Kwanza mwaka 3020 A.D haujafika nadhani ulikuwa unamaanisha mwaka 320 au 302 labda...
ni kweli nilichapia ni mwaka 320 AD, kwanini hujibu swali
Sijui kama unaelewa kitu unaandika hapa,nani amekuambia Ukristo ni dini ya Wayahudi?
Ni kwa namna ipi Ukristo ni dini ya Wazungu? Kwanza Wazungu ni watu gani?
wewe wafikiri ukristo ni dini ya nani?
Ukristo ulikuwa biashara namna ipi?
Ukristo ulipoingia ulaya ulikuwa umekuwa itikadi, mfano dola ya kirumi na makanisa yanayofanna na hayo
angalia mfumo wa makanisa ya marekani, je mifumo hii inafanana?
Naona un aongeza maswali zaidi ya majibu na sijui kama utaweza kujibu haya maswali...
naweza
Hapa umenisikitisha sana na inaonekana umeanzisha thread ambayo huna kabisa elimu ya kutosha kuhusu ulichokianzishia thread...
Nikusaidie tu kwamba Ukristo ni ule ambao umeandikwa kwenye Biblia,hakuna mahali kuna haya madai yako hapa labda unioneshe sasa hivi hapa.Sijaona mahali kuna kitu hiki,nadhani unachanganya Ukristo na Wakristo maana hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa....
unapozungumzia ukristo unaizungumzia biblia, je bibilia hiyo iliandikwa na nani?
Mkristo akiamua kuwa jambazi hiyo haimaanishi kwamba Ukristo ndiyo unafundisha hivyo,jambo rahisi kama hili unashindwa kulielewa? Hayo madai yako ni ya hao weupe ambayo kimsingi hayana biblical back up bali ni namna yao tu ya kusambaza utamaduni wao kwa kutumia uongo.Kwenye Biblia kuna watu wengi tu wa nchi tofauti tofauti waliamua kuwa Wakristo na hatujaona hiki kitu,hakuna mahali kunamlazimisha mtu jambo unalosema...
ukristo au (dini) ni silaha iliyotumiwa na wakoloni km kinga yao ya kutawala na kuwanyonya waafrika kwa madai Mungu kasema, Mungu hahojiwi, kuhoji kitu cha kidini ni kosa la jinai, je umeshasoma church history
Nimekuambia kwamba kabla ya ukoloni Ukristo ulikuwa umeshaingia Afrika,ni kwa namna gani hatukusikia haya unayosema hadi walipokuja Wakoloni?
soma scared philosophy
Duh!! Wewe ni noma...
noma kwa lipi jamani wakati utumwa ulikuwapo?
Kwenye biblia agano jipya unapoona neno watumwa mara nyingi huwa linarejea wafanyakazi,neno wafanyakazi halina tofauti ya kimantiki na neno watumwa kwakuwa wote wanakuwa wanamtumikia mtu au kampuni fulani na ndio maana kuna ujira.Neno watumwa halimaanishi "slaves"mara nyingi lilipotumika kwenye agano jipya...
huo ni ujinga kwa kusema hivyo unapotosha ukweli, utumwa ni kazi unazozifanya bila hiari yako bila malipo, kazi si waomba wewe kwa hiari yako mwenyewe? hiari itakuwaje utumwa?
Pia,hata kama nikiamua kukubaliana na wewe kuwa lilimaanisha unachotaka kukisema hapa,nioneshe ni wapi kuna maelekezo ya kuwa na watumwa au kukamata watumwa...
nimekwambia maandiko ya Paulo anasema enyi watumwa watiini mabwana zenu, hili haliko kwa bibilia? mtu akikupiga shavu la kushoto mggeuzie na la pili huu si utumwa?
Una hokiandika hapa nakijua pengine kuliko hata wewe na ndiyo maana nasema kwamba hii thread huna uelewa nayo kwa namna ipaswavyo....
km wakijua kwanini wapindisha ukweli? au nawe ni mmoja wao wanaowadanganya watu?
Kuwa mmisionari siyo kuifuata biblia.Walikuja na biblia lakini waliyoyafanya na kusema yalikuwa kinyume na biblia hivyo usiseme waliyoyafanya na kuyatenda yalikuwa ni matokeo ya wao kuwa Wakristo maana na wao Ukristo walipelekewa tu kama wewe ulivyoletewa nguo za kimagharibi....
hao unaosema ukristo walipelekewa, walipelekewa na nani? ukristo sio Mungu, ungelisema kwamba waliyo yafanya yalikuwa kinyume cha Mungu, maana mengi waliyofanya ni itikadi ya ukristo, ulikuwa ni upanuzi wa himaya ya ukoloni kwa kisingizio cha Mungu, wakiita wakristo, wakibeba chapa ya ukristo, walikuwa hawaruhusu na hata sasa hawaruhusu kuhoji neno la dini kwa madai kwamba Mungu hahojiwi, je huyo Mungu walikutana nae wapi?
Mito hii imeandikwa hapo na hii inasababisha nisielewe mantiki ya swali lako,labda unataka kuniuliza hii mito ni ya eneo lipi,itakuwa vizuri kama ukiliweka swali lako vizuri....
nimekuuliza hivyo nikitaka kujua bustani ya edeni ilikuwa wapi au nchi gani? hebu nambie edeni ilikuwa wapi
Sijaona hoja ya maana kwenye maelezo yako ya kuuhusisha Ukristo na huu ujinga wa sisi Waafrika kuwa watumwa kifikra na kiutamaduni zaidi sana naona kama hujui jambo hili ipaswavyo maana unachanganya mambo na hii ni kutokana na kutokujua tu...
Mungu si dini na wala dini si Mungu, Mungu si ukristo wala ukristo si Mungu, Mungu hana mwanzo wala Mungu hana mwisho, mwanzo wa ukristo unajulikana, na hata mwanzo wa dini zote unajulikana, napenda watu wafahamu kwamba dini zote pamoja na ukristo hazitokani na Mungu, ni mawazo ya wanadamu juu ya Mungu, yapo mawazo mazuri ndani ukristo na dini, na yapo mawazo ndani ya dini na ndani ya ukristo yamepitwa na wakati, kwa hiyo uwe mwangalifu sana kwa mambo yaliyopitwa na wakati na kuyaweka pembeni
Rudi ukajifunze vizuri zaidi utaelewa....