Wako wapi mabinti waliotajwa na FA kwenye wimbo wa “Mabinti”?

Wako wapi mabinti waliotajwa na FA kwenye wimbo wa “Mabinti”?

Nakumbuka enzi hizo wanatajwa walikua warembo wanaosumbua mjini,wapo wapi siku hizi??? Tukumbushane na lyrics hapa chini...

Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Thamani zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Wengine ndani jeans wengine ndani ya skirt
Wengine mini au magauni ya vitambaa vyepesi
Mradi istizahi wanipore uhuru wa nafsi
Weledi wa ajabu kwenye mambo ya chini ya paa
Kuna werevu wa ajabu kwenye mambo mengi bar
Hawanipi shida sio balaa
Na zaidi nawapenda mabinti watundu
Mapozi ya kichokozi au sio pozi vurugu
Mitindo ya kiyahudi hijabu zikatazo kichwa
Na mikogo ya kifisadi sio mmakini inapotosha
Unaona shanga za miguu naita vikuku
Ingawa wenye ufahamu nipotofu
Watoto wa kibongo hakuna mchezo
Kuna walatino waafrika na wasanta domingo
Kuna mpasua toka chini mpaka kando ya kiuno
Milango wazi kwa yeyote aliye na mdomo
Sijapoteza macho ya kuangazi warembo
Nakosa uzalendo nionyeshwapo miguu
Napata uchizi wa mtima
Choma fedha na muda sioni balaa
Natumai sifunzi hasaraa?
Ni hadithi na sio biashara
Ukishindwa Inshallah
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Thamani zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Kuna kifua kama cha Zay B
Kiuno kama cha Ray C na pozi Jay Dee na sauti kama Fina
Au labda ya aunt Ndina ipo njema matabasamu
Kama binti Maumba wa kino msio nidhamu
Mtafanywa mpende ngono Hold on!
Kuna pozi za kimtoni kama Tausi Likokola
Unataka ni full bakora mabinti wangali wanang'ara
Warefu warembo kama twiga mithili ya Happy Magese
Midomo kama ya Shose
Utapenda uonekane yaani viwanjani ututese
Au binti maarufu utasema Aina anatosha?
Kama nnataka mwanya nafahamu wapi ntaupata
Mwite Aminata wa Keita
Binti wa vigogo unamtafuta Mboni Mhita?
Mwili utakaokufanya upende love kama wa Mercy Galabawa
Na macho yanayovuta kama ya Miriam wa Ikoa
Unaweza utangaze ndoa
Wengine mziki kama Shanice
Au kama Connie Stephans
Naiota rangi ya Caroline na lugha tamu kama ya Seven
Najua mnawaita masister du! Bendera hewani
Sometimes wavute widdy Mentally japo wazuri
Mithili ya Kibibi
Miondoko kama Faudhia
Au ungependa kithethe mithili ya Radhia
Watoto wa shule wassiwafanye mpagawe
Ilhali kuna wenye haiba kama Halima Bandawe
Mi kwa mabinti, nisahauliwe
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Thamani zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Kuna mabinti wapo kamili kila idara familia bora
Akili zisio lala maumbo bomba na sura
Kuwapata ni full Gospel wao ni ajira na hawaitaji zaidi ya sera
Kuna mitego ya khanga mambo kitanga
Kama una jichohii unapaswa kuwa umeiona
Michirizi ya utamu nyuma ya goti mimi hoi
Una moyo hai hili sio toi pigo jingine kama Sunset
Ubishi haufai ona visa kwenye mitindo ya vichwa
Anuani pepe za mitandano na simu zinawehusha
Ukitaka upgawe njoo kiwanja
Jaribu kuwa mkweli nionapo vitovu wazi hakuna si mahututi mimi
Kuna wadada, wamama, masister du wote wapenzi
Wana nataka staki sio kamanda naachia ngazi
Omba majina Amina kawa Amayna, Naima, Clara na Rayyah!
Kuna Tayana, Aneth hata bongo kuna Aaliya?
Candy, Nicole, Uenice au labda Marayah
Sikitu hataki jina na Asia anaitwa Eshia
Pamba hazibani ni hatari
Ni makusudi tuone mstari wa kufuli mambo ya kivazi
Wachumnba wote mpo pina wote funga kazi hakuna
Msiache washkaji wawafanye watumwa nyia ndio mama
Anayewaponda apate laana
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Thamani zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!
Huu ndio ulikua mziki.Nakumbuka nilitoloka shule Kibaha Secondary nikaja Dar kihudhuria show ya FA pale Chuo kikuu Mlimani.Nani kama FA,nilikua namkubali sana kuliko madogo wanavyomkubali Mondi.
Mimi nikiwaona kina FA Jay Mo,Solo huwa nafurahi sana coz hicho ndio kizazi chetu cha muziki.
Nilinunua albamu zote za FA nilikua nazo hadi leo makava ya zile kanda ninazo.Mara ya mwisho nilihangaika sana kupiga picha na FA pale mabibo hostel it was 2003.
Ngoma ya mabinti ni kweli inafanana na ya Jay Mo ile ya kama unataka demu zilikua moto sana zote mbili,na tumecheza sana club hizo ngoma. FA katolewa kimziki na produza Boniluv hadi leo FA hawezi kutaja historia yake career wise bila ku mention jina la Boniluv.
MADEMU KWENYE WIMBO
1.Seven...alikua meneja wa Kiba,alikua pini sana enzi hizo na aliwahi msimamia kimziki Jay dee pia
2."Kisese mithili ya Radhia"....hawa walikua wawili walikua wanaunda kundi la Unique sisters alikuwepo Radhia na Radhina
3.Happy Magese alikua Miss for now anajulikana kama Millen Magese
4.Zay b,Ray C, wote walikua wanamziki.
5.Shose alikua pini sana,now nadhani yupo jela kwa ile case yao pale Stanbic
6.Mboni Mhita alikua mbunge enzi hizo nasikia alikua pini balaa
Enzi hizo ndio Pfunk alikua anammendea Kajala nadhani kwenye wimbo wa Jay mo katajwa kama sijakosea.
Sijawahi ona wimbo mbaya wa mwanafa hadi leo.kwenye laptop yangu nina nyimbo zake zote toka nipo chuo nazitunza.
Kuna ngoma moja yupo na lady jayde inaitwa "siku nikianguka" inahusu kifo usipime kali sana na ina touch sana,kuna mistari hua naipenda inasema
(nihodhi makazi yangu kando ya ufukwe wa bahari,
mke mzuri aliepambwa nyumbani na watoto walionawiri,
mikono yangu izungushe usukani wa motokari,
tupia macho takwimu,mimi mwana wa adamu kwani kasi inatisha,
maisha yangu yatakatika,
nafsi itabaki na tamaa lakini kamwe mwili hautoamka")
Nani kama MwanaFa hiki kizazi cha iyoooo Laizaaaaa haikuji mambo haya.
 
