Wako wapi wale wanawake ambao walikuwa tayari kufa kwa ajili ya watoto wao?

Hujaisoma mada bas,Ina kaujumbe ambako ukiongezea tutajifunza kitu
Ooh kweli mada hii, nilikua sijaisoma. Nilidhani ni ile thread ya "wenza kufanana"

Nashukuru kwa kuniita hapa, ngoja nipitie afu nitie neno. (Maada mada za mlengo huu nazipenda sana)
 
Wakuu habarini za majukumu?

Ninatumaini jitihada za kujipatia mkate wa kila siku zinaendelea salama... Siku ya leo nimeitumia kwa asilimia kubwa hapa stend ya mabasi ya kwenda mkoa baada ya basi nililokuwa ninalisubiria kuchelewa kufika na hivyo nikajikuta nazoeana na baadhi ya abiria niliokuwa nimekaa nao akiwemo baba Agness na Agness mwenyewe. Agness alionekana amevaa mavazi mazuri lakini yamepoteza nuru kwa vile hayasafishwi vizuri...hata nuru yake ya ngozi nyeupe imepotea kutokana na kutoweza kujiogesha vizuri kwa umri wake mdogo, jacket la jeans alilovaa halijafuliwa pia.

Baba Agness alifika jijini akiwa na binti yake wa miaka 10 kufwatilia cheti nadhani ni cha ubatizo wa mwanae baada ya maisha kumshinda hapa jijini na kuhamia Morogoro mjini ambapo anajishuhulisha na kilimo cha bustani. Anadai alishindwa kumuacha peke yake kwani dunia imeharibika na amekuwa akisikia kila siku matukio ya kutisha kuhusu ukatili wanaofanyiwa watoto.

Katika story za hapa na pale akanieleza kwamba mama Agness alimtelekeza Agness akiwa na miaka 3 tu baada ya kumpata mwanaume ambaye wanaishi nae gongolamboto hadi leo na wamefanikiwa kuzaa watoto wengine 3. Na kazi ya malezi ya agness amekuwa akiifanya baba yake kuanzia hapo hadi leo. Anadai mama agness akikuja kumuona mwanae akiwa na miaka saba baada ya baba mtu kumtafuta kwamba wamekuja jijini ili angalau amuone mwanae. Alipokuja alimpatia shilingi mia tano kama zawadi. Baba agness mwenyewe anaonekana msela sana...

Kiuhalisia wanaume sio walezi wa watoto kulingana na maumbile yao. Sasa inakuwaje mwanamke uliyebeba mimba na ukaenda leba uje utelekeze kiumbe katika umri mdogo kiasi hicho? Mbona mama zetu walikuwa tayari kupitia mateso lakini pamoja na yote waling'ang'ana kuwa nasi hadi tukawa watu wazima?? Tulizoea kusikia wanaume ndio wanatelekeza watoto lakini siku hizi wanawake tumekuwa na roho ngumu...unalipa kisasi ambacho kinamuumiza mwanao?

Nimetamani niwe mama wa hiari wa Agness (sio mama wa kambo) ili niwe nae karibu maana anakaribia umri wa usichana na atahitaji mama wa kumshauri na kuongea nae mambo mengi yahusuyo mabadiliko ya mwili wake na mengineyo. Agness mwenyewe ni katoto kazuri sana... na kanaonekana kana upeo mkubwa sana.
Wanawake wenzangu kuliko msumbue kwenye malezi kwa kusingizia wanaume bora msizae kabisa.
* The Premium Answer *

Kwanza nianze kwa kusema wanawake wa kileo wameharibiwa na wimbi la usasa. Swala hili ukiliangalia kwa makini utatambua mama Agnes ni mwanamke ngangari, usinibabaishe 50/50 kama mimi nalea na wewe lea huyo mtoto.

Hatujajua sana kuhusu mama Agnes ila nabashiri ni "msomi" flani mwenye "kaupeo" ka haki sawa unyenyekevu na utii ni sifa asizokua nazo mama Agnes kama ambavyo wanawake wengi wa kileo walivyo.

Naungana na mtoa mada wanawake wa kileo hawana upendo na watoto wao walio wengi wanawaza pesa, vyeo nk. Wanazaa watoto na kuwatelekeza kwa mahouse girl, yeye huyo mwendo alfajiri kurudi jioni muda ambao mume nae ndio anarudi. Kama wanaweza kumtelekeza mtoto kwa house girl wanashindwaje kumtelekeza kwa baba wa mtoto.

Mwanamke analea kwa kupiga simu "haloow, amekunywa maziwa ?!" mtoto anamfahamu house girl kuliko mama yake. Enyi wanawake wa kileo upendo sio kumnunulia mtoto midoli na kumuita majina mazuriii kama Sasha au Junior, upendo hudumishwa na malezi na nyie ndio jukumu lenu la asili., kwingine mnapuyanga tu.

Unajua kwanini Mungu aliwapa manyonyo nyie na hakutupa wanaume ?!, ili mlee watoto na sisi tukatafute ili tuwahudumie nyie na watoto. Sasa nyie haki sawa kutwa maofisini hizo kazi zenyewe huko mnavulunda tu hamna ufanisi wala umakini mmekalia umbea na majungu maofisini.
Screenshot_20220406-101705_Chrome Beta.jpg
 
The Premium Answer *

Kwanza nianze kwa kusema wanawake wa kileo wameharibiwa na wimbi la usasa. Swala hili ukiliangalia kwa makini utatambua mama Agnes ni mwanamke ngangari, usinibabaishe 50/50 kama mimi nalea na wewe lea huyo mtoto.

