Wakoloni walituletea dini kama kinga kwao ili watutawale

Hizi dini nimeachana nazo tangu 1999 baada ya kutumika kwa miaka mingi. We jiulize swali dogo tu, eti mtu akifariki wanamwita mzimu! Yaan leo baba yako akifariki ndio mwisho wa kumuita baba? Akili ni zako chagua mwenyewe ila najua mwisho wa siku wataumbuka baada ya waafrika kujitambua
 
Dini gani inasema mtu akifa anakuwa mzimu?
 
We labda huelewi leo ukimfanyia sherehe au tambiko marehemu unaambiwa unaabudu mizimu pia ukienda kutambika Makaburini unaambiwa unaomba mizimu
 
Hii ni dalili ya kuchoka na maisha. Watanzania tumeanza kufa pole pole na chanzo cha kifo hicho hamtakijua kamwe. Mleta mada inaonekana anafikiri sana lkn khali mbaya ya maisha imemfikisha hapo alipo.
huenda uko sahihi lkn weka akilini kwamba dini hazitokani na Mungu, wala Mungu hatokani na dini, dini ni mawazo ya wanadamu juu ya Mungu, Mungu sio dini wala dini sio Mungu, wakoloni walitumia dini kuwa kinga ya kupanua himaya ya tawala zao, wakoloni hawa bila soni, walianza kupora mali za wa afrika wakatuachaa waafrika tukiwa hoi huku wakijigamba kuwa wao ni watumishi wa Mungu kumbe ni wachumia tumbo tu, hawakuishia hapo walienda mbali hata kuchoma moto nyaraka za historia ya waafrika kwa madai kuwa zilikuwa nyaraka za mashetani,
 
mkuu Eiyer kabla ya afrika kuvamiwa na wakoloni afrika chini ya uongozi wa Mafarao, lilikuwa bara linoongoza kwa tekenolojia na maendeleo duniani, miili ya mafarao waliokufa miaka 3,000 iliyopita ilipakwa dawa ikazikwa haijaoza mpaka leo, maarifa haya leo hayakupo duniani na afrika wakati huo ilikuwa ikiongoza kwa sayansi na utawala bora ikiwa na taasisi nyingi za utafiti wa kisayansi ambazo dini za kigeni mujibu wa dini za kigeni wanaziita Mungu, afrika imewahi kutawala dunia kwa miaka isiyopungua 18,000 au zaidi, tangu hapo afrika lilikuwa bara tulivu kutokana na asili ya watu wake kuwa waungwana na watulivu, (watu weusi)Tawala za afrika zilikuwa tawala za kidemokrasia waatu wake walikuwa na uhuru wa kutoa mawazo yao mradi havunji sheria za nchi, waaafrika wana asili ya utu wema, upole, ni waungwana, wakarimu, hawana asili ya ubaguzi, kama wangelikuwa ni watu wabaguzi, Yusufu wasingempa kazi ya uwaziri mkuu wa nchi yao.

Mambo yalianza kubadilika baada ya Warumi kuchukua dola kutoka mikononi mwa wagiriki waarumi walianzisha utawala wa sheria, mfumo uliowafanya wawe maarufu na kupendwa sana duniani, kwawa bahati mbaya,watawala hawa walijisahau, wakajiingiza katika starehe naufisadi hapo ndipo sayansi, utawala bora na democrasia vikatoweka, badala yake starehe na ufisadi ikawa ndio dira ya watawala, watanashati, wakaasisi siku kuu nyingi za mapumziko kitaifa, siku kuu hizo zilisherehekewa kwa ngono na ufisadi, Moja wapo ya siku kuu za aina hiyo ilikuwa siku ya tarehe 25 Desemba, siku kuu hizo, nyingine zilipigwa marufuku nyingine kubadilishwa kama ile ya Tarehe 25 December ambayo ilibadilishwa ikawa siku kuu ya Chrismas siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu,

