Wako wapi wale waliokuwa wanatetea umeme wa maji utakuwa bei rahisi?

Wako wapi wale waliokuwa wanatetea umeme wa maji utakuwa bei rahisi?

Kifupi tu kodi zote za umeme;
VAT : 18%
REA : 1%
EWIRA : 3%
Jumla 22%
Ongeza kodi ya jengo 2,000 p/m
Unit moja ya umeme wa majumbani kwa tariff 1 ni kama 292.74Tsh(Exl. VAT)

Just imagine 292Tsh kwa unit, walau ingeshuka hadi 150Tsh...sema watawala wameamua kutuumiza kwa maslahi yao.
 
Kushuka kwa bei ya umeme ndio ulikuwa mpango wa Magufuli..sasa ukituuliza tuko wapi wakati unajua mbeba maono alishakufa na maono, huo ni wehu..ndio maana tulikuwa tukiwaeleza Magu ni one man army mkawa hamtuelewi..haya sasa kawaachia hapo mnabaki mnapiga kelele tu..hilo bwawa si mrefu atapewa mwekezaji toka oman awauzie umeme.
Nyie ndio wanaccm, na akajaza wabunge wa ccm ili wasimkwamishe. Je hilo bunge la chama kimoja aliloliweka linaloendana na falsafa zake nalo limezikwa naye?

Isitoshe yeye ndio aliyenunua ndege, mbona hazikuwa na nauli ndogo kama ilivyokuwa fastjet, ili tujue kwenye miradi yake bei ingekuwa nafuu?
 
Nimecheka kwa nguvu, ambao kwenye gas tusingeweza kuupata umeme wa uhakika, ila kwenye maji tungepata. Lakini hata hivyo mbona bado unakatika hovyo?
Tumeupata pia kwenye maji wakati upinzani wa Kenya ukiwa unakuja hoja reasonable upinzani wa Tanzania unakuja na hoja za kitoto toto na badae wanalalamika kwanini watz hatuwasapoti
 
Kama hujawahi kutetea sasa kwanini ufikirie kuwa umeme wa maji utakuwa rahisi kwa Watanzania, au huelewi unachokiandika.

Umeme wa maji kweli ni rahisi sana kuuzalisha kulinganisha na nishati zingine kasoro nuclear.

Uzalishaji kushuka gharama haimaanishi kuwa mtumiaji wa mwisho atapewa unafuu wa ghafla moja. Kwanza kuna kujitosheleza kibajeti, tukishajitolesheza hapo ndipo watumiaji wa kila huduma zitashuka bei kwa kiwango fulani.

Namaanisha ytuzalishe mapato zaidi ndiyo tupate unafuu wa maisha. Itakuwa ni akili ya kijinga bajeti ukope halafu ushushe mapato yako.
Naona kama umeparamia hoja yangu bila kuisoma na kuielewa. Tazama kichwa cha uzi wangu, ujipime na unachoongea hapa. Ama umeanza kunywa pombe kama sio kuvuta shisha? Mimi nawataka waliosema bwawa likianza kazi umeme utakuwa nafuu wajitokeze maana walisema umeme wa gas ni ghali. Sasa wewe hata sijui unanaimbia nini?
 
Tumeupata pia kwenye maji wakati upinzani wa Kenya ukiwa unakuja hoja reasonable upinzani wa Tanzania unakuja na hoja za kitoto toto na badae wanalalamika kwanini watz hatuwasapoti
Yaani wala hujajibu hoja, naona unachomeka habari za Kenya huku huna majibu. Narudia swali, watetezi wa umeme wa maji v/s gas mlisema umeme wa maji utashusha gharama, ila gas bei itakuwa juu. Achana na habari za Kenya maana ziko nje ya uwezo wako, sema kwanini bei ya umeme inazidi kupaa. Ukiweza kutoa ufafanuzi wa hilo, ndio ulete hayo ya Kenya sasa.
 
Maswali hayo matatu yangewezekana angekuwa hai, nina imani angekuwa hai nchi yetu tungeitazama kwa namna tofauti sana.
Kwahiyo nchi hii haina mipango, bali inategemea utashi wa rais aliyeko madarakani? Kama ni hivyo hiyo tume ya mipango ni ya nini?

Ndege zilikuja wakati wake, na kipindi hicho fastjet ilikuwepo kabla ya yeye kuihujumu. Mbona ndege zake hazikuwa na nauli nafuu kulinganisha na fastjet ili huu utetezi wako upate nguvu?
 
