Wako wapi wale waliokuwa wanatetea umeme wa maji utakuwa bei rahisi?

Waulize tuliowapa dhamana!! Kama sukari tu anapewa mshikaji wa Stationary Ili aagize sukari ya Bil 6.6 huoni Kwa mazingaombwe haya haya hata Bei ya Umeme inafanyiwa usanii Ili ipatikane hela ya kupiga??

Waulize wenye mamlaka ni vipi tozo ya miamala inazidi kupaa tu? Waulize pia makato ya LUKU nani kayapaisha??

Mwisho waulize nani kaipaisha Bei ya mafuta ya diesel na petrol??

Ukishajua nani mhusika Mkuu basi nenda huko huko mkaulizane
Nikawaulize mimi, badala ya ww chawa wa watawala? Mimi nilikuwa najua hakuna uwezekano wa bei ya umeme kushuka bila kujali ni chanzo kipi kinatumika kuzalisha umeme. Ndio maana nimewaita watetezi wa hii serekali na wale waliokuwa wanasema bwawa likianza kazi litatupunguzia gharama watumiaji, na kuvutia wawekezaji hasa wa viwanda, kwani gharama ya uzalishaji itashuka kutokana na kuwa na umeme wa uhakika, na wa gharama nafuu.
 
Wakati ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere unaanza, watetezi wake walikuwa wanatoa mishipa ya shingo kuwa bwawa hilo likianza kazi umeme utashuka bei. Nikawa nasema miaka yote tumekuwa tukitumia umeme wa maji, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei rahisi, maana sababu ya umeme kuwa ghali hapa nchini haiendani na gharama za uzalishaji, bali sababu nyingine kabisa.

Watetezi wakawa wanasema gharama kubwa haiwezi kupungua kwa kutumia umeme wa mafuta. Wakajiapiza umeme wa maji ukianza automatically bei itashuka.

Wakati umefika na kile nilichosema kinaonekana. Bwawa limeanza kazi, umeme unazidi kupanda bei, na kibaya zaidi bado sio wa uhakika maana mgao bado upo, hata kama sio kwa kiwango kikubwa. Kwenye hili la bei wote ni mashahidi kwa walioanza kununua umeme hivi karibuni. Na hapo bado.

Paskali Mayalla Choicevariables, Lucas Mwashamba
Watu walikuwa wanataka kupiga pesa kupitia huyo mradi
 
Kwani Tanzania ni mara ya jwanza hii kutumia umeme wa maji?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Soma post yangu vizuri, mimi sikuwahi kuamini ule utetezi wa kuwa umeme wa maji utakuwa bei rahisi, maana tumekuwa tukitumia umeme wa maji miaka yote, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei nafuu. Nilikuwa nawakatalia watetezi wa hiyo dhana ya kuwa umeme utashuka bei, na nilikuwa nawashangaa wanapata wapi imani hiyo?
 
Kwani alieanzisha na anaeliendesha kwa sasa ni mtu mmoja?? Ungeeleweka kama alieanzisha ndo akawa analiendesha,, wengine wamedandia kwa mbele tu
Kwani nchi ni mtu au mipango ya serekali? Au huyo aliyeanzisha ujenzi alikuwa anajenga hilo bwawa kwa mshahara wake, na angeliendesha kwa mtazamo wake binafsi?

Tubakie hapo hapo unapotaka kujifichia. Aliyenunua ndege ndio huyohuyo aliyeanzisha ujenzi wa hilo bwawa, mbona nauli ya ndege zake haikuwa ndogo kama fastjet, ili tuone angekuwepo bei ya umeme ingeshuka?
 
Umeme haushuki bei sio kwa sababu haiwezekani, ni kwa vile serikali sikivu ya ccm ieamua kwa dhati kabis kuwaongezea wananchi wake gharama za malipo/matumizi ya umeme, kwamba umeme uwe anasa kama anasa zingine tu.

Kwa namna ambavyo wanakopa bila mipango, kwa namna ambavyo wnatafuta pesa za kuiba kura next yr kwa namna ambavyo wanafisadi nchi, hakuna uwezekano wowote wa kushusha gharama zozote zile, iwe umeme, maji, kuwekeza kwa afya nk.

Swala sio wao kushindwa, shida ni kutaka kula, kushiba na kuvimbiwa.
 
Hadi gharama za ujenzi zirudi kwanza baada ya zitabaki gharama za uendeshaji tu hapo ndio bei ya umeme itashuka
Kama gharama za ujenzi zirudi ndio bei ishuke mbona wewe daraja la kigamboni unaendelea kutulipisha kila tunapopita,unataka kutudanganya since 2015 mpaka leo gharama za ujenzi wako bado azijarudi!?
 
Wakati ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere unaanza, watetezi wake walikuwa wanatoa mishipa ya shingo kuwa bwawa hilo likianza kazi umeme utashuka bei. Nikawa nasema miaka yote tumekuwa tukitumia umeme wa maji, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei rahisi, maana sababu ya umeme kuwa ghali hapa nchini haiendani na gharama za uzalishaji, bali sababu nyingine kabisa.

