Wakristo Kwanini tunakula viumbe vyote ambavyo Mungu aliruhusu lakini tunachagua na kubagua vilivyokatazwa akiwemo Nguruwe?

Wakristo Kwanini tunakula viumbe vyote ambavyo Mungu aliruhusu lakini tunachagua na kubagua vilivyokatazwa akiwemo Nguruwe?

Soma vifungu hivyo vya Biblia kamakweli una nia ya kujifunza la sivyo kabishane huko Facebook ndio level zako.Kwa kifupi Biblia haikatazi kula vyakula aina fulani vyote vinaruhusiwa kwa Mkristo isopokua Biblia imeweka uhuru kulingana na utamaduni wa jamii husika.Kwa mfano wachina wanakula Punda lakini Tanzania inaonekana sio utamaduni wala Mila zetu
Maneno haya ya Paul yana madaraka yapi ya kubadili sheria za Mungu, ni wapi kapewa kibali kutengua sheria za vyakula safi na najisi ?

Au sababu tu umeona kimendikwa nawe unapita nacho tu bila kukichuja kwenye ubongo, kweli kabisa umeona Paul ndo wakubatilisha sheria za Mungu, you cant be serious !!

Nikupe formula rahisi tu, Sheria za Mungu hazibadiliki na hata Yesu aliweka wazi hajaja kuzibadili. ukiona sehemu zilibadilishwa bila kibali cha aliezitengeneza jua kuna viulizo hivyo ni vema uendelee kuzifuata za Mungu,
 
ufugaji-wa-nguruwe-1-1024x1024.jpg

Huwa nashangaa sana ni vipi kila kiumbe ambacho Mungu alituruhusu kula huwa kinalika bila tatizo na ni salama kwetu lakini linapokuja suala la viumbe ambavyo alivikataza huwa kuna ubaguzi, mfano viumbe kama nzi, nyau, punda, mjusi na panya watu wanabagua lakini kwa wakati huo huo wanakula vingine vilivyokatazwa kama nguruwe na nyau, ni kwanini ?

Wanyama safi na halali kuliwa ni wenye sifa hizi zote : kwato katika miguu yake + mwenye miguu ya kupasuka kati + mwenye kucheua,.... wanyama kama sungura, nguruwe na paka hawaruhusiwi

Samaki walio halali kuliwa na watu ni lazima awe na mapezi + magamba

Ndege wote wanafaa kasoro - tai, furukombe, kipungu, mwewe, kozi, kunguru, mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga, bundi, mnandi, bundi, mumbi, mwari, mderi, korongo, koikoi, hudihudi, popo.

Wadudu halali kwetu ni wale wenye miguu mirefu maalum kwajili ya kuruka juu na chini kama panzi, senene na nzige

Reptiles wote hawafai : chura, nyoka, vinyonga, kenge, n.k.
⚖️Mungu hawezi kamwe kushughulika na vitu vidogo vya kumpangia binaadamu nini Cha kula na nini usile.

⚖️ Suala la vyakula vinabaki katika tamaduni za Kila jamii,na Kila jamii Ina tamaduni zake kuhusu vyakula.

⚖️Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba sii Kila kilichoandikwa kwenye hivi vitabu viwili vya Abrahamic religions ( Christians and Muslims) ni maneno ya Mungu, hapana yapo mengi yameandikwa ambayo ni Mila na tamaduni za sehemu hizo dini hizo zilivyoanzia.

⚖️ Kamwe haikuwa mpangilio wa Mungu tuwe na Mila za aina Moja, vyakula vya aina Moja na Mavazi ya aina Moja, ndio maana alituweka sehemu yenye mazingira tofauti na hapo akatupa vitu kulingana na Hali ya kijografia aliyoipa Kila jamii.

⚖️Manabii walioshukia maeneo hayo, hawakuwa na haja Wala muda wa kupbana na Mila walizozikuta waliishi nao hivyo hivyo ili jamii isiwaone wa ajabu.

⚖️ Mathalani, dini zingeanzia umasaini ungekuta samaki imeandikwa ni haramu, na Vazi rasmi la ibada lingekuwa rubega badala ya kanzu,au zingeanzia Moshi ungekuta vinywaji mbege badala ya divai na ndizi badala ya mkate.

⚖️ Yaani Kuna mamtu ubongo mwepesi kumwrlewa Mungu yamekuwa yakikariri tamaduni za kiarabu na kiyahudi kuanzia namna ya kukaa kwenye nyumba za ibada, Mavazi, vyakula mpaka lugha wanamwomba Mungu kwa lugha ya kigeni, wanataka kumwambia Mungu kuwa Lugha za mama alizotupa ili kuwasiliana naye hazijui na hivyo wanakariri lugha za watu na kumeomba nazo. Huo ni mtindio wa ubongo.

