Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,762
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!
Kama si uimara wa tume na serikali iyopo madarakani basi matakwa ya wanakususasusa yangefuatwa. Tulishuhudia wakisusa bungeni, walipoona hawasikilizwi wakaamua kwenda Ikulu ambako nako mkuu wa kaya akawapa msimamo wake. Wasivyo watu wa kufikiria nini mbeleni wakatangaza kugomea mchakato wa katiba kwa sababu za kipuuzi huku wakimlazimisha professa wa watu ajitoe. Profesa kwa umakini wake akawaambia maslahi ya taifa ni zaidi kuliko maslahi ya chama. Sasa lrasimu imetoka na tumeona ilivyo na matarajio makubwa kwa wananchi tofauti na CDM walivyokuwa wakihubiri na kuwanywesha sumu wananchi. Ninawapongeza wazi wajumbe kwa kuliona kwa umakini suala la majimbo kuwa litaigawa taifa na litakuwa mwanzo wa ukabila, udini na nchi kuanza kumeguka. Kuna watu humu wanadai kuwa CCM imevamia mabaraza kwa ajili ya kuchakachua, kwa upande wangu naona ni wakosefu wa uelewa kwani kama ishu ingekuwa ni kuchakachua katiba wangeaza kabla rasimu haijatolewa ili wananchi wasijue nini kimepependekezwa na baraza. Leo hii wanaanza kuiona tume ipo makini wakati walikesha humu kwenye mitandao wakiichafua tume kuwa inatumika na hata viongozi wao wa chama kuichafua tume kupitia Bunge kuwa haina weledi. Leo hii huo weledi wanauona baada ya rasmi kuwasuta uongo wao. Hizi akili za kushikiwa sijui zitakwisha lini.