Wako wapi wale waliokuwa wanatetea umeme wa maji utakuwa bei rahisi?

Mradi utaisha kwa 100%, alafu utaingizwa gridi ya taifa utaenda kureplace baadhi ya uzalishaji ikiwemo mafuta na gesi, hapo ndio hili swali linapaswa kuja. Sasa hivi bado mapema
Ccm ni ile ile ooh ni ile ile
 
Haya malalamiko ni kwa sababu Watanzania hawajazoea kulipa gharama halisi za umeme.
Ningekubaliana na wewe kama kampuni kama IPTL ilichokuwa inalipwa kilikuwa kinaendana na uhalisi wa inachozalisha.

Tanzania is a different country linapokuja suala la ulaji.
 
Kuna sehemu unakosea, nimekujibu mradi haujakamilika kwa 100% hivyo huwezi sema mbona Bei haijapungua. Ilipaswa mradi uishe megawatt zote ziingie grid ya taifa iende kureplace hizo aina nyingine za uzalishaji ndio hapo sasa tutaanza luhojj

Vyanzo vingine vimepungua mfano umetolea iptl, nikamuuliza unajua mbadala wake gharama zipoje? Mfano tu umeme wa mafuta uzalishaji uliongezeka nakufikia megawatt 80.

Unasema umeme wa majenereta umepungua, unaposema umeme wa majenereta unamaanisha nn? Maana mm nitakuambia haujapungua bali umeongezeka. Twende kwa takwimu sasa
 
Yawezekana kama chuma cha pua Magufuli angekuepo angetimiza ahadi yake ya umeme kupungua bei kwa maana ya bei ya unit, usisahau ni kipindi chake alishusha gharama za maunganisho ya umeme kutoka laki 3 na 20 hadi elfu 27 kwa maeneo ya mjini lakini yule bibi chaudele akaja kufanya anavyo jua yeye
 
Mimi niliwahi tetea lini? Mimi ndio niliqaambia ukweli ambao Maharage Chande na January walikuwa wazi.
 
The oversimplification aside, lini umeona uwekezaji mkubwa hivi umefanywa ili kuleta nafuu Kwa mlaji? Sizungumzii maneno wanayotumiaga ku 'uza' mradi kwa umma, kama Una mfano wa mradi halisi na matokeo yakawa kama yaliyoahidiwa. I am genuinely curious
 
Kwa Tanzania nothing will work especially now watu hawana machungu na nchi bali matumbo yao..., ila sababu Tanzania kitu hakifanyiki sababu ya utendaji mbovu haimaanishi kitu kile / idea ni mbaya bali utendaji ndio mbaya.

Kwahio wewe ukifanya hesabu moja kujumlisha moja ukapata tatu haimaanishi kwamba jibu sio mbili wala haimaanishi tuache kujumlisha bali wewe ndio uache kujumlisha vibaya
 
Huzuni hazikuwahi kuondoka wakati wa Magufuli, bali hakukuwa na uhuru wa kusema madhila ya wananchi, maana ilikuwa marufuku kutangaza jambo negative wakati wake. Wakati wa utawala wake hatukuwa nje ya nchi boss. Ndio maana nimekupa mfano wa nauli za ndege akiwepo, mbona hazikuwahi kushuka? Ajira hazikuwepo nk. Ni kweli alifanya project kubwa kwa mikopo, na akahakikisha media inatangaza hiyo kwa nguvu zote, lakini sio unafuu kwa maisha ya wananchi. Kikubwa alichofanya ni kupunguza kelele kwa wamachinga baada ya kuruhusu biashara holela.
 
Ndio nimeomba mfano wa mradi au wakati ambapo it worked. Maana ili uwe hopeful aidha umewahi ona matokeo, au una taarifa za ndani. Kwa umri wangu nimesikia ya mkonga wa taifa, ving'amuzi, SGR, ndege, mwendokasi, ninayoikumbuka kwa haraka.
 
Wapo humu humu kapuni wamekunja mikia ka mbwa koko!
 
Kuna uzi mmoja nilichangia kuwaambia Watanzania wajiandae kulipia umeme zaidi. Watu hawakuelewa.

