habari ya hapa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 12,791
- 8,749
Heshima kwenu mabibi na mabwana ni imani yangu kuwa hamjambo, poleni na heka heka za maisha
Km kichwa cha habari kinachojieleza hapo juu, nimeona leo nitoe dukuduku langu kuhusiana na hizi dini zilivyo tushika, na kweli tumeshikika na wametuweza na wamefanikiwa sana katika hili, na sisi pasi na kujiuliza tulikubali kuzipokea tukapumbazika, tukawaacha wakawekeza dini zao km vitega uchumi, haikutosha ili kutumaliza kabisa wakadai kuwa, dini zote za watu weusi, zikiwapo mila, desturi na tamaduni zao zote ni zamashetani.
Ndio maana adui wa maradhi, ujinga na umasikini ametuganda kwa sababu akili zetu zimedumaa, tunaendeshwa km gari bovu, hii ni kwasababu tumekubali kuwa vibaraka wa kupigania dini za watu, kupitia dini wametugawa vipande vipande, hawa watu waliotuletea dini wanadai kuwa wao ni mitume na manabii wa Mungu, shetani kwa mujibu wadini zao wanadai kuwa ana sura na maumbile mabaya eti ana mikia mingi mwenye rangi nyeusi km mwaafrika, huu ni upuuzi kabisa.
Tupo hivi tulivyo kwa sababu tuliacha mila, desturi na tamaduni zetu badala yake tukaamua kukumbatia mila na desturi za wengine. Kupitia tamaduni zao wanatudharau sasa kwa kusema kuwa mila, tamaduni na desturi zetu nitatokana na mashetani. Kwa mujibu wa dini hizi wanadai kuwa hapajawahi wala kupata kutokea kwa malaika mweusi tangu kuwapo kwa dunia,
Binafsi huwa nasema na nasema tena dini ni ujinga, tufundishwa ujinga na tumeamini ujinga na huenda waliamua kuletea dini kwa sababu kuna kifo na pengine kifo kisingekuwepo kusingekuwa na kitu dini, hebu tuache kudharauliana na kutengana sisi kwa sisi kwa sababu tu wewe wazijua mila za kiarabu na wewe wazijua mila za kizungu, turudi kwenye asili yetu, hizi dini za kiyahudi na kiarabu hazitatufikisha popote zaidi ya kuendelea kutufanya wajinga.