Umekusudia kuutukana ukristo? Ona hoja zako mfu hapa ambazo zinaonyesha jinsi gani unaleta hadithi za kutunga zisizo na mashiko:
1. Rafiki yako single father watoto watatu. Mama wa watoto hao watatu yuko wapi?
2. Single mother mtoto mmoja, baba wa mtoto yuko wapi?
3. Walikuwa marafiki chuoni (wapenzi)? Wapi Ukristo unaruhusu uchafu huo?
4. Hilo suala la mahari ya waganda lina uhusiano gani na Ukristo? Ni wapi kuna maelekezo ya kudai kiwango fulani cha mahari? Hoja za kipuuzi kweli kweli.
5. Huyo muoaji alitakiwa kusikitikia bajeti yake, kwamba amevamia mila za watu bila mwongozo sahihi. Muache kukurupuka, mambo haya hufanywa kwa utaratibu.
6. Akasema alitegemea watasema.... Kwani mlikwenda kupeleka posa mpangiwe mahari au mlikwenda kuwaeleza kile mlichokuwa tayari kulipa? After all mahari ya MWANAMKE tena mwenye mtoto haiwezi kuwa hicho ulichosema, ni uongo dhahiri. Mengine tuwaachie waganda na mila zao, sasa Ukristo unaingiaje hapo ewe usiye ufahamu?
7. Nilitegemea utasema "WAKATI KATIKA UISLAMU KUTOMALIZA MAHARI NI HESHIMA KUBWA.... " Kumbe umejichanganya mwenyewe, unadai Tanzania ni heshima kutomaliza mahari, kwani Tanzania ni ya Waislamu na Uganda ni ya Wakristo? Una matatizo ya logic kwenye hoja zako.
8. Sasa huyo mtu wenu alikuwa muoaji kweli au ni mhuni tu? Pia ninyi wasindikizaji feki ni genge la malaya tu, eti mngeshangaa kama hana alternative!? You're fake!!
9. Ok, kwa akili yako ukaona ni wakati sahihi kutuingizia character wako muislamu kwenye utunzi wako. Eti kwao wanataka ndoa ya Kiislamu, hapa unamaanisha ndoa za Kiislamu hazina mahari?
10. Mwanamume aliye tayari kwa ndoa, amekwisha kujichagulia mchumba hawezi kamwe kubadili gia angani sekunde moja baadaye kutaka mwanamke mwingine. Hii ni dhahiri huyu hakuwa muoaji, ama utunzi umepwaya.
11. Form four, anaweza kuwa bikira. Kamaliza shule gani huyo? Huyu jamaa yako alidai anaye mchumba mwingine, alimposa lini? Kwa hiyo alikuwa na wanawake wawili akisubiri mwenye unafuu wa mahari? Baada ya kufeli kwa mwanamke wa kwanza akahamia kwa wa pili, huyu jamaa hakuwa na mpango wa kuoa licha ya sifa feki ulizommwagia. Genge la wahuni tu.
12. Mwanamke wa Kiganda ama wa kikristo aliyechanganyikiwa? Umeshutumu ukristo kwa mila za Kiganda?
12. Sasa hapo kwenye hitimisho la upuuzi huu unajazia "ukristo" wakati kwenye andiko lako umebainisha utofauti wa ndoa za Kiganda na za Kitanzania, hivi kichwa chako kinawaza sawa sawa? Hakuna hata sehemu moja umeonyesha uhusika wa viongozi wa kikristo kwenye mchakato wa mahari. Sasa ukristo ujifunze nini kwenye Uislamu?
13. Tofauti ya ndoa za kikristo na nyinginezo ni mchana na usiku. Kwa mfano ndoa nyinginezo (ikiwemo uislamu) ni mikataba ambayo yaweza kuvunjwa wakati wowote lakini ndoa za kikristo ni AGANO LA MAISHA. Hili huvunjika pale tu upande mmoja unapokufa.
14. Mahari ni utamaduni wa kibiblia ambao huashiria nia njema ya muoaji. Pia ni shukrani kwa mzazi kwa malezi bora kwa binti yake. Maandiko hayaweki kiwango cha mahari stahiki, hilo limeachwa kwa jamii husika. Kuutuhumu ukristo kisa mlishindwa kulipa mahari ya Kiganda ni upotofu wa fikra. Yakobo alitumika miaka 14 ili kumpata mkewe aliyempenda sana, sasa huyo jamaa yako safari moja tu ya Uganda imeanzisha mada 'JF. Badala ya kurudi na kupanga hoja ili mwishowe ampate yule ampendaye eti akaona aoe muislamu! Kizazi cha hovyo kweli kweli.
15. Ukusudia wanawake wengi wasio na ndoa duniani ni Wakristo? Kwa utafiti upi? Huu nao ni upuuzi mkubwa. Unataka kumaanisha hata wanaume wa kikristo hupendelea kuoa wanawake wa Kiislamu? Hello, jaribu tena. Wewe si mtunzi mzuri.
Kama hujaoa nakushauri usithubutu kwani hujajua ndoa ni nini. Huo ushauri wako ni wa kijinga kabisa, kama sababu za binti kukubali kuolewa ndio hizi, basi hakuna haja ya kuolewa!! Mtu anayekuja akiwa na 'option' mbili au tatu sio mwoaji, ni malaya kama malaya wengine tu. Tofauti ni kwamba huyu ameamua kuhalalisha umalaya wake kwa kumweka ndani binti wa watu huku moyo wake ukitangatanga hovyo.
Mwanamume anapohangaika kumpata mke ni dalili ya upendo kwake na mara nyingi ndoa za aina hiyo hudumu. Kwa familia yenye maadili kuoa sio hisani kwamba unaisaidia familia. Wewe na huyo jamaa yako bado mna safari ndefu ya kujifunza maana na maisha ya ndoa. Pole sana.