Hatujajua sana kuhusu mama Agnes ila nabashiri ni "msomi" flani mwenye "kaupeo" ka haki sawa unyenyekevu na utii ni sifa asizokua nazo mama Agnes kama ambavyo wanawake wengi wa kileo walivyo.

Naungana na mtoa mada wanawake wa kileo hawana upondo na watoto wao walio wengi wanawaza pesa, vyeo nk. Wanazaa watoto na kuwatelekeza kwa mahouse girl, yeye huyo mwendo alfajiri kurudi jioni muda ambao mume nae ndio anarudi.

Mwanamke analea kwa kupiga simu "haloow, amekunywa maziwa ?!" mtoto anamfahamu house girl kuliko mama yake. Wanawake wa kileo upendo sio kumnunulia mtoto midoli na kumuita majina mazuriii kama Sasha au Junior, upendo hudumishma na malezi na nyie ndio jukumu lenu la asilg.

Unajua kwanini Mungu aliwapa manyonyo nyie na hakutupa wanaume ?!, ili mleo watoto na sisi tukatafute ili tuwahudumie nyie na matoto pia. Sasa nyie haki sawa kutwa maofisini hizo kazi zenyewe huko mnavulunda tu hamna ufanisi wala umakini mmekalia umbea na majungu maofisini.View attachment 2262027
Kuna aspects nakubaliana na wewe na zipo ambazo sitakubaliana na wewe kwenye hoja yako....ngoja nihudumie kwanza family nitarudi
 
Oooh safi sana, hudumia familia mkuu, hongera kwa kuthamini kuhudumia familia kama majuajumu yako ya asili wengi wa wanawake wa kileo hapo wangemuita "dada wa kazi" na kutoa msululu wa maagizo.
 
Nikajua mtoto sijui katupwa mtaroni au katelekezwa kwa bibi yake kumbe yupo na baba yake mzazi!!
Ni baba yake, acha amlee maana ni wajibu wake pia.

Anyway ni story ya upande mmoja hivyo lazima ngoma aivutie kwake.
Kwani huyo baba ameshaoa? Kama bado basi bado haujachelewa kuwa mama yake
Shida sio yupo Kwa baba yake, shida IPO kwenye malezi. Kumbuka huyo ni mtoto wa kike na anaelekea kwenye umri wa kuvunja ungo kuna mambo ya kike ambayo sio rahis Kwa Binti kumwambia mzazi wa kiume na tambua kuwa pia kuna vitu ataitaji kuelekezwa Kwa ukaribu zaid maswala ya uanamke kitu ambacho sio rahis Kwa Binti kumwambia baba yake
 
Wakuu habarini za majukumu?

Ninatumaini jitihada za kujipatia mkate wa kila siku zinaendelea salama... Siku ya leo nimeitumia kwa asilimia kubwa hapa stend ya mabasi ya kwenda mkoa baada ya basi nililokuwa ninalisubiria kuchelewa kufika na hivyo nikajikuta nazoeana na baadhi ya abiria niliokuwa nimekaa nao akiwemo baba Agness na Agness mwenyewe. Agness alionekana amevaa mavazi mazuri lakini yamepoteza nuru kwa vile hayasafishwi vizuri...hata nuru yake ya ngozi nyeupe imepotea kutokana na kutoweza kujiogesha vizuri kwa umri wake mdogo, jacket la jeans alilovaa halijafuliwa pia.

Baba Agness alifika jijini akiwa na binti yake wa miaka 10 kufwatilia cheti nadhani ni cha ubatizo wa mwanae baada ya maisha kumshinda hapa jijini na kuhamia Morogoro mjini ambapo anajishuhulisha na kilimo cha bustani. Anadai alishindwa kumuacha peke yake kwani dunia imeharibika na amekuwa akisikia kila siku matukio ya kutisha kuhusu ukatili wanaofanyiwa watoto.

Katika story za hapa na pale akanieleza kwamba mama Agness alimtelekeza Agness akiwa na miaka 3 tu baada ya kumpata mwanaume ambaye wanaishi nae gongolamboto hadi leo na wamefanikiwa kuzaa watoto wengine 3. Na kazi ya malezi ya agness amekuwa akiifanya baba yake kuanzia hapo hadi leo. Anadai mama agness akikuja kumuona mwanae akiwa na miaka saba baada ya baba mtu kumtafuta kwamba wamekuja jijini ili angalau amuone mwanae. Alipokuja alimpatia shilingi mia tano kama zawadi. Baba agness mwenyewe anaonekana msela sana...

Kiuhalisia wanaume sio walezi wa watoto kulingana na maumbile yao. Sasa inakuwaje mwanamke uliyebeba mimba na ukaenda leba uje utelekeze kiumbe katika umri mdogo kiasi hicho? Mbona mama zetu walikuwa tayari kupitia mateso lakini pamoja na yote waling'ang'ana kuwa nasi hadi tukawa watu wazima?? Tulizoea kusikia wanaume ndio wanatelekeza watoto lakini siku hizi wanawake tumekuwa na roho ngumu...unalipa kisasi ambacho kinamuumiza mwanao?

Nimetamani niwe mama wa hiari wa Agness (sio mama wa kambo) ili niwe nae karibu maana anakaribia umri wa usichana na atahitaji mama wa kumshauri na kuongea nae mambo mengi yahusuyo mabadiliko ya mwili wake na mengineyo. Agness mwenyewe ni katoto kazuri sana... na kanaonekana kana upeo mkubwa sana.
Wanawake wenzangu kuliko msumbue kwenye malezi kwa kusingizia wanaume bora msizae kabisa.
Agness unaongeaga naye?
 
Back
Top Bottom