Wako wapi wale wanawake ambao walikuwa tayari kufa kwa ajili ya watoto wao?

Wako wapi wale wanawake ambao walikuwa tayari kufa kwa ajili ya watoto wao?

Nakadori

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,778
Reaction score
21,010
Wakuu habarini za majukumu?

Ninatumaini jitihada za kujipatia mkate wa kila siku zinaendelea salama... Siku ya leo nimeitumia kwa asilimia kubwa hapa stend ya mabasi ya kwenda mkoa baada ya basi nililokuwa ninalisubiria kuchelewa kufika na hivyo nikajikuta nazoeana na baadhi ya abiria niliokuwa nimekaa nao akiwemo baba Agness na Agness mwenyewe. Agness alionekana amevaa mavazi mazuri lakini yamepoteza nuru kwa vile hayasafishwi vizuri...hata nuru yake ya ngozi nyeupe imepotea kutokana na kutoweza kujiogesha vizuri kwa umri wake mdogo, jacket la jeans alilovaa halijafuliwa pia.

Baba Agness alifika jijini akiwa na binti yake wa miaka 10 kufwatilia cheti nadhani ni cha ubatizo wa mwanae baada ya maisha kumshinda hapa jijini na kuhamia Morogoro mjini ambapo anajishuhulisha na kilimo cha bustani. Anadai alishindwa kumuacha peke yake kwani dunia imeharibika na amekuwa akisikia kila siku matukio ya kutisha kuhusu ukatili wanaofanyiwa watoto.

Katika story za hapa na pale akanieleza kwamba mama Agness alimtelekeza Agness akiwa na miaka 3 tu baada ya kumpata mwanaume ambaye wanaishi nae gongolamboto hadi leo na wamefanikiwa kuzaa watoto wengine 3. Na kazi ya malezi ya agness amekuwa akiifanya baba yake kuanzia hapo hadi leo. Anadai mama agness akikuja kumuona mwanae akiwa na miaka saba baada ya baba mtu kumtafuta kwamba wamekuja jijini ili angalau amuone mwanae. Alipokuja alimpatia shilingi mia tano kama zawadi. Baba agness mwenyewe anaonekana msela sana...

Kiuhalisia wanaume sio walezi wa watoto kulingana na maumbile yao. Sasa inakuwaje mwanamke uliyebeba mimba na ukaenda leba uje utelekeze kiumbe katika umri mdogo kiasi hicho? Mbona mama zetu walikuwa tayari kupitia mateso lakini pamoja na yote waling'ang'ana kuwa nasi hadi tukawa watu wazima?? Tulizoea kusikia wanaume ndio wanatelekeza watoto lakini siku hizi wanawake tumekuwa na roho ngumu...unalipa kisasi ambacho kinamuumiza mwanao?

Nimetamani niwe mama wa hiari wa Agness (sio mama wa kambo) ili niwe nae karibu maana anakaribia umri wa usichana na atahitaji mama wa kumshauri na kuongea nae mambo mengi yahusuyo mabadiliko ya mwili wake na mengineyo. Agness mwenyewe ni katoto kazuri sana... na kanaonekana kana upeo mkubwa sana.
Wanawake wenzangu kuliko msumbue kwenye malezi kwa kusingizia wanaume bora msizae kabisa.
 
Wazazi wa wazazi...
Hivi naanzaje kumwambia mama au baba kwamba nimemtupia mwanaume mtoto wa umri huo?
Nadhani mda huo huo nitarudishwa nikamfwate
What if mama Aggy hajasema kwao kama ametelekeza mtoto? au pengine ni mtu wa Pwani/mshwahili haswaa asiyejali lolote maana ye mwwenyewe ukute ni chakaramu tu na mdangaji huko GOMEZ
 
FB_IMG_1655280719573.jpg
 
Tupo,mpaka tone la damu.Nikiwa job wananitesa sana kichwani...nawawaza mno.Ee Mwenyez Mungu niongezee afya nilee wanangu.
 
Sahv ukatili upo 50/50 tena naona wanawake wanakuja Kasi kushinda wanaume.
 
Tupo,mpaka tone la damu.Nikiwa job wananitesa sana kichwani...nawawaza mno.Ee Mwenyez Mungu niongezee afya nilee wanangu.
Yani hata upitie yapi usije ukaacha wanao popote eti unamkomoa mwanaume. Chochote utakachokula na wanao wale hichohicho
 
Yani hata upitie yapi usije ukaacha wanao popote eti unamkomoa mwanaume. Chochote utakachokula na wanao wale hichohicho
Mkuu kama Mungu amekujaalia Fanya jambo kwa huyoo malaika na utabarikiwa
 
Back
Top Bottom