Natafuta "haina fagio" Mwana FA. Yani sijaweza ipata kwenye platform yoyote online.
 
Natafuta "haina fagio" Mwana FA. Yani sijaweza ipata kwenye platform yoyote online.
Usipime hilo dude,"najaribu kuandika rymes ili hali wino sina........",toka kwa B ushauri wa kirafiki,msiongee nikiwa sipo wanafiki, njooni sitawadhuru mademu zenu,zimia bovu washikaji zangu kama navyowazimia machangu,"....ipo boom play kule nenda utazikuta zote
 
Nakumbuka wimbo huu ulifanana Sana na wimbo wa Jay mo Kama unataka demu... Kiasi ikaleta bifu Kati ya wawili hao coz Kila mtu alisema mwenzie kaiba idea...Hadi Leo hatujui idea ilikuwa ya Nani
Mbona inajulikana mkuu.
Idea ilikuwa ya Juma Mchopanga alitaka amshirikishe huyo dogo FA na ndio huo wimbo wa kama unataka demu.
Dogo alivyo snitch akamzunguuka msela akaenda kutoka na hiyo mabinti.
Sema 'kama unataka demu' ya Jay Mo imesimama zaidi.
 
Shose Sinare alikuwa anafanya kazi Stanbic bank Tz kama mkuu wa moja idara za benki hiyo.

Halima Bandawe huyu manzi alikuwa kisu sana miaka 2000 mwanzoni alikuwa anatokea Tanga. Kwa sasa labda atakuwa mmama wa miaka 38 ~ 40. Japo nilikuwa mtoto hata mimi nilikuwa nammezea mate kama FA.
Halima namfaham sikuwahi kujua Kama alitajwa kwenye hii nyimbo, mdogo ake wa kiume kazaa na Rose ndauka mtoto wa kwanza. Alikuwa anafanyakazi Vodacom.
 
Back
Top Bottom