Wako wapi wale wanawake ambao walikuwa tayari kufa kwa ajili ya watoto wao?

Hujaisoma mada bas,Ina kaujumbe ambako ukiongezea tutajifunza kitu
Ooh kweli mada hii, nilikua sijaisoma. Nilidhani ni ile thread ya "wenza kufanana"

Nashukuru kwa kuniita hapa, ngoja nipitie afu nitie neno. (Maada mada za mlengo huu nazipenda sana)
 
* The Premium Answer *

Kwanza nianze kwa kusema wanawake wa kileo wameharibiwa na wimbi la usasa. Swala hili ukiliangalia kwa makini utatambua mama Agnes ni mwanamke ngangari, usinibabaishe 50/50 kama mimi nalea na wewe lea huyo mtoto.

Hatujajua sana kuhusu mama Agnes ila nabashiri ni "msomi" flani mwenye "kaupeo" ka haki sawa unyenyekevu na utii ni sifa asizokua nazo mama Agnes kama ambavyo wanawake wengi wa kileo walivyo.

Naungana na mtoa mada wanawake wa kileo hawana upendo na watoto wao walio wengi wanawaza pesa, vyeo nk. Wanazaa watoto na kuwatelekeza kwa mahouse girl, yeye huyo mwendo alfajiri kurudi jioni muda ambao mume nae ndio anarudi. Kama wanaweza kumtelekeza mtoto kwa house girl wanashindwaje kumtelekeza kwa baba wa mtoto.

Mwanamke analea kwa kupiga simu "haloow, amekunywa maziwa ?!" mtoto anamfahamu house girl kuliko mama yake. Enyi wanawake wa kileo upendo sio kumnunulia mtoto midoli na kumuita majina mazuriii kama Sasha au Junior, upendo hudumishwa na malezi na nyie ndio jukumu lenu la asili., kwingine mnapuyanga tu.

Unajua kwanini Mungu aliwapa manyonyo nyie na hakutupa wanaume ?!, ili mlee watoto na sisi tukatafute ili tuwahudumie nyie na watoto. Sasa nyie haki sawa kutwa maofisini hizo kazi zenyewe huko mnavulunda tu hamna ufanisi wala umakini mmekalia umbea na majungu maofisini.
 
Kuna aspects nakubaliana na wewe na zipo ambazo sitakubaliana na wewe kwenye hoja yako....ngoja nihudumie kwanza family nitarudi
 
Kuna aspects nakubaliana na wewe na zipo ambazo sitakubaliana na wewe kwenye hoja yako....ngoja nihudumie kwanza family nitarudi
Oooh safi sana, hudumia familia mkuu, hongera kwa kuthamini kuhudumia familia kama majuajumu yako ya asili wengi wa wanawake wa kileo hapo wangemuita "dada wa kazi" na kutoa msululu wa maagizo.
 
Shida sio yupo Kwa baba yake, shida IPO kwenye malezi. Kumbuka huyo ni mtoto wa kike na anaelekea kwenye umri wa kuvunja ungo kuna mambo ya kike ambayo sio rahis Kwa Binti kumwambia mzazi wa kiume na tambua kuwa pia kuna vitu ataitaji kuelekezwa Kwa ukaribu zaid maswala ya uanamke kitu ambacho sio rahis Kwa Binti kumwambia baba yake
 
Agness unaongeaga naye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…