kupitia dini walitukandamiza wa afrika wakapanua dola yao kwa kisingizio kuwa wametumwa na Mungu, wazungu walikuwa watu wa kwanza kufika afrika kuleta dini, walitumia ulaghai mwingi kulaghai watu kuzisadikisha dini zao, waarabu nao walipoleta dini, walitumia ulaghai ule ule uliotumiwa na wazungu kusadikisha dini zao, pamoja na kutumia ulaghai mwingi, pia waarabu walitumia mabavu kusadikisha dini yao, yaani jihad, walifanya mauaji ya kikatili ya hali ya juu, mfano mzuri ni pale walipovamia afrika kaskazini, walichinja watu kama watu wanavyochinja kuku, waliwaona watu weusi kuwa nimashetani makafri hawatokani na Mungu, wakidai kuwa wao wametumwa na Mungu kuleta dini, huu ni ushenzi wa hali ya juu waliotufanyia hawa watu na dini zao,
 
Mtoa mada as if u are reading my mind ,,binafsi nakiri umekomboleka na pia endelea kukomboa ,hoja yako nzito sana kwa jinsi ambavyo waafrika dini zilivowaingia inahiyaji nguvu ya ziada ,,umetema ukweli ""kwa wakristo wenzangu unabiwa FUNGU LA KUMI " hapo watu bora alale njaaa ili atoe fungu la kumi waliwaweza kwangu dini hainiendeshi
 
ni zaidi ya hatari mkuu dini zimejaa vitisho kuwatisha watu tu eti usipotoa zaka na sadaka wewe ni mwizi unamwibia Mungu na utakwenda motoni, huu ujinga ulianza katika karne ya 17, wakati wakoloni walipotaka kuigawana Afrika, waliwaagiza wa missionary kuwafundisha waafrika kuwa eti Mungu anakaa juu mbinguni, baraka zote wanazotaka zinapatikana mbinguni na si duniani, wakiisha omba wakae watulie wamsubiri Mungu kuwaletea kile walichoomba, wawatoze kodi bila yakuwapa stakabadhi yaani zaka, wawatoze michango washirika wao kila wanapohudumu ndo hiyo sadaka, wawasadikishe kuwa zaka na sadaka ni mali ya Mungu, kutomtolea Mungu zaka na sadaka huko ni kumwibia.
 
We labda huelewi leo ukimfanyia sherehe au tambiko marehemu unaambiwa unaabudu mizimu pia ukienda kutambika Makaburini unaambiwa unaomba mizimu
Wewe ulisema kwamba dini zinasema kwamba marehemu ni mizimu,maandiko yako haya hayaelezi ni kwa vipi dini zinasema marehemu ni mizimu kwakuwa kwanza hayo ni maneno ya wanadini siyo dini zenyewe kwa maana ya vitabu....

Sijui hata kama unajua tofauti hii.....
 
mkuu Eiyer kabla ya afrika kuvamiwa na wakoloni afrika chini ya uongozi wa Mafarao, lilikuwa bara linoongoza kwa tekenolojia na maendeleo duniani, miili ya mafarao waliokufa miaka 3,000 iliyopita ilipakwa dawa ikazikwa haijaoza mpaka leo, maarifa haya leo hayakupo duniani na afrika wakati huo ilikuwa ikiongoza kwa sayansi na utawala bora ikiwa na taasisi nyingi za utafiti wa kisayansi ambazo dini za kigeni mujibu wa dini za kigeni wanaziita Mungu, afrika imewahi kutawala dunia kwa miaka isiyopungua 18,000 au zaidi, tangu hapo afrika lilikuwa bara tulivu kutokana na asili ya watu wake kuwa waungwana na watulivu, (watu weusi)Tawala za afrika zilikuwa tawala za kidemokrasia waatu wake walikuwa na uhuru wa kutoa mawazo yao mradi havunji sheria za nchi, waaafrika wana asili ya utu wema, upole, ni waungwana, wakarimu, hawana asili ya ubaguzi, kama wangelikuwa ni watu wabaguzi, Yusufu wasingempa kazi ya uwaziri mkuu wa nchi yao.

