Wakristo mjitafakari kwenye suala la mahari, mnawakosea sana binti zenu. Kilichotokea hivi karibuni kwa jamaa yangu kina funzo

Kwa taarifa yako ukristo haujaweka mahari bali kila kabila lina viwango vyake vya mahari!

Jielimishe!
 
Umenipa hoja zako wapi? Post namba ngapi? Thread ipi? Nitajuaje wewe si muongo tu?

Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Unakosea kuingiza ukristo kwenye mahari. Kwenye ndoa za kikristo mahali huwa ni issue ya kimila, tena Mila za kabila la bibi harusi mtarajiwa. Wakimalizana ndo wanaenda kanisani kutangaza ndoa issue ya mahari haiwi topic tena na wala haiuliziwi kanisani.
 
mkuu nikili kwamba ulicho ongea ni ukweli mtupu, mwaka 2017 nilitaka kuoa na nilikuwa na mahusiano na binti fulani hivi ambaye alitoka kijijini alipo fija mjini nikambrashi na mitoko,pamba hata pesa, maana nilikuwa na kijiajira, baada ya kwenda kuuliza mahari kwa tetesi tu bila ya mshenga nikaambiwa milioni 1.8.
Basi nikapotezea hapo binti kashanawili uno snura wana wakaanza mtamani mara wakapita naye me nikajiweka kando.
Mwaka jana nilitokea kumpenda mdada mwingine nikasema round hii siwekezi kwa binti basi kumudokezea muhusika swala la posa kuuliza wazazi walizi na sio wa kumzaa wakamwambia bila milion 2.3 asisubutu kusogea hapa tutamuaibisha, harafu demu fundi nguo tu, aisee ilinibidi ninyooshe mikono,
Ukweli wakristo batmdo tunashida ya tamaa inayotusumbua
 
Unakosea kuingiza ukristo kwenye mahari. Kwenye ndoa za kikristo mahali huwa ni issue ya kimila, tena Mila za kalila la bibi mtarajiwa. Wakimalizana ndo wanaenda kanisani kutangaza ndoa issue ya mahari haiwi topic tena na wala haiuliziwi kanisani.
Sio kweli mkuu, mimi ni mkrosto na unapozungumzia mahari kwa sehemu moja au nyingine lazima uongozi wa kanisa uhusike na uthibitishe
 
Hivi wakristo mahali wanapanga wazazi au anaeolewa ndo anataja mahari??
Hakuna mahari Kwa Wakristo, Bali makabila na mila zao, inatokea Sasa mkristo ndio anaolewa mahari inapangwa na familia Kwa mujibu wa mila na desturi zao, mkaja wa mama ni mama mwenyewe ndio anatakamka anataka how much vyote vinaorodheshwa kwenye barua ya majibu ya poss anapewa Mshenga mkajipange.

Unapokwenda kutowa mahari maana yake umekubaliana na yaliyoandikwa kwenye barua ya majibu.
 
Huo uwezo ndo kias gan? Unahisi kiasi gani kinatosha na kwa kuzingatia kipimo kipi?
Uwezo wa kulipa maharj au kupangia mtu mahari unatakiwa uangaliwe kwa pande zote mbili, muozeshaji na muoaji. Kwa family zingine zilizostaarabika binti ndo huwa anawapa mwanga wazazi wake juu ya uwezo au hali ya mchumba wake pale wanapotaka kupanga mahari.
 
Kaka hapa nakazia aisee kuoana na mtu wa dini tofauti ni shida kidogo. Issue inakuja kwa wazazi na kwa wanandugu. Imetutokea kwa familia yetu baada ya kaka kuchumbia binti wa kiisilamu kutoka kigoma. Imekua issue sana mpaka wakaamua k7zaa tu waendelee kuishi.
 
Sawa, kaoa huyo wa mahari elfu 40 ila moyo wake uko Uganda.
Wanaume hatuna huu utaratibu, akili mbele hisia nyuma. Upendo unatengenezwa na hata huyu wa 40 nikampenda vile vile na ukiangalia uyo mwengine ni fimbo ya mbali ndo kabisaaaa
 
Tanzania makabila mengi,hasa ya Pwani,wamechanganya dini.Unaweza ukaona ukoo mmoja,mjomba mkristo,mama muislamu,baba mkubwa mkristo,baba mdogo muislamu.Na watoto wa ukoo huo huo wamo waislamu na wapo wakristo.Wapo majirani niliishi nao hivyo,ni ndugu,hawa wanakwenda kanisani,wale wanakwenda msikitini.Na wapo wengi tu.
 
Hapana bhana, hata Bakhresa asingependa binti yake azalie nyumbani kwa namna yoyote ile na hapa ndipo thamani ya mwanamke inapopimwa na hapa ndipo hiyo unayoita bei ya kutupa inapoingia
 
Kwamba jamaa yako kabadilishwa dini na mbususu tena ya form four aiseee na unakuja kujisifia hapa. Si angebadili tu tangu mwanzo kuliko kutaka kujibebesha mganda asiyemuweza.
Hapa mkuu tunaweza kusema hakuna ndoa kwa wale tunaojua! najaribu kutafuta lugha ya kusema ambayo haitagusa maumivu kwa muoaji siioni lakini kwa kifupi ajitafakari uamuzi aliofanya:-
  1. alitakiwa kumpa taarifa tena ingewezekana official kupitia mshenga kwa familia kuwa kwa mahali hiyo hatutakuwa tayari kuoa na familia itafakari upya. vinginevyo hakumpenda toka mwanzo.
  2. maamuzi ya kuoa mke mwingine na kwa muda uliotaja umetumia zaidi mission na si vision kwa lugha rahisi maamuzi yaliangalia hitaji la sasa na kufanya maamuzi. akili ilitumika zaidi kuliko busara.
  3. mwanaume hana maamuzi na msimamo anayumba mazingira ya ndoa kufa ni makubwa sana vinginevyo ajipange sukari na pressure siku zijazo
 
Ooh sawa
 
Juzi nilikuwa kwenye "wedding reception" ya wanandoa wa kiislam. Bajeti ilikuwa zaidi ya 50M na maharusi waliweka na mabango ya picha zao katikati ya mji. Harusi ndogo au kubwa ni utashi wa mtu binafsi na sio dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…