Ngoja nikuweke pazuri, mimi nilipinga bwawa kujengwa kwa hoja. Kwanza nilisema tulikopa $1.3b kama 3t+ ili kujenga bomba la gas. Tuliimbishwa kama watoto wadogo kuhusu umeme wa gas na faida zake. Ama umeshau maneno kuwa umeme wa gas ukianza mgao itakuwa historia? Kumbuka mgao uliokuwepo tuliambiwa vyanzo vya maji matatizo yake ni mabadaliko ya tabia nchi. Ahadi ya umeme wa gas ilikuwa ni kuzalisha 5,000m na kuuza nje ya nchi. Kila mtu akakamata hiyo chorus kwa lazima au vinginevyo.
Cha kushangaza chama kile kile kilichotuimbisha kuhusu umeme wa gas, na tatizo la mabadaliko ya tabia nchi kuachana na umeme wa maji kabla ya 2015, wakawa kimya kabisa tulipoambiwa baada ya 2015 kuwa sasa tunahamia umeme wa maji! Hapa hapakuwa na utetezi wa mabadiliko ya tabia nchi tena, na tukaambiwa umeme wa maji ni gharama nafuu. Na tutawekeza 7t+ ili kupata 2,115m kwenye maji! Wenye akili zetu tukahoji kwanini 7t ipelekwe yote kwenye maji ambako kuna tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ili kuzalisha 2,115m, na kuachana na gas yenye ahadi ya kuzalisha 5,000m, huku tukiwa tumeshakopa $1.3b, na bomba la gas tayari liko hapa Dar?
Sasa achana na mambo yote unayojaribu kurukia, toa ufafanuzi wa kina kwani umeme wa maji utakaozalisha 2,115m kwa 7t+, na kuacha umeme wa gas ambao umeshakula 3t+ na miundombunu iko hapa Dar tayari, na lengo ilikuwa kuzalisha 5,000m. Je hiyo 7t+ tusingeweza kupata umeme zaidi ya hiyo 2,115m kwenye gas? Ukishindwa muite Kafulila maana ndio mnamtegemea siku hizi kwa ufafanuzi wa mambo makubwa. Nchimbi, Makala, Makonda majibu ya haya hawana maana wao ni propaganda tu. Hangaika na hoja hii ama ukae kimya.
NB: Zingatia kisingizio cha umeme wa maji kuwa nafuu hicho kimedhihirika sio kweli.
Paskali Mayalla, nguruvi3, bams, zitto junior