Mambo yalianza kubadilika baada ya Warumi kuchukua dola kutoka mikononi mwa wagiriki waarumi walianzisha utawala wa sheria, mfumo uliowafanya wawe maarufu na kupendwa sana duniani, kwawa bahati mbaya,watawala hawa walijisahau, wakajiingiza katika starehe naufisadi hapo ndipo sayansi, utawala bora na democrasia vikatoweka, badala yake starehe na ufisadi ikawa ndio dira ya watawala, watanashati, wakaasisi siku kuu nyingi za mapumziko kitaifa, siku kuu hizo zilisherehekewa kwa ngono na ufisadi, Moja wapo ya siku kuu za aina hiyo ilikuwa siku ya tarehe 25 Desemba, siku kuu hizo, nyingine zilipigwa marufuku nyingine kubadilishwa kama ile ya Tarehe 25 December ambayo ilibadilishwa ikawa siku kuu ya Chrismas siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu,

kupitia dini walitukandamiza wa afrika wakapanua dola yao kwa kisingizio kuwa wametumwa na Mungu, wazungu walikuwa watu wa kwanza kufika afrika kuleta dini, walitumia ulaghai mwingi kulaghai watu kuzisadikisha dini zao, waarabu nao walipoleta dini, walitumia ulaghai ule ule uliotumiwa na wazungu kusadikisha dini zao, pamoja na kutumia ulaghai mwingi, pia waarabu walitumia mabavu kusadikisha dini yao, yaani jihad, walifanya mauaji ya kikatili ya hali ya juu, mfano mzuri ni pale walipovamia afrika kaskazini, walichinja watu kama watu wanavyochinja kuku, waliwaona watu weusi kuwa nimashetani makafri hawatokani na Mungu, wakidai kuwa wao wametumwa na Mungu kuleta dini, huu ni ushenzi wa hali ya juu waliotufanyia hawa watu na dini zao,
Umeandika maelezo mengi lakini sijaona umuhimu wa maelezo yako haya kutokana na nilichokisema hapo mwanzo.....

Kwanza nilikuambia kuwa Ukristo siyo dini ya wazungu..

Pia,Nilikuambia kwamba,hao wazungu wakati wanakuja huku Afrika hiyo karne ya 17 tayari huku Ukristo ulikuwepo,labda uniambie tu kwamba walipeleka Ukristo baadhi ya maeneo na siyo kwamba walileta Ukristo hapa Afrika....

Lakini zaidi nilikuambia kuwa Ukristo hajawahi kumfanya mtu akaacha mila zake,kama wazungu walikuja na ulaghai hilo ni suala lingine...

Hebu niambie dini hii inakandamizaje watu na kuwafanya waache mila zao na desturi zao na hatimaye kuwa watumwa wa desturi zingine?

Kwanini hatukusikia habari ya utumwa wakati akila Luka wanakwenda Libya?
Kwanini hatukusikia habari ya watumwa wakati akina Barnaba wanakwenda Ethiopia huko?

Unachokiongelea wewe hapa hakikusababishwa na Ukristo hivyo weka hoja yako kwa namna nyingine ili upate michango sahihi.Tatizo la Waafrika halijasababishwa na Ukristo bali mambo mengine tu....
 
Hebu tuanze na kueleza hapa kwetu Tanzania,hebu tufafanulieni ni vp kwamba tupo hivi tulivyo kwa sababu ya ukristo na uislamu. Hebu tupeni uchambuzi wa umasikini wa Tz ni vp dini hizi mbili zimehusika.
 
[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeforLema[/HASHTAG]
 
Bnafsi dini imenisaidia sana malezi yao walivyonielekeza na kunielea kiutu na kimaadili ni mtu muhimu sana ktk position yangu kama mtumishi wa umma na mwanadamu kweli ninayejiheshimu n kuwaheshimu wenzangu
Ni sawa lkn utamaduni wenu unakuongoza kufanya ma
 
Umeandika maelezo mengi lakini sijaona umuhimu wa maelezo yako haya kutokana na nilichokisema hapo mwanzo.....

