Wakongwe wa hii platform jf mkuje na shout out kwenu

Wakongwe wa hii platform jf mkuje na shout out kwenu

Salamu wakubwa jaman nilikua na survey Kuna member since 2007 ndo natambaa sijui ila ivi mnajuaga kama Kuna watu wamepotea, au hatupo nao Tena ila muendelee kutupa madini nawaheshimu viongozi muendelee kuepo 💯.
Hongera kwa kutotumia muandiko wa kiafumbili soon ukikuwa wewe ni lishangazi linalojielewa.
 
Hatari sana mkuu. Kulikuwa na ile era kiatu kirefu unavaa sox hata pair 5. Yani buti linatangulua kabla ya wewe kufika kukuhakikishia usalama. Jeans bwanga na tshirt kubwa.
Ulikuwa unachana nini mkuu na wana guantanamo?
Alafu kipindi hicho mimi ndo dancer wa Guantanamo, oya sio poa nimevaa riboni mkononi, suruali ya kijeshi, na vestie nyeusi ikipigwa Ile nyimbo ya H. Baba, mpenzi wangu bubu

mume bwege, hakuna kulala la J. Nature, Hi la duly Sykes, amekoma q chief ft temba,dar mpaka Moro, bado kuna ile ya ay ft mwanafa, rayc na banana zori-ingia kati
 
Noma sana mkuu. Maisha ndivyo yalivyo. Mimi mwenyewe nililuqa producer enzi hizo na fl studio 3 yangu.
Lakini🤣nikijifikiria ety nilikuwa na ndoto za kuwa msanii mkubwa

Sasa nikiwa naenda studio tunalipa 60k Sasa nikiingia gheto nikijaribu kusikiliza zile ngoma, nasikia Yan saut mbaya kinoma
 
Lakini🤣nikijifikiria ety nilikuwa na ndoto za kuwa msanii mkubwa

Sasa nikiwa naenda studio tunalipa 60k Sasa nikiingia gheto nikijaribu kusikiliza zile ngoma, nasikia Yan saut mbaya kinoma
Umenichekesha saaana. Tuliwahi rekodi ngoma nlipoisikiliza nikaona mbona sauti mbaya nikawa staki hata watu waisikie. Nikawa nawaza mbona zinazotoka mj, pfunk hazisound kama za kwetu.
Daah maisha yako kasi sana.
Akili ikawa inanituma nikifka dar tu naenda bongo records na nishatoka
 
Kumbe uwa mnapenda kusalimiwa sikujua 😹😹😹🙌🏾
Mie sio napenda, mie mkubwa ujue.
Imagine mwanangu wa kike wa kwanza nimemzaa nikiwa primary mwaka 98.
Wa pili wa kiume nimemzaa 2007 na huyu wa tatu wa kike nimemzaa mwaka jana 2024, hapohapo nina mjukuu.
We huogopi Anastasia21 ?
 
Umenichekesha saaana. Tuliwahi rekodi ngoma nlipoisikiliza nikaona mbona sauti mbaya nikawa staki hata watu waisikie. Nikawa nawaza mbona zinazotoka mj, pfunk hazisound kama za kwetu.
Daah maisha yako kasi sana.
Akili ikawa inanituma nikifka dar tu naenda bongo records na nishatoka
Afu akili kila kijana anayo, kwamba ukienda dsm, unatoboa siku ya kwanza natua ubungo mara paap, na sweat kishenzi, mpaka zile begi zangu zinatoa jasho kufika pale gheto kwa mwana
Akasema welcome daslam asubuhi kila mtu kapewa chapati moja na maji ya moto hayana majani wala sukari, tukaambiwa hiyo ndo chai masela

Mshikaji mmoja pembeni akawa anapiga zake kuba(kuberi), mmoja anakula fegi akanipa pafu moja

(kumbe mimi situmii sigara Sasa Ikabidi nisilete unyonge kupiga pafu mbili) nikakohoa kishenzi 😅
 
Back
Top Bottom