⚖️ Yapo makabila hawali kondoo wengine wanakula, wengine hawali Bata wengine wanakula, wengine sehemu Fulani za mnyama hawali kama moyo figo wengine wanakula. Kuna sehemu za mnyama huliwa na wanawake tuu na nyingine huliwa na wanawake. Kama kabila lako au koo kula mdudu ni ruksa wewe gonga achana na ma Mila ya kizamani ya kiyahudi na kiarabu. Mungu kaba wanyama wote kwa ajili yetu
 
Ni madhehebu machache yanafuata hizo sheria, Ni mambo ambayo ukitumia akili ya kawaida kabisa unaona ni wazi ni heri kula vyakula vilivyoruhiswa na Mungu tu
Kikubwa hapo naona ni siasa za kijamii tu na mapokeo..... Kama hufi na hakiathiri afya yako we peleka motoo
 
Paul haya maneno alikuwa anayaongea kwa madaraka yapi ?

Maneno haya ya Paul yana madaraka yapi ya kubadili sheria za Mungu ?
Nilijua tu msabato huwezi kujificha kwenye kichaka cha Usabato😀😀....kama hukubaliani na mafundisho ya Mtume Paulo basi fanya kunyofoa vifungu hivyo vyote vya Biblia nadhani utakua kwenye nafasi nzuri zaidi🤣🤣
 
Unaposoma biblia jiongeze, ukiisoma kichwa kichwa utaamini kwamba hata yesu alisafisha vyakula vyote wakati yeye mwenyewe alishasema hajaja kubadili sheria zozote za baba yake, hata yale mabano ya lwa kusema hivi alitakasa vyakula vyote ni mawazo ya watu wengine wala Yesu hahusiki.

Biblia sio story ya kusoma ama shairi la kukariri, ni kitabu cha kukisoma kwa kuelewa.

Utazunguka weee ila tunarudi pale pale

ni kwanini kila chakula ambacho kiliruhusiwa na Mungu kinaliwa bia tatizo lakini si kila kilichokatazwa kinaliwa ?

Wewe unaweza kula nzi za chooni ?
 
Wasabato kila siku unaanzisha Uzi
 
ufugaji-wa-nguruwe-1-1024x1024.jpg

Huwa nashangaa sana ni vipi kila kiumbe ambacho Mungu alituruhusu kula huwa kinalika bila tatizo na ni salama kwetu lakini linapokuja suala la viumbe ambavyo alivikataza huwa kuna ubaguzi, mfano viumbe kama nzi, nyau, punda, mjusi na panya watu wanabagua lakini kwa wakati huo huo wanakula vingine vilivyokatazwa kama nguruwe na nyau, ni kwanini ?

Wanyama safi na halali kuliwa ni wenye sifa hizi zote : kwato katika miguu yake + mwenye miguu ya kupasuka kati + mwenye kucheua,.... wanyama kama sungura, nguruwe na paka hawaruhusiwi

"Sifa za viumbe wengine"

Samaki walio halali kuliwa na watu ni lazima awe na mapezi + magamba

Ndege wote wanafaa kasoro tai, furukombe, kipungu, mwewe, kozi, kunguru, mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga, bundi, mnandi, bundi, mumbi, mwari, mderi, korongo, koikoi, hudihudi, popo.

Wadudu halali kwetu ni wale wenye miguu mirefu maalum kwajili ya kuruka juu na chini kama panzi, senene na nzige

Reptiles wote hawafai : chura, nyoka, vinyonga, kenge, n.k.
Kuna Hali ya kupindisha maagizo ya Mwenyezi Mungu Ili watu waweze kuishi vile wanavyotaka mfano,hata katika biblia imeelezwa mwanamke kufunika nywele zake means kichwa chake lakin hatuyafuati hayo imekua kama ni namna ya kumtofautisha muisilam na mkristo...Leo hii ukienda kanisani utachoka uvaaji imekua mbovu sana,watu wanavaa mavazi hayana sitara,kiasi kwamba inaweza mtoa mtu mwingine kwenye uwepo wa ibada,simu ikiita mtu anatoka nje kupokea ama apokee hapohapo....Aiseee eniwei
 
Unachekesha sana wewe msabato ....nani kwakwambia kitimoto ni najisi😀😀

Mathayo 15:11
kinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.”
Naona mnabishana wenyew kwa wenyew. Haliyakuwa wote mnatumia kitabu kimoja.

Lkn kitabu chenyew huku kimeandika ni najisi huku kimehalalisha. Sasa watu (wakristo) washike lipi waache lipi?
 