Kwanza nilikuambia kuwa Ukristo siyo dini ya wazungu..

Pia,Nilikuambia kwamba,hao wazungu wakati wanakuja huku Afrika hiyo karne ya 17 tayari huku Ukristo ulikuwepo,labda uniambie tu kwamba walipeleka Ukristo baadhi ya maeneo na siyo kwamba walileta Ukristo hapa Afrika....

Lakini zaidi nilikuambia kuwa Ukristo hajawahi kumfanya mtu akaacha mila zake,kama wazungu walikuja na ulaghai hilo ni suala lingine...

Hebu niambie dini hii inakandamizaje watu na kuwafanya waache mila zao na desturi zao na hatimaye kuwa watumwa wa desturi zingine?

Kwanini hatukusikia habari ya utumwa wakati akila Luka wanakwenda Libya?
Kwanini hatukusikia habari ya watumwa wakati akina Barnaba wanakwenda Ethiopia huko?

Unachokiongelea wewe hapa hakikusababishwa na Ukristo hivyo weka hoja yako kwa namna nyingine ili upate michango sahihi.Tatizo la Waafrika halijasababishwa na Ukristo bali mambo mengine tu....

1. Ukristo sio dini ya wayahudi, ni dini ya wazungu, wkati warumi walipoutaifisha ukristo mwaka 3020 AD, wakaufanya ukristo kuwa itikadi ya Ulaya, Ukristo huo huo ulipoingia marekani ukawa biarasha.

2. Unapotaka kuwa Mkristo, ukristo unakulazimisha kuacha jina lako la asili na kuchukua jina la kizungu au kiyahudi

3. Utumwa ulikuwapo ndio maana Paulo ana sema hivi enyi watumwa watiini mabwana zenu,

halafu unaposema matatizo ya waafrika hayakusababishwa na dini unajua historia vizuri? km unajua historia, katika karne ya 17 wa misionary waliagizwa wawafundisheje waafrika?

MWANZO sura 2. mstari wa 10, unasema hivi ukatoka mto mmoja ukamwagilia bustani ya edeni, kutoka hapo ukagawanyika katika viunga vinne, ambavyo ni Gishoni na Pishoni, Euphrates na Tigris hivi wajua mto huu ni mto gani?,
 
Hebu tuanze na kueleza hapa kwetu Tanzania,hebu tufafanulieni ni vp kwamba tupo hivi tulivyo kwa sababu ya ukristo na uislamu. Hebu tupeni uchambuzi wa umasikini wa Tz ni vp dini hizi mbili zimehusika
 
Hebu tuanze na kueleza hapa kwetu Tanzania,hebu tufafanulieni ni vp kwamba tupo hivi tulivyo kwa sababu ya ukristo na uislamu. Hebu tupeni uchambuzi wa umasikini wa Tz ni vp dini hizi mbili zimehusika.

Dini zina husika sana kwa umasikini afrika na Tz, zinafundisha vitu vingi ambayo vinamfanya mtu akili yake idumae, huwa nasema dini na wapiga ramsli ni kitu kimoja, wote hawa wanafanya biashara za kuuza pepo, wote hawa wanapandisha pepo, pepo linapowapagaa wana dini, dini hudai ni roho mtakatifu wa Mungu, ni pepo wazuri, lkn pepo wanaopandishwa nje ya dini za kigeni yaani wapiga ramli dini zinadau kuwa pepo hao hutokana na mashetani, hao wote wanadini na wapiga ramli asili yao ni ujinga kwa sababu wanaimarisha ujinga miongoni mwa binadamu, si wanadini wala wapiga ramli wanaruhusu binadamu kuhoji mambo yao, wanadai mambo yao wanoyafanya hayahojiwi, ukihoji wanadai unampinga Mungu na kujitafutia laana kwa kuhoji unamkufuru Mungu.

