzalisha mtoto? ''

Jamaa akasema hana shida, na kumbe jamaa alikuwa anampenda sana huyo mtoto na kumfanya kama wakwake wakwanza.

Yule Binti alikuwa hadi anaenda Moshono-Arusha nyumbani kwa Mwakasege na kushinda na mama mkwe.

Baada ya kuishi na Kijana, aisee haijapita hata miaka miwili akamtumia ujumbe kijana kuwa ''Anaomba amsamehe sana kwakuwa ameamua kurudiana na Baba wa mtoto'' it means walikuwa wanawasiliana.
 
Mkuu hivi mwanaume aliyeoneshwa staili nyingi na wanawake tofauti akioa mwanamke asiyezijua hizo staili ndiyo hatatafuta wanaozijua nje??

Mbona humu kila siku tunakutana na nyuzi zinasema mwanaume ili asichepuke lazima umuoneshe staili tofauti tofauti sasa hizo staili mwanaume angezijuaje kama asingekuwa na uzoefu nazo??
Mwanamume hata ukilala kama gogo atakojoa tu, na furaha yote ipo hapo, get the facts straight
 
Habari za Jumapili Wadau.

Joshua Christopher Mwakasege ni Mtoto wa Mwalimu wa Neno la Mungu, C. Mwakasege.

Ninawafahamu wote wawili na familia yao kwa ujumla vizuri tangu nikiwa mtoto mdogo.

Sijaagizwa kuyasema nitakayoyasema ILA nitakwenda kuandika yafuatayo kwakuwa pia Mwl. Mwakasege ni Mtu MUWAZI sana katika kitu / mambo yanayofundisha wengine. Amekuwa akitoa mifano mingi hata kuhusu alivyoanza uhusiano na mkewe wa sasa Diana.

Kijana wake alifariki ghafla October mwaka Jana, sasa ana mwaka kaburini.

SABABU YA KIFO CHAKE: Mengi yanasemwa, na mengine hayafahamiki na hata Mwl. Mwakasege alisema tu kuwa Mwanae amefariki ghafla. Ila kwakuwa kuna cha kujifunza nitaeleza kifupi sababu ya kifo chake.

Msomi Joshua Mwakasege alikuwa na Uhusiano na mwanamke mzuri, aliyekuwa na Mtoto. Mwanamke huyu (sitamtaja jina) aliwahi kuwa miss wa wilaya mojawapo hapa DSM. Walipendana sana na Joshua mpaka ikafikia mahali pa Joshua kumtambulisha rasmi kwa wazazi wake.

Mwl. Mwakasege hakuwahi kumkatalia Mwanae kumuoa binti mwenye mtoto hata siku moja, ila alimuuliza swali

''Unamfahamu vizuri binti unayetaka kumuoa'' ?

'' Unamfahamu aliyezaa nae'' ?

Mara zote majibu yalikuwa ndio na hakukuonekana na tatizo lolote.

Mwishoni Mzee mwakasege alimwambia kijana wake kuwa unapaswa kumwomba Mungu sana kuhusu mke wa kumuoa na tutaomba pamoja LAKINI, mwisho wa yote wewe ndiye unayemfahamu zaidi binti utakayemuoa, na hatuwezi kukuchagulia Mke.

Joshua Mwakasege alimpenda sana yule Mwanamke na walikuwa na malengo, alimpenda yule mtoto kama wakwake na kuamua kumsomesha, kumlisha na kumvisha na alikuwa anamwita ni Mwanae wa kwanza, wengine watafuata.

Pamoja na yote hayo, na baada ya kupita muda flani wa mahusiano, bila kutegemea yule mwanamke alisafiri kutoka DSM na kuja Arusha, kisha siku moja Joshua akiwa kazini alipata ujumbe kutoka kwa Mke wake (Ninasema hivyo kwakuwa walikwishaoana) ujumbe ulimwomba msamaha sana na mkewe akimwambia kuwa ameamua kurudiana na Baba wa mtoto wake.

Hii inamaana walikuwa katika mawasiliano na mahusiano bado.

Kilichomuua Joshua Mwakasege bila shaka ni Msongo wa mawazo ulipitiliza, Depression ingawa iliitwa shinikizo la damu.

USHAURI : Vijana wote wa kiume na wa kike, tuwe makini sana na watu tunaoanzisha nao mahusiano ya kuelekea kwenye Ndoa. Ni vizuri sana kuchunguza ikiwa wana uhusiano wa awali na wapenzi wao haswa waliochangia damu kuzaa mtoto/watoto.

Hata Mabinti pia mnapaswa kuwa makini sana katika hili.

Jumapili Njema.
 
Inawezekana bwana mdogo ilikuwa ndio penzi lake la kwanza hivyo moyo wake ulikuwa haujatoboka toboka...

In short katika mapenzi yatupasa kutumia akili na sio moyo, moyo ubakie tu kuwa chemchem ya maji ya uzima...
 
Unaanzaje kumuoa singo maza??? Mabaharia mnakwama wapi? Njooni niwape connection ya mabinti bikra wanaosubiria upepo wa kisulisuli ili waolewe.

Usithubutu! Usithubutu! Usithubutu! Kuoa singo maza, ni laana hiyo.
 
Back
Top Bottom