WAKOMUNISTI pekee ndio wamefaulu kuweka mbali dini na siasa za nchi

WAKOMUNISTI pekee ndio wamefaulu kuweka mbali dini na siasa za nchi

Huwezi tenganisha dini na siasa maana vyote uhudumia watu.
Dini uhudumia roho siasa uhudumia mwili.
Dini inaathiri siasa na siasa inaathiri dini
 
Ni Kweli, dini na siasa visichanganywe.

Lakini ni hatari KUONGOZWA na watu wasio na IMANI na HOFU ya Mungu, tukiendelea kuruhusu wezi na wazinzi nk nk kutuongoza, IPO siku Mapepo nusu mtu nusu binafamu yatatawala Wana wa Mungu.
Kuongozwa na mtu aliye na asie na hofu ya Mungu wala asiye mjua Mungu sio tatizo wala haina maana kwa sababu hayo ni masuala yake binafsi jambo la msingi ni aheshimu katiba ya nchi basi
 
Dini inaleta upendo,utu, heshima na maadili ya mtu.
Dini inapinga mtu asiwe mwizi, fisadi,rushwa,mtu asiye na dini ni rahisi kuwa na hivyo.
Hapana mtu yoyote mwenye ufahamu anafahamu kuwa hiki kibaya na hiki kizuri bila kujali ana dini au laaah!
 
Ukomunist nchi ni mali ya wahuni wachache, mtawaliwa yeyeto hana haki juu ya maamuzi yeyeto kuhusu nchi yake.
Mtawaliwa ni mali ya mtawala ndo maana ya kurithithana ufalme.
 
Huwezi tenganisha dini na siasa maana vyote uhudumia watu.
Dini uhudumia roho siasa uhudumia mwili.
Dini inaathiri siasa na siasa inaathiri dini
Unaweza kuweka dini mbali na siasa za nchi sijui uelewa wako wa mambo upoje
 
Ukomunist nchi ni mali ya wahuni wachache, mtawaliwa yeyeto hana haki juu ya maamuzi yeyeto kuhusu nchi yake.
Mtawaliwa ni mali ya mtawala ndo maana ya kurithithana ufalme.
Hatupo hapa kuelezeana namna ukomunisti unavyo chukuliwa na watu bali namna ukomunisti umefaulu kuweka mbali dini na siasa za nchi tujikite hapo
 
China zipo mbili ya Sasa na ya zamani.
Ya Sasa iliutupa shimoni ukomunist ndo maana Ina maendeleo.
Ukomunist umebakia kwenye chama tu na Sio kwenye maisha ya watu
Umevuta bangi ? Unasema China imeachana na Ukomunisti hapo hapo unasema ukomunisti upo kwenye chama tu.
kwani hicho chama kinaongoza buguruni ?!
 
Sio propaganda katika hili la dini wamefaulu kuweka mbali na siasa za nchi wala hakuna propaganda kila mwenye macho anaona tofauti na hapa kwetu na mataifa mbalimbali
Halafu woote tumuabudu Chairman MAO

Hakuna mfumo mzuri kwa Taifa kama Liberal Democracy kila taasisi inatoa maoni yake na kushauri

Kuhusisha Viongozi wa Dini na makundi mengine ya Jamii kuishauri Serikali yao

Kumbuka Mwanasiasa anaweza kukuuza Utumwani ukizubaa
 
Sasa chak
Umevuta bangi ? Unasema China imeachana na Ukomunisti hapo hapo unasema ukomunisti upo kwenye chama tu.
kwani hicho chama kinaongoza buguruni ?!
Sasa chama ndio maisha ya Wachina,wachina wa Sasa Sio wale wa miaka ile
 
Halafu woote tumuabudu Chairman MAO

Hakuna mfumo mzuri kwa Taifa kama Liberal Democracy kila taasisi inatoa maoni yake na kushauri

Kuhusisha Viongozi wa Dini na makundi mengine ya Jamii kuishauri Serikali yao

Kumbuka Mwanasiasa anaweza kukuuza Utumwani ukizubaa
Hakuna anaye abudia ndani ya mfumo wa ukomunisti hicho ni kinyume na ukomunisti wenyewe ila kuna heshima ya kipuuzi iliyo pitiliza kwa wakomunisti kwa mwenyekiti wao by the way huo upuuzi wa Mao alikufa nao mwenyewe na genge lake mwenyewe. Ukomunisti uo against masuala ya kuabudu chochote kile
 
Sasa chak

Sasa chama ndio maisha ya Wachina,wachina wa Sasa Sio wale wa miaka ile
Dogo ukomunisti ni mfumo wa siasa na uchumi usifikiri ukomunisti ni uchumi tu siasa haihusiki
 
Hakuna anaye abudia ndani ya mfumo wa ukomunisti hicho ni kinyume na ukomunisti wenyewe ila kuna heshima ya kipuuzi iliyo pitiliza kwa wakomunisti kwa mwenyekiti wao by the way huo upuuzi wa Mao alikufa nao mwenyewe na genge lake mwenyewe. Ukomunisti uo against masuala ya kuabudu chochote kile
North Korea nilienda miaka fulani inabidi usujudie hata picha ya Dear Leader.
 
