Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Katika historia ya dunia na uchipukaji wa dini duniani unaonesha kwamba mara nyingi dini huenda sambamba pamoja na siasa na tawala za nchi.
Hali hii ilikuwa na nguvu katika ujenzi wa mwanzo wa mataifa ya Ulaya na makoloni yake sehemu mbalimbali za duniani hata mataifa ya mashariki ya kati nayo yalitumia na yana tumia mtindo huu pia hata kwa Afrika Misri ya kale ilifanya hivi hata Ethiopia katika historia yake inafanya hivi.
Urusi( Usovieti ) katika hatua za mwanzo walijaribu kuunda taifa ambalo dini na siasa zipo mbali lakini baada ya kuanguka Usovieti miaka ya 90 Kanisa la orthodox lina ushawishi mkubwa katika maamuzi na siasa za Urusi na majirani zake mfano Ukraine.
Tuje kwenye lengo la uzi kama kichwa cha uzi kinavyosema" WAKOMUNISTI pekee ndio wamefaulu kuweka mbali dini na siasa za nchi".
Ndio, hapa nitatumia mfano wa wakomunisti waliobaki nao ni China, North Korea, Vietnam kwa mfano rahisi utakao eleweka na wote ni China kutokana na ukubwa wake na mambo yake mengi kuwa wazi kufahamika kwa yoyote atakaye hitaji kuyafahamu tofauti na North Korea kidogo.
Kwanza kabisa sheria na katiba ya chama cha wakomunisti wa huko uchina hakitoi Uhuru wa mwanachama kuwa muumini wa dini yoyote hiki ndicho chama cha "atheist" wengi duniani ( wakana Mungu,dini ) hivyo kinanyima na kuondoa nafasi ya dini kuwa na influence ndani ya chama tawala cha China.
Kama tunavyo fahamu chama cha kikomunisti cha China ndicho chama tawala cha China toka uhuru wao mpaka sasa hivyo dini kukosa nafasi ndani ya chama moja kwa moja dini inakosa nguvu ya kiushawishi ndani ya serikali na nchi kwa ujumla.
Hiki chama kinauwezo wa kufanya au kuchukua maamuzi yoyote yale kwa maslahi mapana ya nchi pasipo kujali dini ya mtu mfano hiki chama kimewahi kutatua migogoro yake maeneo mbalimbali ya uchina ambapo dini ilikuwa na influence kubwa sana na tishio kwa serikali na utawala.
Kwa hapa kwetu nchini ni ngumu sana kuzitenganisha dini na siasa itahitajika nguvu kubwa itakayoleta maafa kwasababu:-
i, Nchi yetu haina muundo wa nchi za kikomunisti
ii, Harakati zetu za uhuru kwa kiasi kikubwa ziliratibiwa na dini( Waislamu na makanisa)
iii, Dini imechukua nafasi kubwa ndani ya watu na kutawala hisia zao kwa kiasi kikubwa
iv, Vyama vya siasa kutumia viongozi wa dini na taasisi za kidini kupata ushawishi na umaarufu wa kisiasa ( hapa mifano mingi ipo wazi )
V, Shughuli za kiserikali kuongozwa na watu wa dini( masheikh na wachungaji huu umekwisha onekana kama utaratibu wa kawaida )
Vi, Dini kutawala mambo ya nchi, serikali mfano bungeni, wimbo wa taifa( kinyume na katiba ya nchi )
Mwisho taifa letu sio la kiatheist kama ilivyo China na North Korea, we are not communists hivyo dini kuwa mbali na siasa zetu za hapa nchini moja kwa moja bila kupindisha mpaka sasa haiwezekani kamwe labda tuunde taifa upya kwa gharama kubwa ya maisha ya watu ndio hilo liwezekane.
Ni hayo machache