Juzi kuna mdau kafukua kakubali utabiri wangu.
Nakumbuka sana uzi ule. Leo watetezi kwa aibu wanasema muanzilishi hayupo ndio maana tunapigwa! Nawauliza kwenye ndege alikuwepo, mbona hakushusha nauli iwe chini ya fastjet, hawataki kurudi!

Nilisema hakuna uwezekano umeme kuwa bei nafuu maana ni fedha za mkopo, na sababu nyinginezo. Watetezi walisema ni fedha za ndani kama walivyokuwa wanalishwa propaganda!
 
Siyo kwa ccm ya huyu chura kiziwi!

Chura kiziwi anatafuta wapi pa kukamua alafu akupunguzie wewe gharama za umeme?
 
No ! Hali ilikuwa na fuuu na furaha ilikuwepo ndio maana hata leo ukiweka pol ya marais wote wanne Magufuli atapata asilimia 70+ na samia hafikishi asilimia hata 10 ya kura zote.
Nchi kipindi cha Magufuli ilikuwa ina muelekeo,wananchi tulikuwa tunajua hiki ni hiki sio kile... na kwanini ni hiki.
Tulishaanza kujitambua na hata wazungu walikuwa hawaji kichwa kichwa inabidi wawaze vizuri kuleta proposal ya jambo lolote maana nchi ilikuwa inaongozwa na mtu makini.
Yule baba alikuwa mzalendo nakwambia tusingekuwa tunalalamika mambo madogo kama gharama za umeme kupanda.
Hapa shida ya sasa ni roho mbaya,mama hana huruma na wananchi wake.
 
Tatizo la Africa / Tanzania ni vipaumbele & wizi

Hii methali huwa ninaupenda.

Mfano kuna haja gani ya mkurugenzi , DC , RC katika mikoa 26 yote kutembelea gari za milioni 500+ .

Je gharama za kuhudumia hizo gari , misafara isiyo na tija , matengenezo na mafuta nani anafanya??

Ukiona hilo utajua mzigo unamuangukia mwananchi wa chini hata hicho anachokamuliwa kikitoka bado [ mafisadi/majizi] yanakitolea mate na yanakikwapua ushahidi ni upi jibu ni ripoti ya CAG!

Je ikifikia hatua matumizi ya anasa kama hayo tu ya gari tuseme watembelee gari tu za milioni 10-20 nini kitapungua ?

Pesa kiasi gani itakuwa imeokolewa kwenye gari zinazohitaji pesa nyingi kuzitunza !

Hebu fikiria hayo mamilioni yakiokolewa na kwenda kuwa "subsidized " kwenye mradi wa umeme watu wapate umeme kwa gharama nafuu utahitaji kukodi vikundi vya wasifiaji eti " Mama anaupiga mwingi"??

Juzi tu hapo tumeona vilio vya kodi ya jengo kwenye umeme imeongezeka 500/= tu imekuwa story ya siku.

Watawala hawajali maana wananchi sio kipaumbele chao na hizo gharama watawala hao hata hawajui zinalipwaje maana ni jasho la wananchi linawalipia pesa ya ununuI wa gari, bili za maji, umeme, usafiri, posho, mishahara.

Halafu baadae mtu anakuja kusema "Mama ametoa bilioni......"

Bajeti ukiona pesa za maendeleo ni kiduchu ila "matumizi mengine" ni rundo la pesa kwenye mengine humo ndio wezi wanajipakulia.

Kiufupi watawala wanaiibia nchi kwa kuwarubuni wananchi kuwa wako vizuri kwa kuwapa vitu wasivyo na uhitaji navyo huku vilivyo na uhitaji hawapewi.

Niishie hapo kwa leo.
 
Hata angepata kura 100% dhidi ya marais wengine, hiyo haimaanishi kuwa maisha wakati wake yalikuwa nafuu. Na sidhani hata angekuwepo yangekuwa na afadhali maana aliingia mikopo mingi kwa pupa inatutesa hadi sasa. Haya matozo, sijui malimbikizo ni kuwahi marejesho ya mikopo ya wakati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…