dini inawambia watu watamani vitu kutoka juu mbinguni wasitamani mali za dunia, hawa wana dini hawa kuishia hapo walihakikisha kuwa waafrika wanauona na kuuhesabu utajiri sawa na mavi, ukiacha hayo wanatufundisha kuwa watakatifu wote wataishi mbinguni kwa maisha ya umilele, umilele wa maisha haya hutofautiana kati ya dini na dini, mfano dhana wakikristo wasema, mbinguni hakuna kufa, hakuna kula wala kunywa ni kuabuda na kusifu tu, kwa waislamu wao wanadai kuwa maisha ya umilele mtu atapata thawabu ya kukaa katika bustani iliyo na majani mabichi yenye mito inotiririsha maji mengi, watahudumiwa kwa vinywaji vitamu, huduma itakayokuwa ikitolewa na wanawake warembowenye macho makubwa km vikombe, kwa ufupi dini na wapiga ramli wote ni kitu kimoja yaani dini ramsli, ramli ni dini
 
Mkuu mbona unaponda dini badala ya kueleza hatua kwa hatua jinsi dini zilivyofanya Tz ikawa masikini?

Mimi nimetaka kufahamishwa jinsi dini zilivyohusika na umasikini wa Tz.
 
1. Ukristo sio dini ya wayahudi, ni dini ya wazungu, wkati warumi walipoutaifisha ukristo mwaka 3020 AD, wakaufanya ukristo kuwa itikadi ya Ulaya, Ukristo huo huo ulipoingia marekani ukawa biarasha.
Kwanza mwaka 3020 A.D haujafika nadhani ulikuwa unamaanisha mwaka 320 au 302 labda...

Sijui kama unaelewa kitu unaandika hapa,nani amekuambia Ukristo ni dini ya Wayahudi? Ni kwa namna ipi Ukristo ni dini ya Wazungu? Kwanza Wazungu ni watu gani?

Ukristo ulikuwa biashara namna ipi?

Naona un aongeza maswali zaidi ya majibu na sijui kama utaweza kujibu haya maswali...
2. Unapotaka kuwa Mkristo, ukristo unakulazimisha kuacha jina lako la asili na kuchukua jina la kizungu au kiyahudi
Hapa umenisikitisha sana na inaonekana umeanzisha thread ambayo huna kabisa elimu ya kutosha kuhusu ulichokianzishia thread...

Nikusaidie tu kwamba Ukristo ni ule ambao umeandikwa kwenye Biblia,hakuna mahali kuna haya madai yako hapa labda unioneshe sasa hivi hapa.Sijaona mahali kuna kitu hiki,nadhani unachanganya Ukristo na Wakristo maana hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa....

Mkristo akiamua kuwa jambazi hiyo haimaanishi kwamba Ukristo ndiyo unafundisha hivyo,jambo rahisi kama hili unashindwa kulielewa? Hayo madai yako ni ya hao weupe ambayo kimsingi hayana biblical back up bali ni namna yao tu ya kusambaza utamaduni wao kwa kutumia uongo.Kwenye Biblia kuna watu wengi tu wa nchi tofauti tofauti waliamua kuwa Wakristo na hatujaona hiki kitu,hakuna mahali kunamlazimisha mtu jambo unalosema...

Nimekuambia kwamba kabla ya ukoloni Ukristo ulikuwa umeshaingia Afrika,ni kwa namna gani hatukusikia haya unayosema hadi walipokuja Wakoloni?
3. Utumwa ulikuwapo ndio maana Paulo ana sema hivi enyi watumwa watiini mabwana zenu,
Duh!! Wewe ni noma...

Kwenye biblia agano jipya unapoona neno watumwa mara nyingi huwa linarejea wafanyakazi,neno wafanyakazi halina tofauti ya kimantiki na neno watumwa kwakuwa wote wanakuwa wanamtumikia mtu au kampuni fulani na ndio maana kuna ujira.Neno watumwa halimaanishi "slaves"mara nyingi lilipotumika kwenye agano jipya...

