Wakristo kitu gani kimewakuta mpaka mmeanza kuwaiga waislamu?

Wapi kwenye BIBLIA panaposema MUNGU ni mnyenyekevu

Kwanza soma Tito 2:13 utoe wenge then usome maneno ya Yesu kwenye Mathayo 11:29 akisema " Jitieni nira yangu, mjifunze toka kwangu kwa kuwa Mimi ni mpole na MNYENYEKEVU wa moyo,nanyi mtapata raha nafsini mwenu
 
Zaidi ya yote, kila mtu aamini akitakacho ila tusilazimishane, mimi huwa nakerwa na wale ambao hulazimisha dini yao na miungu yao iabudiwe na kila mtu, na wanatumia upanga kulazimisha, na ndio wamekosesha amani duniani kwa huo upimbi wao.
 


Kaka kwa mujibu wa imani yako? Je kuna kitu chochote ambacho Mwenyezi Mungu hana uwezo wa kukifanya?
 
Dini ni njia. Utasemaje Ukristu siyo dini?
Afrika sio nchi ila ndani ya Afrika kuna nchi nyingi, ukristo sio dini ila ndani ya ukristo zipo dini (thehebu ) tofauti tofauti . Zingatia kuwa ukatoliki sio usabato , wala upentecoste sio ukkt...hawa wote kila mtu ana namna na taratibu z/yake ya kuabudu ...but wote ni wakristo!
 


Nakupongeza sana, inaitaji akili kubwa sana Kuyajua haya

"1. Ukristo ni imani ila Uislamu ni dini( mfumo wa maisha)

2. Uislamu umekaa kisheria na kisayansi zaidi kuliko " imani" lakini Ukristo umekaa kiimani zaidi kuliko sayansi na sheria. Ndio maana waislamu husema hadi sayansi inaweza kuthibitisha kwamba Qur'aan Tukufu, lakini huwezi sikia wakristu wakisema Biblia inaweza kuthibitishwa kisayansi..


3. Wakristu hawana dini ila wana imani.

4. Waislamu wana dini lakini hawana imani"
 
Kwanza soma Tito 2:13 utoe wenge then usome maneno ya Yesu kwenye Mathayo 11:29 akisema " Jitieni nira yangu, mjifunze toka kwangu kwa kuwa Mimi ni mpole na MNYENYEKEVU wa moyo,nanyi mtapata raha nafsini mwenu
Wewe unasoma Biblia juu juu tu...

Tito 2:13 katika Agano Jipya linasema, "tukitarajia tumaini lenye baraka, yaani, kufunuliwa kwa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo."

Wapi hapo kwa Tito kuna neno MUNGU
ananyeyekea, hapo kwa TITO wanazungumzia nafsi mbili tofauti yani MUNGU MKUU na YESU KRISTO, wote wawili.

Mathayo 11:29 katika Injili ya Mathayo inasema, "Jifungeni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu."

hapo Katika kitabu cha mathayo, anayezungumza ni YESU, kwamba tujifunze kutoka kwake kwa sababu yeye ni mpole na mnyenyekevu. Hapo hazungumzi MUNGU MKUU, kwa sababu yeye hana wa kumnyenyekea. YESU ndio mnyenyekevu mbele za MUNGU.

BIBLIA sio ya kuivalijia Msuli, Biblia unatakiwa ukae usome na kuelewa neno kwa neno
 
Matendo gani ameyafanya?
 
Dini hapo ni Ukristo, hayo Mengine kama wasabato, wakatoliki, walutheri, na wengineo ni Madhehebu tu...

Acha kupotosha watu
 
"Mt 11:29 SUV
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu".

Huyu ni Mungu,aliuvaa mwili,akala chakula,akanya,akapata kiu etc.
Huyu alibakisha kuoa tu angekuwa anat*mber kama binadamu wafanyavyo.
 
Hiyo Tito

Hiyo Tito2:13 umeitwist mkuu. Nilitaka nikupe maandiko zaidi lakini naona itakuwa ni kazi bure kwa sababu uta ya twist tena.
 
Sasa mbona kuna mahali Yesu anatambulika ndiye Mungu Mkuu?
 
Umeitwist mkuu
 

Attachments

  • Screenshot_20231210-125911.png
    59.3 KB · Views: 6
Wa
Warumi 9:5
 

Attachments

  • Screenshot_20231210-125759.png
    39 KB · Views: 6
Mmh!!! Wa christu wana Iman ila hawana Dini ila waislamu wana Dini ila hawana Iman, its confusing to understand fafanua zaidi
Amefanunua vizuri kupata mwanga ni somo kubwa ukitafuta kufahamu hakika utaelewa
 
Dini ni njia. Njia ina sheria na amri zake.
Ukristo sio njia kwa sababu hauna sheria wala Amri.

Ukristo ni kama wewe utokee kumuamini Gwajima alafu muitwe Wagwajima, yaani wafuasi Wagwajima
Hakuna njia isiyo na kanuni ya kuzifuata. Labda mnahangaishwa na swala la Utamadunisho, hivyo mkatamani dini inayofuata utamaduni wa watu fulani huku waumini wake wakitakiwa kuufuata utamaduni wa nchi fulani.
Katika Ukristo watu walitenganisha imani na utamaduni.
 
Elimu nzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…