Katika historia ya dunia na uchipukaji wa dini duniani unaonesha kwamba mara nyingi dini huenda sambamba pamoja na siasa na tawala za nchi.

Hali hii ilikuwa na nguvu katika ujenzi wa mwanzo wa mataifa ya Ulaya na makoloni yake sehemu mbalimbali za duniani hata mataifa ya mashariki ya kati nayo yalitumia na yana tumia mtindo huu pia hata kwa Afrika Misri ya kale ilifanya hivi hata Ethiopia katika historia yake inafanya hivi.

Urusi( Usovieti ) katika hatua za mwanzo walijaribu kuunda taifa ambalo dini na siasa zipo mbali lakini baada ya kuanguka Usovieti miaka ya 90 Kanisa la orthodox lina ushawishi mkubwa katika maamuzi na siasa za Urusi na majirani zake mfano Ukraine.

Tuje kwenye lengo la uzi kama kichwa cha uzi kinavyosema" WAKOMUNISTI pekee ndio wamefaulu kuweka mbali dini na siasa za nchi".

Ndio, hapa nitatumia mfano wa wakomunisti waliobaki nao ni China, North Korea, Vietnam kwa mfano rahisi utakao eleweka na wote ni China kutokana na ukubwa wake na mambo yake mengi kuwa wazi kufahamika kwa yoyote atakaye hitaji kuyafahamu tofauti na North Korea kidogo.

Kwanza kabisa sheria na katiba ya chama cha wakomunisti wa huko uchina hakitoi Uhuru wa mwanachama kuwa muumini wa dini yoyote hiki ndicho chama cha "atheist" wengi duniani ( wakana Mungu,dini ) hivyo kinanyima na kuondoa nafasi ya dini kuwa na influence ndani ya chama tawala cha China.

Kama tunavyo fahamu chama cha kikomunisti cha China ndicho chama tawala cha China toka uhuru wao mpaka sasa hivyo dini kukosa nafasi ndani ya chama moja kwa moja dini inakosa nguvu ya kiushawishi ndani ya serikali na nchi kwa ujumla.

Hiki chama kinauwezo wa kufanya au kuchukua maamuzi yoyote yale kwa maslahi mapana ya nchi pasipo kujali dini ya mtu mfano hiki chama kimewahi kutatua migogoro yake maeneo mbalimbali ya uchina ambapo dini ilikuwa na influence kubwa sana na tishio kwa serikali na utawala.

Kwa hapa kwetu nchini ni ngumu sana kuzitenganisha dini na siasa itahitajika nguvu kubwa itakayoleta maafa kwasababu:-
i, Nchi yetu haina muundo wa nchi za kikomunisti
ii, Harakati zetu za uhuru kwa kiasi kikubwa ziliratibiwa na dini( Waislamu na makanisa)
iii, Dini imechukua nafasi kubwa ndani ya watu na kutawala hisia zao kwa kiasi kikubwa
iv, Vyama vya siasa kutumia viongozi wa dini na taasisi za kidini kupata ushawishi na umaarufu wa kisiasa ( hapa mifano mingi ipo wazi )
V, Shughuli za kiserikali kuongozwa na watu wa dini( masheikh na wachungaji huu umekwisha onekana kama utaratibu wa kawaida )
Vi, Dini kutawala mambo ya nchi, serikali mfano bungeni, wimbo wa taifa( kinyume na katiba ya nchi )

Mwisho taifa letu sio la kiatheist kama ilivyo China na North Korea, we are not communists hivyo dini kuwa mbali na siasa zetu za hapa nchini moja kwa moja bila kupindisha mpaka sasa haiwezekani kamwe labda tuunde taifa upya kwa gharama kubwa ya maisha ya watu ndio hilo liwezekane.

Ni hayo machache
communism inaamini dini ni kama madawa ya kulevya inaua jamii ya watu walio wamoja

mfano waafrica leo wanaonana maadui kisa dini isingekua dini wangekua kitu kimoja
 
Back
Top Bottom