Pia,hata kama nikiamua kukubaliana na wewe kuwa lilimaanisha unachotaka kukisema hapa,nioneshe ni wapi kuna maelekezo ya kuwa na watumwa au kukamata watumwa...
halafu unaposema matatizo ya waafrika hayakusababishwa na dini unajua historia vizuri? km unajua historia, katika karne ya 17 wa misionary waliagizwa wawafundisheje waafrika?
Una hokiandika hapa nakijua pengine kuliko hata wewe na ndiyo maana nasema kwamba hii thread huna uelewa nayo kwa namna ipaswavyo....

Kuwa mmisionari siyo kuifuata biblia.Walikuja na biblia lakini waliyoyafanya na kusema yalikuwa kinyume na biblia hivyo usiseme waliyoyafanya na kuyatenda yalikuwa ni matokeo ya wao kuwa Wakristo maana na wao Ukristo walipelekewa tu kama wewe ulivyoletewa nguo za kimagharibi....
MWANZO sura 2. mstari wa 10, unasema hivi ukatoka mto mmoja ukamwagilia bustani ya edeni, kutoka hapo ukagawanyika katika viunga vinne, ambavyo ni Gishoni na Pishoni, Euphrates na Tigris hivi wajua mto huu ni mto gani?,
Mito hii imeandikwa hapo na hii inasababisha nisielewe mantiki ya swali lako,labda unataka kuniuliza hii mito ni ya eneo lipi,itakuwa vizuri kama ukiliweka swali lako vizuri....

Sijaona hoja ya maana kwenye maelezo yako ya kuuhusisha Ukristo na huu ujinga wa sisi Waafrika kuwa watumwa kifikra na kiutamaduni zaidi sana naona kama hujui jambo hili ipaswavyo maana unachanganya mambo na hii ni kutokana na kutokujua tu...

Rudi ukajifunze vizuri zaidi utaelewa....
 
wakati umefika waa afrika tuachanane na mambo ya dini kwani hayana tija, kila mtu atumie akili yake kuchambua maandiko yote ya misaafu ya kidini na kwenda na muda, muda umefika wa kuacha kwenda kumpiga shetani mawe, ili hali mkujua kuwa kwa mujibu wa dini wanasema kuwa shetani ni roho, sasa km shetani ni roho inawezekana vipi kuwahasisha watu wakashindane kupiga hewa? katika kushindana huko kuipiga hiyo hewa watu huwa wanakufa kwa kukanyagana, km shetani ni roho nani aliyewahi kumwona?. jamani kumponda mawe shetani ni kuchukia na kuachana na uovu wote, tenda haki, simamia haki na tetea haki maishani wako, huko ndiko kufunga na si vinginevyo, zaidi sana wapende binadamu wote bila kuwabagua na uwe tayari kuwasaidia katika matatizo yao mahali unapojiweza, usisahau kwamba kkila siku na kila mwezi na kila mwama Mungu ni Mtukufu, siku zote unapaswa kuachana na maovu, kwa kufanya hivyo dini yako haikusaidii wala Mungu hatakuwa na radhi nawe maana siku na miezi yote ni ya Mungu,
 
Nakuunga mkono kwa asilimia zote.

Dini ni moja ya alama ya utamaduni[Cultural element]
Ni kama ilivyo lugha, mtindo wa mavazi, mila na desturi n.k.

Sasa walipokuja wazungu, wakaanza ku-undervalue kila kilichokuwa cha mwaafrika,
Waka waambia waafrika lugha zao ndo bora zaidi, dini zao ndo bora zaidi maana zinatoka kwa Mungu tofauti na za waafrika zinazotoka kwa Shetani.
Hata majina ya waafrika yalidharaulika na kupewa yale ya waleta dini.

Dini hazikuwa na lengo la kufanya penetration ya ukoloni pekee bali kumtawala mwaafrika milele.
Dini ni aina ya utawala kama zililvyo tawala zingine.

Ngoja wale walokole wakuskie waje
 
Back
Top Bottom