Kuna Hali ya kupindisha maagizo ya Mwenyezi Mungu Ili watu waweze kuishi vile wanavyotaka mfano,hata katika biblia imeelezwa mwanamke kufunika nywele zake means kichwa chake lakin hatuyafuati hayo imekua kama ni namna ya kumtofautisha muisilam na mkristo...Leo hii ukienda kanisani utachoka uvaaji imekua mbovu sana,watu wanavaa mavazi hayana sitara,kiasi kwamba inaweza mtoa mtu mwingine kwenye uwepo wa ibada,simu ikiita mtu anatoka nje kupokea ama apokee hapohapo....Aiseee eniwei
Mambo mengi hua mnajionea wenyew, lkn mnashindwa kutafakari na kuwaza na kutumia akili.
 
S
Kwani nguruwe kawakosea nin, mim nimeanza kula NGURUWE tangu niote meno adi sasa ivi naitwa baba sijawai kuiona iyo dhambi Physically wala impact yoyote juu ya iyo nyama.

ata ivyo nimetoa oda ya nusu kilo na viazi vya 2000 muda huu nipo nasubiri nishushie na Kvant.

nakeleka sana na izi mada za kumuhusu uyu mpendwa wetu. izo dhambi mbona hatuzioni zinavyotukumba tulapo,
Sawa sawa mzee
 
Maneno haya ya Paul yana madaraka yapi ya kubadili sheria za Mungu, ni wapi kapewa kibali kutengua sheria za vyakula safi na najisi ?

Au sababu tu umeona kimendikwa nawe unapita nacho tu bila kukichuja kwenye ubongo, kweli kabisa umeona Paul ndo wakubatilisha sheria za Mungu, you cant be serious !!

Nikupe formula rahisi tu, Sheria za Mungu hazibadiliki na hata Yesu aliweka wazi hajaja kuzibadili. ukiona sehemu zilibadilishwa bila kibali cha aliezitengeneza jua kuna viulizo hivyo ni vema uendelee kuzifuata za Mungu,
........
 
VYAKULA NA VINYWAJI VILIVYO HARAMU KATIKA UISLAMU.

Vyakula vyote visivyo haramishwa katika Qur-an na

Vyakula vilivyoharamishwa katika Qur-an:
Mnaharamishiwa nyamafu na damu na nyama ya
nguruwe na mnyama aliyechinjwa si kwa ajili ya Allah,
na kilichokufa kwa kusongeka koo, na kilichokufa kwa
kupigwa, na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufa
kwa kupigwa pembe (na wanyama wengine), na
alichokila mnyama ila mkiwahi kukichinja. Na (pia
mmeharamishiwa) kilichochinjwa panapo fanyiwa Ibada
isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu (kama mizimu)… (5:3).

Aya hizi za Qur-an pamoja na (6:145) zinatupatia
mafunzo yafuatayo juu ya vyakula vilivyoharamishwa:
1. Mnyama aliye kufa bila ya kuchinjwa kwa sababu
yoyote iwayo (mzoga).
2. Mnyama asiyechinjwa kwa jina la Allah –
Tumeamrishwa katika Qur-an:

Basi swali kwa ajili ya Mola wako na uchinje (kwa ajili
ya Mola wako). (108:2).

Kutokana na amri hii si halali kula nyama ya mnyama
aliyechinjwa na Kafiri, Mshirikina au yeyote asiye Muamini
Allah (s.w) na Upweke wake. Nyama itakuwa halali iwapo
mchinjaji ni Muislamu atakaye chinja kwa jina la Allah –
Bismillah Allahu Akbar na atakayezingatia masharti ya
kuchinja ya kumkata mnyama koo (shingo) kwa kisu kikali
au kitu chochote cha kukatia kilicho kikali.
Muislamu yeyote awe mtoto, mwanamume au
mwanamke katika hali yoyote anaruhusiwa kuchinja. Wala
hapana suala la kupewa kisu na Sheikh.

3. Mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya matambiko,
mashindano, n.k. mnyama huyo maadam kusudio
la kuchinjwa kwake ni kumshirikisha Allah (s.w)
nyama yake ni haramu kuila hata kama mwenye
kuchinja anajiita Muislamu na ametaja jina la Al-lah wakati wa kuchinja.
4. Nyama ya nguruwe.
5. Damu inayomwagika – damu inayobakia kwenye
nyama si haramu.

