Wako wapi mapedeshee walioimbwa na kugawa pesa kwa wasanii wa bendi?

Wako wapi mapedeshee walioimbwa na kugawa pesa kwa wasanii wa bendi?

Deal zao zimekatwa,kwa sasa wako bize kumchafua Mh.Rais kichin chini.
 
Habari za week end wadau,

Kwa wale mashabiki wa mziki wa dance nchini,hasa bend za Fm Acadamia,Twanga pepeta,Malaika Bend,Acudo impact,Mashujaa band,Msondo Ngoma,Sikinde n.k mtakua mashahidi katika hili,

Miaka michache iliyopita nyuma kulikua na wimbi kubwa la vibopa,matajiri au kwa jina lingine mapedeshee wa jiji hili la Dsm waliokua wakiimbwa sana na kutajwa tajwa kwenye nyimbo za bendi hizi kila mara au kwenye matamasha ya bendi hizi,hii ilipelekea wao kutawanya au kugawa pesa nyingi kwa wanamuziki husika (hasa wenye asili ya Congo) na kwa mashabiki pia hasa dada zetu wa bongo movie na wasanii.

Wakati mwingine walikua hata wakigawa dola ya mmarekani na euros.

Jambo la kushangaza siku hizi siwasikii wala kuwaona wakifanya kufuru hizo,
Napatwa na mashaka pengine nini kimewakuta?au wameamua kwenda kutapanya nchi za jirani kama Malawi na Msubiji?

Wadau unaweza mtaja pedeshee uliyekua unamwamini sana kwa kutapanya au moja ya tukio uliloshuhudia akitapanta.

Binafsi nakumbuka kufuru ya Pedeshee Ndama mutoto ya ngombe na Pedeshee Bitus dhahabu...wadau wakubwa wa Fm Academia wazee wa Ngwasuma popote pale ndani ya jiji hili hasa Mango Gardern na maeneo mengine.
Daah kweli kuna siku hata elf kumi sn..alafu jamaa kaenda kuwatunza wazee wa kupekecha pekecha akudo impact..siku hizi hawapo ina maana wamehamia kenya ama south sudan?
 
Kuna mmoja bado yupo hasaa FM Academia wakipiga pale Mango Garden ni mrefu hivi anavaaga siku zote shorts na t-shirt basi huwezi mkuta anavaa suruali anatoaga sanaa hela kwa FM sijui ni nani yule??
 
Mkuu nimekamatwa na majukumu fulani kiasi kwamba sina muda tena kama zamani.
Najiandaa kustaafu kazi mwakani labda nitarejea kwa kasi

Acha hizo lazima na Mama Ngina amekubana haswa, ha ha haaaa.

Kila la kheri Mola awe nawe.

Ila ukipata muda uletege zile story story za maisha na safari za kurudi home kwa mamaa.

Na miss JF ya zamani, wengi mmeamua kuwa kimya, hamjui mnatukosesha mengi.
 
Pesa chafu hazina adabu na matumizi yake hayana adabu....Muda huu wanajifunza kuwa na adabu
 
Back
Top Bottom