Watetezi wakawa wanasema gharama kubwa haiwezi kupungua kwa kutumia umeme wa mafuta. Wakajiapiza umeme wa maji ukianza automatically bei itashuka.

Wakati umefika na kile nilichosema kinaonekana. Bwawa limeanza kazi, umeme unazidi kupanda bei, na kibaya zaidi bado sio wa uhakika maana mgao bado upo, hata kama sio kwa kiwango kikubwa. Kwenye hili la bei wote ni mashahidi kwa walioanza kununua umeme hivi karibuni. Na hapo bado.

Paskali Mayalla Choicevariables, Lucas Mwashamba
Tatizo lako ni kuwa kila kilichoanzishwa na JPM, kwa vile ulimchukia huwa unapenda kukikosoa na kuweka lawama kwake ingawa hatupo naye
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Aisee Kazi ipo ....., Hivi unapouziwa perfume laki moja na kununua nanasi tshs 500 inamaanisha gharama za kutengeneza hio perfume ni kubwa kuliko nguvu kazi ya kufanikisha hilo nanasi ?
Mfano wako ni irrelevant maana nanasi na umeme zipo kwenye market structure tofauti kabisa ndio maana hata Ferry, Umeme competition Law ni tofauti na hizo perfect competition markets za mananasi et al. Meaning kutengeneza unit moja ya umeme kuna gharama nyingi kuliko kuuza nanasi la kwanza.

Baada ya kusema hayo operation cost za Bwawa ni kubwa so variable costs zinaongezeka. Kingine Tanesco hiyo hiyo inauza umeme chini ya bei ya soko so inategemea ruzuku wakati mwingine kufidia bei ya chini ila wakisema wauze bei ya soko kwa kuweka gharama zao zote unit Inauzwa hata Shs 500!!

So sio kweli bei itawahi kushuka unless tubakie na bwawa la Nyerere pekee tufunge mabwawa mengine yoteee plus umeme wa gesi tuache kabisa. Ili cost ziwe za JHNEP hapo pengine bei itashuka maana variable cost na fixed pia zitapungua.
 
Wakati ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere unaanza, watetezi wake walikuwa wanatoa mishipa ya shingo kuwa bwawa hilo likianza kazi umeme utashuka bei. Nikawa nasema miaka yote tumekuwa tukitumia umeme wa maji, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei rahisi, maana sababu ya umeme kuwa ghali hapa nchini haiendani na gharama za uzalishaji, bali sababu nyingine kabisa.

Watetezi wakawa wanasema gharama kubwa haiwezi kupungua kwa kutumia umeme wa mafuta. Wakajiapiza umeme wa maji ukianza automatically bei itashuka.

Wakati umefika na kile nilichosema kinaonekana. Bwawa limeanza kazi, umeme unazidi kupanda bei, na kibaya zaidi bado sio wa uhakika maana mgao bado upo, hata kama sio kwa kiwango kikubwa. Kwenye hili la bei wote ni mashahidi kwa walioanza kununua umeme hivi karibuni. Na hapo bado.

Paskali Mayalla Choicevariables, Lucas Mwashamba
Aliyeanzisha ujenzi wa bwawa la Nyerere Ili Tanzania iwe na umeme wa uhakika na bei nafuu ameshakufa

Hawa viongozi waliobakia hayo mambo hawayajui Wala hawakuwahi kuwaza vichwani mwao

Hivyo swali lako hauwezi kupata majibu labda Magufuli afufuke
 
Mfano wako ni irrelevant maana nanasi na umeme zipo kwenye market structure tofauti kabisa ndio maana hata Ferry, Umeme competition Law ni tofauti na hizo perfect competition markets za mananasi et al. Meaning kutengeneza unit moja ya umeme kuna gharama nyingi kuliko kuuza nanasi la kwanza.
Hakuna umeme ambao una running costs ndogo duniani kama HEP
Baada ya kusema hayo operation cost za Bwawa ni kubwa so variable costs zinaongezeka.
In comparison to what ? Kununua mafuta na kuwasha generator ?
Kingine Tanesco hiyo hiyo inauza umeme chini ya bei ya soko so inategemea ruzuku wakati mwingine kufidia bei ya chini ila wakisema wauze bei ya soko kwa kuweka gharama zao zote unit Inauzwa hata Shs 500!!
Moja umeme / Nishati ni Huduma na sio money making scheme; mbili kama hivi sasa wananunua mafuta kwa dalali ili wawashe generator ili wakuuzie wewe umeme na umeme huo mpaka sasa hivi tunapata nusu; Je wakiweza kuzalisha wenyewe bila kununua kwa dalali na kuongeza uzalishaji mara mbili bei inabidi ipande au ishuke ? Na hio Tshs 500/ umeitoa wapi hewani ?

