Wako wapi waliodai Tume ya Katiba haina weledi na wala si huru!??

Hayo Nape anayaandika baada ya kuona mambo mengi yanmewaendea kombo CCM. Naamini asingekuja humu kama tume ingependelea upande wao. Tunakumbuka sana kuwa CCM walikuwa wanapinga sana wazo la katiba mpya, wala hatujasahau!
 
Mkuu Aweda. Hao ni lazima waondoke na hata wakibaki wasiwe wa kuteuliwa.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wamejificha porini kuficha nyuso zao kwa aibu kuu waliyopata single ya katiba imeisha jana hawana jipya tena.
 
nadhani unajua kazi kubwa ya upizani bwana nape usiwe wapenda kubwabwaja maneno uonekane tu unavitu vya kuongea tulia bro!
 
Nape Nnauye

Tatizo lako kwenye mada muhimu kama hizi zinazohitaji umahiri wa mtu huwa unazileta kwa mtindo wa mipasho, ungekuwa unatoa mada neutrally watu wangekuwa wanajadili vizuri, back to the topic.

Kwanza hakuna aliyesema tume haina weledi ila penye kitu kipya ni vizuri kuwa na tahadhali, kelele za wapinzani na akina Deus Kibamba wa Jukwaa la katiba zilikuwa ni katika kuhakikisha tunapata katiba nzuri lakini kwa wengine mliwaona kama wahuni.

Nikwambie @Nape, bila kelele hizo hata rasimu tunayoisifia leo ingekuwa tofauti na matarajio ya wengi, najua nyie wenzetu wa CCM kutaja kwa uchache hamkuwa kabisa wala wazo la sera ya katiba mpya, mlikuwa hamtaki serikali tatu, mlikuwa hamtaki mgombea binafsi, kwa hiyo kwa mawazo yangu sidhani kama rasimu hii mmeipokea kwa moyo mmoja mnachekelea usoni lakini moyoni mnajua itawaumiza.
 
jana nimemckia mmoja wa. waliokuwa wakipinga. tume hyo akipongeza rasimu hyo
sasa ina maana alikuwa anapinga kitu asichokijua
 

Acha upoyoyo GAMBA wewe!!! hivi ni kina nani walipendekeza nchi iwe na katiba mpya?!!! BASI NIKUULIZE NA WEWE ''' wako wapi waliosema hakuna umuhimu wa kuwa na katiba mpya?!!!''' Tafakari

 
....issue sasa si contents zilizo ndani ya rasimu ya katiba bali ni je nyie ccm mtakubaliana na implementation ya contents hizi????hili ndo jambo la msingi....

....Hata tume zilizopita za kina Jaji Kisanga et al...zilikua na mapendekezo mazuri sana ya marekebisho ya katiba.....lakini hayakua implemented yote....Issue hapa ni je nyie ccm mtayakubali mapendekezo haya ya tume ya Warioba???
 
Kamtuma yule wa buku7 aandike hivi, si yeye

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wamejificha porini kuficha nyuso zao kwa aibu kuu waliyopata single ya katiba imeisha jana hawana jipya tena.
Short minded wanadhani suala la katiba limeisha jana kwa watu weledi ndiyo kwanza limeanza.
 

Bwana Nape nina mashaka na uelewa wako! kilicholalamikiwa ni mabaraza ya katiba na tunasubiri tuone!
 

kaka watu hawajalalamikia tume wamelalamikia mfumo wa upatikanaji wa wawakilishi wa baraza la katiba ngazi za chini. We jamaa mtupu kabisa aisee.
 
Mark Francis kweli hata mimi sikutegemea mtu mwenye hadhi ya Katibu Mwenezi wa chama tawala aje na mipasho ya aina hii kwenye jambo la msingi kama hili.
 
kaka kuchambua rasimu ya katiba kunahitaji werevu, uwezo wa akili kutafakari; hapa hakuna mchambuzi bali kuna mshabiki wa siasa.
 
Tatizo ndugu yangu wewe unashindwa kutafsiri mambo kulingana na muktadha na unaweka mbele ushabiki.Haimaanishi kwamba mtu anapomkosoa mwenzake kwa jambo fulani; basi ndio ataendelea kumkosoa kila siku kwa udhaifu aliouonesha wakati fulani. Kimsingi mtu anapofanya kitu visivyo anakosolewa na anapofanya ndivyo anaungwa mkono. sasa sio kwa kuwa mtu kafanya zuri fulani hata akifanya makosa tumsifu tu na kwa kuwa kafanya kosa fulani hata akifanya zuri tumpinge tu! huo ni utabula rasa wa hali ya juu.Ndio maana unaona hata Deus Kibamba Jana kasifu vipengele vingi katika rasimu licha ya kuwa yeye alikuwa ni miongoni mwa watu wanaokosoa mwenendo mara kwa mara.
 
Reactions: Pai
Nape Nnauye

Professor Baregu amewavua nguo CHADEMA na katibu wako mkuu......


Professor Baregu once said

“If I told to choose between my country and my party (CHADEMA), I will choose my country,” akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha CHADEMA, angechagua nchi yake kwanza.
 
Vyema wananchi. Hii ni katiba tuachane na Nape tuijadili Katiba. Katiba haina chama, itaathiri na kufaidisha wote wanasiasa, wasio wanasiasa ila wananchi wote. Ukileta ushabiki wa rasimu hii utakuwa sawa na Nape asiyejua kwamba sio lazima awe CCM milele ila atakuwa Mtanzania/Mtanganyika milele.

katiba ndio uhai wa Taifa. Hii katiba imeacha mambo muhimu sana, inatupasa kuzingatia yale yote ambayo hayajawekwa kwenye rasimu.
 
Haya ni maoni ya chama chako au ndo mwisho wa upeo wako?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…