Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Wakati ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere unaanza, watetezi wake walikuwa wanatoa mishipa ya shingo kuwa bwawa hilo likianza kazi umeme utashuka bei. Nikawa nasema miaka yote tumekuwa tukitumia umeme wa maji, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei rahisi, maana sababu ya umeme kuwa ghali hapa nchini haiendani na gharama za uzalishaji, bali sababu nyingine kabisa.
Watetezi wakawa wanasema gharama kubwa haiwezi kupungua kwa kutumia umeme wa mafuta. Wakajiapiza umeme wa maji ukianza automatically bei itashuka.
Wakati umefika na kile nilichosema kinaonekana. Bwawa limeanza kazi, umeme unazidi kupanda bei, na kibaya zaidi bado sio wa uhakika maana mgao bado upo, hata kama sio kwa kiwango kikubwa. Kwenye hili la bei wote ni mashahidi kwa walioanza kununua umeme hivi karibuni. Na hapo bado.
Paskali Mayalla Choicevariables, Lucas Mwashamba