Wakristo, waislam, walevi, maDJ na wezi muwe watulivu wakati NEMC wakifanya kazi yao halali

Hama kam
Nimefurahi sana kusikia NEMC wameanza kuwashughulikia wapiga kelele wanaosababisha zogo mtaani na kuwafanya raia wengine wakose raha na utulivu. Kipekee kabisa naomba NEMC wamulike zaidi makanisa, misikiti, vigodoro na wauza muziki (wezi wa kazi za wasanii) kwani hawa ndio wamekithiri kwenye uchafuzi wa hewa kwa kelele, hivyo kupelekea raia wasiishi kwa raha na amani katika maskani yao.

Hivi ninavyoandika uzi huu kuna nyumba moja ya ibada hapa karibu na nyumbani kwangu wamefungulia maspika yao wanatoa mawaidha kwa sauti ya juu hadi mtaa mzima umechafuka kwa kelele. Na maspika yako maanne na yamefungwa kuelekea upande zote nne za dunia. Na utaratibu huu sio wa siku moja tu bali ni wa kila siku. Inakuwa vigumu watu kusikilizana na wagonjwa kupumzika kwa amani kwa kuwa kelele ni kubwa sana.

Jirani na nyumbani kwangu kuna nyumba ya ibada ambamo kila siku lazima wawashe mispika wakati wa kuswalisha na mawaidha. Na pamoja na kuwa spika husaidia kukuza sauti lakini hata mswalishaji mwenyewe huongea kwa sauti hadi mishipa inakaribia kukatika.

Kuamsha watu asubuhi sasa ndio usiseme. Kiongozi wao huanza kuwaita wenzake na kuimba nyimbo kwa sauti kubwa tangu saa 9 alfajili hadi saa 11 swala inapoanza. Yaani tunakomaje hapa mtaani! Kuanzia saa 9 hadi saa 11 alfajili huwezi kulala hata ukiwa na usingizi mwingi kiasi gani. Ni KERO kubwa sana kwa kweli. Hivi kwanini kila muumini asiweke alarm kwenye saa au simu yake iwe inamuamsha badala ya kukera mtaa mzima kwa mikelele ya maspika? Ustaarabu uko wapi? Hapa ndipo nampendea Rais Kagame. Nchini kwake amepiga marufuku matumizi ya maspika.

Pamoja na kero ya kelele kutoka misikitini, pia kuna hizi kelele za maspika ya walokole na kengele za wakatoliki zinazopigwa kwa sauti ya juu hadi kukaribia kupasua ngoma za masikio ya raia. Utakuta muumini wa kilokole anaishi nyumba ya kupanga na kila wiki wenzake wanakuja kwake kukesha wakinena kwa lugha, kupiga vinanda na kuimba kwa sauti kiasi cha kuwa kero kwa wapangaji wengine. Kuabudu ni jambo zuri lakini isiwe kero kwa wenzako. Hata Mungu hapendi. Kuwakera wenzako kwa kelele za ibada kunaondoa baraka zote ambazo ungepata kutokana na kumuabudu Mungu wako.

Kelele nyingine za kuudhi hutoka kwenye mabaa, kwa kisingizio cha kuwaburudisha walevi. Pombe ikishakolea, usikivu wa mlevi hupungua, hivyo kuwalazimu maDJ kupiga muziki wa juu ili walevi wafurahi. Matokeo yake ni kuwakera raia wengine wasiolewa. Kero hii hupelekea wananchi na wafanyakazi kushindwa kulala usingizi mzuri, hivyo kupunguza utendaji kazi na kushusha uchumi wa taifa. Serikali isipokuwa makini kuzuia kelele hizi, uchumi wa nchi utashuka bila sababu za msingi.

Kero nyingine ya kelele hutoka kwa wauza CD, ambao wengi wao ni wezi wa kazi za wasanii. Ukipita kila mtaa, maeneo kama Kariakoo, kelele za wezi wa muziki zinakuwa kubwa kiasi cha kuondoa utulivu na kusababisha wafanyabiashara kushindwa kusikilizana na wateja wao. Kitendo hiki pia kinashusha uchumi wa nchi na kupunguza mapato ya serikali. Hapa uchumi wa nchi hushuka kwa namna mbili – namna ya kwanza ni kushusha mapato ya kodi na namna ya pili ni kupitia wizi wa sanaa za wanamuziki.

Kero ya mwisho kutokana na kelele, hasa maeneo ya uswahilini, ni vigogoro. Kuna mitaa ambayo kila wiki hukosi kusikia muziki wa kutisha kutoka kwenye maspika makubwa ya vigodoro. Unaambiwa kwamba hiyo ni never miss. Usiombe ukajenga au kupanga maeneo hayo. Hukawii kutelekeza nyumba yako uliyoijenga kwa mikono yako mwenyewe ukaenda kupanga mitaa ya mbali. Kelele za vigodoro ni kero zaidi hasa katika maeneo ya ukanda wa pwani na uswazi.

MAONI YANGU
Naunga mkono juhudi za NEMC kuwashughulikia wapiga kelele kwani kelele hizi, kama ilivyoainishwa hapo juu, zinasababisha ghasia kwa umma na kuvuruga uchumi wa taifa. Shime watanzania wote tushikane mikono kuhakikisha kwamba tunatoa ushirikiano wa kutosha kwa NEMC wakati wanapofanya juhudi za kuondoa kelele hizi kwenye mitaa yetu ili wananchi tuishi kwa amani na furaha.

