Wakongo (Congo DR) wametudharau sana Wabongo (Tanzania) Jana haki ya nani

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kocha wa Taifa Stars Kim Paulsen amekisuka Kikosi chake kwa Siku 8 mfululizo, huku Kocha Hector Couper ameungana na Wachezaji wake Juzi Usiku tu na Jana wametufunga Kishalubela (Kikatili) Magoli 3 kwa 0 kwa Mkapa tena mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waandamizi wengine wa Serikali.

Asante Wakongo wa Kutudharau Jana.
 
Tanzania kwa siku hizi hatuna kabisa wachezaji wenye vipaji vya asili vya kusakata kabumbu tumebaki na watu wa kufanya "Show" kwenye vyombo vya habari na kupiga pesa. That's all.

Hatuna wachezaji kama akina Abdallah Kibaden, Sunday Manara, Saad Ally, Gibson Sembuli, Haidary Abeid, Mohammed Kajole, Omar Kapera, Martin Kikwa, Nico Njohole, Mwinda Ramadhani, Leodgar Tenga, Jellah Mtagwa, Omar Mahadhi, Aluu Ally, Peter Tino, Abdallah Burhani, Rishard Adolph, Zamoyoni Mogella, Hamisi Gaga, Mohammed Salim, Salim Omar, Elisha John, Hillal Hemed, Malota Soma, Mohammed Hussein, Edibily Lunyamila, Kitwana Selemani, Fumo Felician nk nk nk.

Hao ndio walikuwa wachezaji wa mpira lkn hawa wa leo ni Nyambole tu.
 
Mkuu acha tu..

Tumeolewa...
😪😪
 
Manula kweli shati, kafungwa magoli ya hovyo kabisa.
 
Mohammed hussein Huyu huyu wa sasa wa simba?
 
Hizo ngonjera tu, hao unaowataja walienda kombe la dunia lipi?

Bongo hatujawahi kukosa vipaji vya soka tuna vipaji vingi ila changamoto haviendelezwi.. kipaji hiki hiki cha nyoni kucheza hapa na kina adam adam kisha kucheza na kina adama traore, cavani huko kuna vitu unapata..
 
Tanzania kwa siku hizi hatuna kabisa wachezaji wenye vipaji vya asili vya kusakata kabumbu tumebaki na watu wa kufanya "Show" kwenye vyombo vya habari na kupiga pesa. That's all.
Hatu kama talent ni muhimu lakini tunahitaji zaidi wachezaji wachezaji waliofundishwa kucheza soka toka utotoni, na wanaojituma mazoezini na uwanjani pengine kuliko hao wenye talent ya asili

Talent doesn't pay but hardworking does!

Ni kama kwenye muziki wetu.... Ali Kiba vs Diamond!

Wakati mmoja anategemea na kujivunia kipaji cha asili (though ninachokiona ni karama ya sauti), mwingine anajivunia hustle and hardworking!!

Lau kama hao wawili wangekuwa ni wachezaji soka na wewe unamiliki timu ya soka, sijui ungemsajili nani!!!
 

Hao kina Kibaden walishiriki world cup ya mwaka gani?
 
Unategemea ushinde kwa wachezaji akina Kibu, Mzamiru na Nyoni
Unategemea kweli Ushinde ukiwa ni Michezaji Mizuzu ( Mijuha ) kama Dickson Job, Bakari Mwanyeto na Feisal Salum Fei Toto?
 
Swala sio kucheza World Cup, swala ni quality ya mpira waliokuwa wakiucheza kipindi hicho na unaochezwa sasa hivi, ndicho nilichokuwa najaribu kuongelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…