Ni kwamba HEP maji yana potential energy sasa kama hio PE ni 1000 Units uzitumie au usizitumie either zitapotea bure au utazifanyie kazi (workdone)..., Ndio maana muhenga alijesemea In Abundance of Water a Fool is Thirsty....
So sio kweli bei itawahi kushuka unless tubakie na bwawa la Nyerere pekee tufunge mabwawa mengine yoteee plus umeme wa gesi tuache kabisa. Ili cost ziwe za JHNEP hapo pengine bei itashuka maana variable cost na fixed pia zitapungua.
Hapa sidhani hata kama wewe binafsi unaweza ukajielewa.... Haya sio mashindano ya baina ya nani na nani anatoa zaidi bali ni kuwa na as much energy as possible na ukifanya hivyo economy of scale (wateja wengi wakitoa kidogo kidogo utapata kingi) na kumbuka all these are under one entity ambayo ni Tanesco (kwahio Bwawa linaweza kutumika kama muhimili wa energy MIX chanzo chochote kama ni cheaper kinaunganishwa na BWAWA nadhani ili kupata concept nzima pitia hapa

Soma post yangu vizuri, mimi sikuwahi kuamini ule utetezi wa kuwa umeme wa maji utakuwa bei rahisi, maana tumekuwa tukitumia umeme wa maji miaka yote, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei nafuu. Nilikuwa nawakatalia watetezi wa hiyo dhana ya kuwa umeme utashuka bei, na nilikuwa nawashangaa wanapata wapi imani hiyo?
Kama hujawahi kutetea sasa kwanini ufikirie kuwa umeme wa maji utakuwa rahisi kwa Watanzania, au huelewi unachokiandika.

Umeme wa maji kweli ni rahisi sana kuuzalisha kulinganisha na nishati zingine kasoro nuclear.

Uzalishaji kushuka gharama haimaanishi kuwa mtumiaji wa mwisho atapewa unafuu wa ghafla moja. Kwanza kuna kujitosheleza kibajeti, tukishajitolesheza hapo ndipo watumiaji wa kila huduma zitashuka bei kwa kiwango fulani.

Namaanisha ytuzalishe mapato zaidi ndiyo tupate unafuu wa maisha. Itakuwa ni akili ya kijinga bajeti ukope halafu ushushe mapato yako.
 
Aisee Kazi ipo ....., Hivi unapouziwa perfume laki moja na kununua nanasi tshs 500 inamaanisha gharama za kutengeneza hio perfume ni kubwa kuliko nguvu kazi ya kufanikisha hilo nanasi ?

Issue ni kwamba kumalizika kwa Bwawa uzalishaji unatakiwa uwe zaidi ya mara mbili na uendeshaji unapungua sababu overheads za kununua mafuta kwa madalai zinaondoka.....

Sasa kama hio faida inaamuliwa kuliwa na walamba asali hapo katikati hio ni issue nyingine wala haimaanishi kwamba uongozi wenye busara usingeweza kupunguza bei kwenye hii huduma

Sasa mtu mwenye busara angehoji iweje production iongezeke na uendeshaji (gharama zipungue) na bado bei ipande ? Na sio kukubaliana bei inayoletwa mezani kwa ngonjera yoyote ile

Una akili sana mkuu , nyumbu hawatakuelewa
 
Soma post yangu vizuri, mimi sikuwahi kuamini ule utetezi wa kuwa umeme wa maji utakuwa bei rahisi, maana tumekuwa tukitumia umeme wa maji miaka yote, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei nafuu. Nilikuwa nawakatalia watetezi wa hiyo dhana ya kuwa umeme utashuka bei, na nilikuwa nawashangaa wanapata wapi imani hiyo?
Ni sahihi bei kutokushuka au ni janja janja tu ya walioshika hatamu ??
 
Wakati ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere unaanza, watetezi wake walikuwa wanatoa mishipa ya shingo kuwa bwawa hilo likianza kazi umeme utashuka bei. Nikawa nasema miaka yote tumekuwa tukitumia umeme wa maji, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei rahisi, maana sababu ya umeme kuwa ghali hapa nchini haiendani na gharama za uzalishaji, bali sababu nyingine kabisa.

Watetezi wakawa wanasema gharama kubwa haiwezi kupungua kwa kutumia umeme wa mafuta. Wakajiapiza umeme wa maji ukianza automatically bei itashuka.

Wakati umefika na kile nilichosema kinaonekana. Bwawa limeanza kazi, umeme unazidi kupanda bei, na kibaya zaidi bado sio wa uhakika maana mgao bado upo, hata kama sio kwa kiwango kikubwa. Kwenye hili la bei wote ni mashahidi kwa walioanza kununua umeme hivi karibuni. Na hapo bado.

Paskali Mayalla Choicevariables, Lucas Mwashamba
Kushuka kwa bei ya umeme ndio ulikuwa mpango wa Magufuli..sasa ukituuliza tuko wapi wakati unajua mbeba maono alishakufa na maono, huo ni wehu..ndio maana tulikuwa tukiwaeleza Magu ni one man army mkawa hamtuelewi..haya sasa kawaachia hapo mnabaki mnapiga kelele tu..hilo bwawa si mrefu atapewa mwekezaji toka oman awauzie umeme.
 
Back
Top Bottom