Vyakula vilivyoharamishwa katika Hadith
6. Wanyama na ndege wote wanaowinda wengine kwa
makucha na meno au midomo yao ni haramu kula
nyama yao kwa mnasaba wa Hadith zifuatazo:

Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah
amesema:“Kila mnyama awindae kwa meno ni haramu
kuliwa” (Muslim)
Ibn Abbas ameeleza kuwa Mtume wa Allah aliharamisha
kila mnyama awindaye kwa meno na kila ndege
anayewinda wengine kwa kucha. (Muslim)
Wanyama wanaowinda kwa meno na kucha ni kama
simba, chui, paka, fisi, vicheche, mbwa mwitu, n.k.
Ndege wanao winda kwa makucha ni kama tai,
mwewe, kipanga, n.k.
7. Nyama ya punda wa nyumbani, farasi na nyumbu
ni haramu kwa mnasaba wa Hadith ifuatayo
Khalid bin Walid ameeleza kuwa Mtume wa Allah
ameharamisha nyama ya farasi, nyumbu na punda wa
nyumbani. (Abu Daud, Nisai).
Bali nyama ya punda milia ni halali kama
tunavyofunzwa katika Hadithi ifuatayo:

Abu Watadah ameeleza kuwa alimchinja pundamilia
(punda wa porini). Mtume (s.a.w) akamuuliza:
Unachochote katika nyama yake?” Alijibu: Tuna miguu
miwili ya nyuma. Kisha alichukua na kula. (Bukhari na
Muslim).
8. Nyama ya wanyama wachafu wenye kuathiri mwili
na utu kama nguruwe, mbwa, paka, n.k.
Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah
ameharamisha nyama na maziwa ya wanyama wachafu.
(Tirmidh).
9. Ni haramu kula nyama ya mjusi na jamii yote ya
mijusi:
Abdul-Rahman bin Shibl amesimulia kuwa Mtume (s.a.w)
ameharamisha nyama ya mijusi. (Abu Daud).

10.Nyama ya paka ni haramu:
Jabir amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) ameharamisha
nyama ya paka na kumpiga bei.
11.Nyama ya kiungo cha mnyama kilichokatwa
mwenyewe akiwa yungali hai kama vile mkia wa
kondoo, mguu wa mnyama uliokatika kwa ajali, n.k.
ni haramu kwa mnasaba wa Hadith ifuatayo:
Abu Waqidil Laysi ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alikuja
Madina akawakuta wanapenda nundu za ngamia na
kukata mikia ya kondoo. Mtume (s.a.w) akasema: “Kile
kilichokatwa kwa wanyama wakingali hai ni mzoga. Ni
haramu kuliwa”. (Tirmidh, Abu Daud).
12. Ni haramu kula wadudu isipokuwa nzige kwa
mujibu wa Hadith ifuatayo:
Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
Mizoga ya aina mbili na damu za aina mbili, vimefanywa
halali kwetu: Mizoga ya samaki na nzige na damu ya
maini na wengu. (Ahmad, Ibn Majah, Darqutni).
Hivi ndivyo vyakula vilivyo haramishwa katika Qur-an
na Hadith lakini Muislamu atakaposongwa na njaa ya kufa
na kupona na pakawa hapana njia yoyote ya kupata
chakula, ameruhusiwa kula haramu kiasi kidogo cha
kumuwezesha kuishi na wala asile kwa kufurahia kama
tunavyojifunza katika Qur-an:
“… Lakini aliyelazimika (kula kwa ajili ya njaa, n.k.)
pasipokupenda wala kwa kuvuka mipaka, basi,
Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na mwingi
wa kurehemu. (6:145)

Vinywaji vilivyoharamishwa
Vinywaji vyote vinavyolevya (intoxicants)
vimeharamishwa hata kuonja.
Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa
(na kuombwa) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na
kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwa
vinginevyo); (yote haya) ni uchafu (ni) katika kazi ya
shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufaulu
(kutengenekewa). (5:90)
Ulevi, kamari, kumshirikisha Allah na kutazamia ni
matendo yanayoivuruga jamii na kuifarikisha:
Hakika shetani anataka kukutieni uadui na bughudha
baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari na anataka
kukuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na
(kukuzuilieni) kuswali. Basi je, hamtaacha haya)? (5:91).
Vinywaji vyote vinavyolevya na vilivyo najsi kama vile
damu, mkojo, n.k. vimeharamishwa kunywewa hata kwa
dawa kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Waili al-Hadhrami ameeleza: Tariqa bin Suwaid
alimuuliza Mtume (s.a.w) juu ya ulevi. Mtume (s.a.w)
aliuharamisha. (Tariqa) akasema hakika natengeneza
ulevi kwa ajili ya dawa. Mtume (s.a.w) alijibu: Huo si
dawa bali ni ugonjwa. (Muslim).
Ulevi ni haramu ukinywewa kwa wingi au kwa uchache
kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Jabir ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Kinacholevya ni haramu kikiwa kingi au kidogo.
(Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).

Nmeikopy huko google.
 
Back
Top Bottom