Yaani wala hujajibu hoja, naona unachomeka habari za Kenya huku huna majibu. Narudia swali, watetezi wa umeme wa maji v/s gas mlisema umeme wa maji utashusha gharama, ila gas bei itakuwa juu. Achana na habari za Kenya maana ziko nje ya uwezo wako, sema kwanini bei ya umeme inazidi kupaa. Ukiweza kutoa ufafanuzi wa hilo, ndio ulete hayo ya Kenya sasa.
Huna hoja mzee baadala ya kulalamika kwanini Bei ya umeme haijashuka licha bwawa kukamilika wewe unapinga bwawa kujengwa hoji mamlaka inayohusika na Bei za nishati kiukweli kama wapinzani tutakuwa na hoja za kitoto kama hizi sijui hata tukishika Dora tuiendeshaji nchii na ni utoto utoto wa kifikra
 
Gharama ni wakati wa kufunga tu. Baada ya hapo ni mpaka betri itakapochoka ndipo ubadilishe. Hakuna sijui umeme umekatika, sijui kulipishwa 2000 kila mwezi! Achilia mbali kununua hizo units kwa bei iliyochangamka.
Gharama ya wakati wa kufunga, ukiigawa na kwa time frame ya matumizi, unaweza kuta production cost ya kilowatt hour moja ipo juu sana. Hii ya kilamwezi 2000/- ni longolongo za hao mnaowatetea tu..!! Na ndiyo maana kila mmoja anasema yeye hahusiki nayo..!! Siyo sehemeu ya gharama za ujenzi wala uendeshaji
 
Tupate umeme mwingi zaidi ya 2,115m, na umeme wa uhakika maana umeme wa maji tuliambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Chama kilichosifia kutotumia umeme wa maji na kuhamia kwenye gas, ndio kilichosifia maji tena bila kujali mabadaliko ya tabia nchi. Kama una akili hoja yangu iko wazi.
Duniani kote sasa hivi wanawekeza zaidi kwenye renewable energy. Hata magari yayotengenezwa sasa ni ya umeme kupunguza uchafuzi wa hewa.
 
Huna hoja mzee baadala ya kulalamika kwanini Bei ya umeme haijashuka licha bwawa kukamilika wewe unapinga bwawa kujengwa hoji mamlaka inayohusika na Bei za nishati kiukweli kama wapinzani tutakuwa na hoja za kitoto kama hizi sijui hata tukishika Dora tuiendeshaji nchii na ni utoto utoto wa kifikra
Ngoja nikuweke pazuri, mimi nilipinga bwawa kujengwa kwa hoja. Kwanza nilisema tulikopa $1.3b kama 3t+ ili kujenga bomba la gas. Tuliimbishwa kama watoto wadogo kuhusu umeme wa gas na faida zake. Ama umeshau maneno kuwa umeme wa gas ukianza mgao itakuwa historia? Kumbuka mgao uliokuwepo tuliambiwa vyanzo vya maji matatizo yake ni mabadaliko ya tabia nchi. Ahadi ya umeme wa gas ilikuwa ni kuzalisha 5,000m na kuuza nje ya nchi. Kila mtu akakamata hiyo chorus kwa lazima au vinginevyo.

Cha kushangaza chama kile kile kilichotuimbisha kuhusu umeme wa gas, na tatizo la mabadaliko ya tabia nchi kuachana na umeme wa maji kabla ya 2015, wakawa kimya kabisa tulipoambiwa baada ya 2015 kuwa sasa tunahamia umeme wa maji! Hapa hapakuwa na utetezi wa mabadiliko ya tabia nchi tena, na tukaambiwa umeme wa maji ni gharama nafuu. Na tutawekeza 7t+ ili kupata 2,115m kwenye maji! Wenye akili zetu tukahoji kwanini 7t ipelekwe yote kwenye maji ambako kuna tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ili kuzalisha 2,115m, na kuachana na gas yenye ahadi ya kuzalisha 5,000m, huku tukiwa tumeshakopa $1.3b, na bomba la gas tayari liko hapa Dar?

Sasa achana na mambo yote unayojaribu kurukia, toa ufafanuzi wa kina kwani umeme wa maji utakaozalisha 2,115m kwa 7t+, na kuacha umeme wa gas ambao umeshakula 3t+ na miundombunu iko hapa Dar tayari, na lengo ilikuwa kuzalisha 5,000m. Je hiyo 7t+ tusingeweza kupata umeme zaidi ya hiyo 2,115m kwenye gas? Ukishindwa muite Kafulila maana ndio mnamtegemea siku hizi kwa ufafanuzi wa mambo makubwa. Nchimbi, Makala, Makonda majibu ya haya hawana maana wao ni propaganda tu. Hangaika na hoja hii ama ukae kimya.

NB: Zingatia kisingizio cha umeme wa maji kuwa nafuu hicho kimedhihirika sio kweli.

