Wakristo: Vita ya Israel inayoendelea ni ishara tosha kuwa wakati wa kuja kwake mwana wa Adamu (YESU) umekaribia. Tuamke

Mungu alishindwa vipi kuiumba dunia isiyo na migogoro? Alishindwa vipi kumzuia shetani asilete uasi wake humu duniani? Alishindwa vipi kuzuia mateso wanayopitia watoto walioko Gaza ambao hawana dhambi yoyote?

Siku ya hukumu ikifika (kama kweli ipo), nitamwambia face to face, hakwepi lawama kwa haya yanayotokea duniani.

Kama ambavyo mpishi anabeba lawama chakula kikipikwa vibaya, ndivyo ambavyo Mungu anatakiwa kuwajibika kwa kuumba ulimwengu pamoja na walimwengu wenye madhaifu!


With all your mighty powers, you could have easily fix all this shit dear God. Why leave it all to me?
 
acha mibangi yako hicho kinachoendelea hapo mashariki ya kati ni sababu ya kuwa na binadamu wajinga na uncivilized haiwezekani mkakubali kuumiza maelfu ya watoto na wanawake kwa sababu ya vitabu vya dini vilisema hivi..stupidiii!
 

mkuu maswali yako yanaonesha ni dhahiri hujasoma na hujafanya utafiti wa kutosha kuhusu haya mambo.

Fahamu ya kuwa ugomvi wa Israel na Palestine ni imani

S
asa tafiti kuanzia hapa ...iweje imani izue ugomvi wote huu usioisha Karne na Karne? Ukijibu hili swali itakufaa.
 
acha mibangi yako hicho kinachoendelea hapo mashariki ya kati ni sababu ya kuwa na binadamu wajinga na uncivilized haiwezekani mkakubali kuumiza maelfu ya watoto na wanawake kwa sababu ya vitabu vya dini vilisema hivi..stupidiii!
Mawazo kama mawazo!

Kwamba vitabu vya dini ni stupid!
 
Sikupingi hata kidogo mkuu ila mbona huku nilipo kuna watu bado hata hawajasikia jina la huyu Yesu, nikiwa na maana ya kwamba iliandikwa kuwa kila kiumbe lazima kiwe na taarifa hii
 
Umeotah!! Hadi uandike gazeti!!
 
Nilichokiandika hakihusiani na imani. It's just simple common sense. And it goes beyond Israel Vs Palestine!
 
kwani HITLER alivyoua Israel milioni 6 haikuwa ndio nyakati za mwisho?
 
Mwenye sikio na asikie
🙏🙏🙏
Mm sibishii Wala siungi mkono huu uzi; ninachosema hapa chini si ushabiki bali ina proof ya kihistoria na tukio lililotokea wakati wetu tunaishi.
Wote mnakumbuka Dunia ilivyozizima huku wakingojea kwa Wasiwasi ujio wa mwaka 2000!! Lakini kumbe hayo yalikuwa ni mawazo ya kibinadamu na wala si ya Mungu na Wala hakuwa time table yake. Ulimwengu ulisema ati miaka 2000 Tangu Yesu kuzaliwa. Hata hivyo Ulimwengu haujui kihalisi lini Yesu alizaliwa na pia Kumbe Mungu hakumtambulisha Yesu kuwa ndiye yule Messiah siku alipozaliwa!! Soma kitabu Cha Daniel 9:25 na kuendelea. Yesu alitambulishwa siku alipobatizwa. Je ni mwaka Gani huo? Biblia inatambulisha kuwa alibatizwa mwaka wa 15 wa MTAWALA wa Kiroma anayeitwa Tiberius. Sasa Historia inatuambia kuwa Tiberius alianza kuutawala mwaka wa 14. Hiyo inamaamisha Yesu alibatizwa mwaka 19.
Nimeisha andika uzi humu JF kuhusu umuhimu wa mwaka 2029, lakini inaonyesha watu haijawaingia akilini. Pia nikasema huenda ndyo maana huu muongo wa miaka ya 2020-2030 imegubikwa na matukio ambayo kila linapotukia linamuacha kila mtu kuduwaa kwakuwa haijawahi kutokea hivyo katika historia ya Karibuni
1. Coronavirus
2.Vita ya Ukraine
3. Tetemeko Uturuki, Morocco
4. Mafuriko China, Libya Pakistan
5. Moto wa Ajabu Hawaii
6. Na sasa Vita Israel vs Hamas
Hii vita, inaweza kabisa kuendelea kutushangaza kama ilivyotushangaza Ile ya Ukraine; na imeonyesha jinsi Ulimwengu ulivyogawanyika kutokana na tofauti ya dini ya kiislam na Kikiristo. Usishamgae vurugu ikatokea nchi za magharibi, India na China kutokana na migawanyiko hii.
Keep on the watch Dunia kwa sasa hivi inakwenda kwa Kasi sana
 
Unaweza nionyesha huo Uzi wako niusome.

Kingine Yesu alibatizwa na Yohana siyo huyo mtawala wa Kirumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…