Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!
Nape Nnauye , Habari za siku mkubwa.
Kwanza hakuna aliyesema unnayoyasema hapa, ila malalamiko ni mabaraza ya katiba yaliingiliwa na makada wa CCM mmoja wapo ni mama yangu, dada yangu Asha rose Migiro na wewe. Mliwatengeneza watu wa kuingia kuyapigia kura haya maoni. Naomba utafute matamko ya wote waliopinga utajua wapi walipinga. Mpaka sasa tunapinga upatikanaji wa watu watakao jadili na kuyapitisha haya maoni. Je kweli watayakubali wakati wengi ni makada wa kuingizwa wa CCM?
Tutafurahi wengi kama mtawaelekeza makada wengi kuzingatia maoni ya watanzania.
Maoni yangu binafsi sikubaliani na uwakilishi wa wanaume na wanawake kwenye majimbo utaongeza gharama kubwa sana za kuendesha bunge. Kama nimeelewa vyema yaani kuwe na wawakilishi wa kike na kiume kwenye jimbo moja. No huu utakuwa ni mzigo kwa walipa kodi. yaani majimbo 239 yatoe wabunge 478??? come on haiwezekanai. ni wengi mno ukilingisha na uwezo wa nchi. Nilitegemea tume ingepunguza majimbo ya uchaguzi na kufikia walau 70 au 100. ya kudumu.
Nape tujadili hizi rasimu Tanzania ni yetu wote, wewe utapita, Jk atapita, Lowasaa atapita , Membe Atapita ila Tanzania bado tunayo sana, msifikiri ninyi viongozi wa sisasa mna maana sana zaidi ya maisha yetu la hasha ninyi mnatetea ajira tu hamna la maana mnalilifanya, hamtetei taifa, wananchi wala ustawi wa tanzania. hamna uchungu na uhalisia wa maisha magumu ya Mtanzania.
ndio maana hamjali kushuku kiwango cha elimu manapendekeza utumbo wa kuwaongezea wanafunzi alama. Tukishindwa kuwaandaa vijana wetu leo kwanini kesho tulalamike kuhusu huduma za afya, barabra, mahakama , waalimu wabovu?? Kama leo tunashindwa kuandaa wataalamu kwanini kesho tushangae ghorafa zikituangukia ?? Nape serikali yenu imeshindwa vibaya sana. Na ninaomba miradi yote ya viongozi walioshiriki kuuwa elimu ya nchi ife kwa ukosefu wa utaalamu labda mtajifunza. Nape leo mnafurahia kutibiwa nje na kuiuwa Muhimbili na hospitali zote za ndani, ila ukumbuke kesho mnastaafu uwezo wa kwenda nje kwa fedha za walipa kodi masikini mtakuwa hamna. Najua wote mnapigana vikumbo kutuibia ili kujaza mafedha ya kesho mkiwa nje ya siasa za kibazazi.
Ila Iko siku watanzania watadai fedha zao kwa nguvu.