Paskali Mayalla, nguruvi3, bams, zitto junior
 
Duniani kote sasa hivi wanawekeza zaidi kwenye renewable energy. Hata magari yayotengenezwa sasa ni ya umeme kupunguza uchafuzi wa hewa.
Safi, pitia post yangu namba 72, kisha uje na maelezo mazuri. Hayo ya dunia yote yaache kwanza, kisha tutakuja kwenye hitimisho baaada ya ufafanuzi wa hoja zangu namba 72.
 
Tatizo ni upeo,nchi yetu ina wajinga wengi,wanaotakiwa kuelemishwa kutambua jema na baya.

Ni kweli hydo power ni nafuu sana kuliko umeme wa mafuta,ila Nchi kama Saudia mafuta ni sawa na bei ya hewa yaani ni karibu na bure.
Huku kwetu tulitegemea umeme wa maji uwe nafuu kama enzi za Mwalimu Nyerere, RIP.
lakini baada ya kuondoka umeme ukakaondoka pia.
Tukaja na Gesi ndio tena mbwa koko tuliowalipia elimu ya ubobezi wa mafuta wakatukaaga asubuhi mapema na fake advice.
Mjomba alifikiri umeme wa maji utakuwa nafuu akaanza kujenga bwa la Nyerere.
Lakini controller ni wale wale walanguzi wa siasa na uchumi ndio wanapanga bei.
Tuje na sheria ya kuwaasi au kuwafukia wakiwa hai
 
Ngoja nikuweke pazuri, mimi nilipinga bwawa kujengwa kwa hoja. Kwanza nilisema tulikopa $1.3b kama 3t+ ili kujenga bomba la gas. Tuliimbishwa kama watoto wadogo kuhusu umeme wa gas na faida zake. Ama umeshau maneno kuwa umeme wa gas ukianza mgao itakuwa historia? Kumbuka mgao uliokuwepo tuliambiwa vyanzo vya maji matatizo yake ni mabadaliko ya tabia nchi. Ahadi ya umeme wa gas ilikuwa ni kuzalisha 5,000m na kuuza nje ya nchi. Kila mtu akakamata hiyo chorus kwa lazima au vinginevyo.

Cha kushangaza chama kile kile kilichotuimbisha kuhusu umeme wa gas, na tatizo la mabadaliko ya tabia nchi kuachana na umeme wa maji kabla ya 2015, wakawa kimya kabisa tulipoambiwa baada ya 2015 kuwa sasa tunahamia umeme wa maji! Hapa hapakuwa na utetezi wa mabadiliko ya tabia nchi tena, na tukaambiwa umeme wa maji ni gharama nafuu. Na tutawekeza 7t+ ili kupata 2,115m kwenye maji! Wenye akili zetu tukahoji kwanini 7t ipelekwe yote kwenye maji ambako kuna tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ili kuzalisha 2,115m, na kuachana na gas yenye ahadi ya kuzalisha 5,000m, huku tukiwa tumeshakopa $1.3b, na bomba la gas tayari liko hapa Dar?

Sasa achana na mambo yote unayojaribu kurukia, toa ufafanuzi wa kina kwani umeme wa maji utakaozalisha 2,115m kwa 7t+, na kuacha umeme wa gas ambao umeshakula 3t+ na miundombunu iko hapa Dar tayari, na lengo ilikuwa kuzalisha 5,000m. Je hiyo 7t+ tusingeweza kupata umeme zaidi ya hiyo 2,115m kwenye gas? Ukishindwa muite Kafulila maana ndio mnamtegemea siku hizi kwa ufafanuzi wa mambo makubwa. Nchimbi, Makala, Makonda majibu ya haya hawana maana wao ni propaganda tu. Hangaika na hoja hii ama ukae kimya.

NB: Zingatia kisingizio cha umeme wa maji kuwa nafuu hicho kimedhihirika sio kweli.

Paskali Mayalla, nguruvi3, bams, zitto junior
Kwani tumeacha kuzalisha umeme wa gesi kama umeme wa gas unazalishwa na umeme wa maji unazalishwa Sasa kosa liko wapi?
 
Kwani tumeacha kuzalisha umeme wa gesi kama umeme wa gas unazalishwa na umeme wa maji unazalishwa Sasa kosa liko wapi?
Ndio maana nikasema , kwanini tuingize 7t yote kwenye maji, badala ya kupeleka nusu ya hiyo kwenye gas, na kisha hela nyingine itumike kwenye maendeleo. Kumbuka ni pesa ya mkopo. Je huo umeme wa maji tatizo ma mabadiliko ya tabia nchi mmelimaliza?

Hata hivyo nilitegemea utajibu kwa ufasaha maswali yangu gas v/s hydro, na why hela nyingi kwenye hydro tu. Ila majibu yako yanaonyesha ww ni bendera fuata upepo, huna hoja nje ya uliokaririshwa. Muite Kafulila.
 
Back
Top Bottom