Hainiingii akilini kwa nini wakristo wanaoamini kwamba Yesu ameshinda mauti lakini ikitokea mmoja wetu amefikia mwisho wa uhai wake tunakisujudia kifo badala ya kutangaza ushindi juu ya kifo. Nimekulia kwenye kanisa Katoliki na hizi nyimbo za maombolezo zinanitia kisirani kabisa. Fikiri wimbo wenye maneno kama haya za kuudhalilisha ushindi wetu dhidi ya kifo:
- SHUKA LANGU NA BLANKETI LANGU NI UDONGO MZITO, WANIELEMEA
Kweli kabisa? seriously? Maiti anaelemewa na udongo uliomfukia? Akili ya wapi hii ya kuongeza huzuni isiyokuwa na ukweli?
Kwa nini wakristo hatuimbi nyimbo za ushindi juu ya kifo kama tunavyoahidiwa katika imani yetu? Nawasihi sana hasa kanisa katoliki jirekebisheni kwenye hili. Nyimbo hizo zinaongeza huzuni badala ya kuleta faraja kwenye msiba.