Wako wapi mabinti waliotajwa na FA kwenye wimbo wa “Mabinti”?

Huu ndio ulikua mziki.Nakumbuka nilitoloka shule Kibaha Secondary nikaja Dar kihudhuria show ya FA pale Chuo kikuu Mlimani.Nani kama FA,nilikua namkubali sana kuliko madogo wanavyomkubali Mondi.
Mimi nikiwaona kina FA Jay Mo,Solo huwa nafurahi sana coz hicho ndio kizazi chetu cha muziki.
Nilinunua albamu zote za FA nilikua nazo hadi leo makava ya zile kanda ninazo.Mara ya mwisho nilihangaika sana kupiga picha na FA pale mabibo hostel it was 2003.
Ngoma ya mabinti ni kweli inafanana na ya Jay Mo ile ya kama unataka demu zilikua moto sana zote mbili,na tumecheza sana club hizo ngoma. FA katolewa kimziki na produza Boniluv hadi leo FA hawezi kutaja historia yake career wise bila ku mention jina la Boniluv.
MADEMU KWENYE WIMBO
1.Seven...alikua meneja wa Kiba,alikua pini sana enzi hizo na aliwahi msimamia kimziki Jay dee pia
2."Kisese mithili ya Radhia"....hawa walikua wawili walikua wanaunda kundi la Unique sisters alikuwepo Radhia na Radhina
3.Happy Magese alikua Miss for now anajulikana kama Millen Magese
4.Zay b,Ray C, wote walikua wanamziki.
5.Shose alikua pini sana,now nadhani yupo jela kwa ile case yao pale Stanbic
6.Mboni Mhita alikua mbunge enzi hizo nasikia alikua pini balaa
Enzi hizo ndio Pfunk alikua anammendea Kajala nadhani kwenye wimbo wa Jay mo katajwa kama sijakosea.
Sijawahi ona wimbo mbaya wa mwanafa hadi leo.kwenye laptop yangu nina nyimbo zake zote toka nipo chuo nazitunza.
Kuna ngoma moja yupo na lady jayde inaitwa "siku nikianguka" inahusu kifo usipime kali sana na ina touch sana,kuna mistari hua naipenda inasema
(nihodhi makazi yangu kando ya ufukwe wa bahari,
mke mzuri aliepambwa nyumbani na watoto walionawiri,
mikono yangu izungushe usukani wa motokari,
tupia macho takwimu,mimi mwana wa adamu kwani kasi inatisha,
maisha yangu yatakatika,
nafsi itabaki na tamaa lakini kamwe mwili hautoamka")
Nani kama MwanaFa hiki kizazi cha iyoooo Laizaaaaa haikuji mambo haya.
 
Natafuta "haina fagio" Mwana FA. Yani sijaweza ipata kwenye platform yoyote online.
 
Natafuta "haina fagio" Mwana FA. Yani sijaweza ipata kwenye platform yoyote online.
Usipime hilo dude,"najaribu kuandika rymes ili hali wino sina........",toka kwa B ushauri wa kirafiki,msiongee nikiwa sipo wanafiki, njooni sitawadhuru mademu zenu,zimia bovu washikaji zangu kama navyowazimia machangu,"....ipo boom play kule nenda utazikuta zote
 
Nakumbuka wimbo huu ulifanana Sana na wimbo wa Jay mo Kama unataka demu... Kiasi ikaleta bifu Kati ya wawili hao coz Kila mtu alisema mwenzie kaiba idea...Hadi Leo hatujui idea ilikuwa ya Nani
Mbona inajulikana mkuu.
Idea ilikuwa ya Juma Mchopanga alitaka amshirikishe huyo dogo FA na ndio huo wimbo wa kama unataka demu.
Dogo alivyo snitch akamzunguuka msela akaenda kutoka na hiyo mabinti.
Sema 'kama unataka demu' ya Jay Mo imesimama zaidi.
 
Halima namfaham sikuwahi kujua Kama alitajwa kwenye hii nyimbo, mdogo ake wa kiume kazaa na Rose ndauka mtoto wa kwanza. Alikuwa anafanyakazi Vodacom.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…