Nawasilisha.
Hama kama huwezi kuendana na wenyeji hapo hami Kigamboni au mwituni ukapumzike. Bila hizo kelele za muziki na bar huo si mji ni nyumba za kulelea mapdri wastaafu.
When in Rome live like the Romans
 
Na vipaza sauti vya WAISLAM yaniii vikifunguliwa basi huwezi pata usingizi Tena. Navyo vizuiliwe kabisaa.
Hawa ndio KERO kubwa kuliko zote hapa nchini. Wanatuwashia maspika pembe zote za dunia utadhani kila mtu ni mwislamu. Kwanini wasiwahimize wafuasi wao wanunue saa na simu wawe wanaweka alarm zinawaamsha asubuhi na kuwambusha muda wa ibada unapowadia? Kama vipi basi wapunguze idada ya swala walau zibaki mbili kwa siku; swala tano zinatuchosha kwa kelele. Wanakera sana aisee!
 
Hama kam
Hama kama huwezi kuendana na wenyeji hapo hami Kigamboni au mwituni ukapumzike. Bila hizo kelele za muziki na bar huo si mji ni nyumba za kulelea mapdri wastaafu.
When in Rome live like the Romans
Kuna mahali ambapo unaweza kuhamia usiwakute waislamu na mispika yao mkuu? Labda niihame dunia.
 
Hawa jamaa yaani wanatusumbua sana na mikelele yao hapa mtaani. Serikali isipowachukulia hatua, wananchi tutajichukulia wenyewe sheria mkononi. Tumechoka.
Chomen moto hizo spika
 
Mtaani kwetu kuna shehe mmoja alikuwa anaanza kupiga kelele kuanzia saa 9 usiku! Hata waislamu wenzake walimkataa. Walimfukuza.
 
Nimefurahi sana kusikia NEMC wameanza kuwashughulikia wapiga kelele wanaosababisha zogo mtaani na kuwafanya raia wengine wakose raha na utulivu. Kipekee kabisa naomba NEMC wamulike zaidi makanisa, misikiti, vigodoro na wauza muziki (wezi wa kazi za wasanii) kwani hawa ndio wamekithiri kwenye uchafuzi wa hewa kwa kelele, hivyo kupelekea raia wasiishi kwa raha na amani katika maskani yao.

Hivi ninavyoandika uzi huu kuna nyumba moja ya ibada hapa karibu na nyumbani kwangu wamefungulia maspika yao wanatoa mawaidha kwa sauti ya juu hadi mtaa mzima umechafuka kwa kelele. Na maspika yako maanne na yamefungwa kuelekea upande zote nne za dunia. Na utaratibu huu sio wa siku moja tu bali ni wa kila siku. Inakuwa vigumu watu kusikilizana na wagonjwa kupumzika kwa amani kwa kuwa kelele ni kubwa sana.

Jirani na nyumbani kwangu kuna nyumba ya ibada ambamo kila siku lazima wawashe mispika wakati wa kuswalisha na mawaidha. Na pamoja na kuwa spika husaidia kukuza sauti lakini hata mswalishaji mwenyewe huongea kwa sauti hadi mishipa inakaribia kukatika.

Kuamsha watu asubuhi sasa ndio usiseme. Kiongozi wao huanza kuwaita wenzake na kuimba nyimbo kwa sauti kubwa tangu saa 9 alfajili hadi saa 11 swala inapoanza. Yaani tunakomaje hapa mtaani! Kuanzia saa 9 hadi saa 11 alfajili huwezi kulala hata ukiwa na usingizi mwingi kiasi gani. Ni KERO kubwa sana kwa kweli. Hivi kwanini kila muumini asiweke alarm kwenye saa au simu yake iwe inamuamsha badala ya kukera mtaa mzima kwa mikelele ya maspika? Ustaarabu uko wapi? Hapa ndipo nampendea Rais Kagame. Nchini kwake amepiga marufuku matumizi ya maspika.

Pamoja na kero ya kelele kutoka misikitini, pia kuna hizi kelele za maspika ya walokole na kengele za wakatoliki zinazopigwa kwa sauti ya juu hadi kukaribia kupasua ngoma za masikio ya raia. Utakuta muumini wa kilokole anaishi nyumba ya kupanga na kila wiki wenzake wanakuja kwake kukesha wakinena kwa lugha, kupiga vinanda na kuimba kwa sauti kiasi cha kuwa kero kwa wapangaji wengine. Kuabudu ni jambo zuri lakini isiwe kero kwa wenzako. Hata Mungu hapendi. Kuwakera wenzako kwa kelele za ibada kunaondoa baraka zote ambazo ungepata kutokana na kumuabudu Mungu wako.

Kelele nyingine za kuudhi hutoka kwenye mabaa, kwa kisingizio cha kuwaburudisha walevi. Pombe ikishakolea, usikivu wa mlevi hupungua, hivyo kuwalazimu maDJ kupiga muziki wa juu ili walevi wafurahi. Matokeo yake ni kuwakera raia wengine wasiolewa. Kero hii hupelekea wananchi na wafanyakazi kushindwa kulala usingizi mzuri, hivyo kupunguza utendaji kazi na kushusha uchumi wa taifa. Serikali isipokuwa makini kuzuia kelele hizi, uchumi wa nchi utashuka bila sababu za msingi.

Kero nyingine ya kelele hutoka kwa wauza CD, ambao wengi wao ni wezi wa kazi za wasanii. Ukipita kila mtaa, maeneo kama Kariakoo, kelele za wezi wa muziki zinakuwa kubwa kiasi cha kuondoa utulivu na kusababisha wafanyabiashara kushindwa kusikilizana na wateja wao. Kitendo hiki pia kinashusha uchumi wa nchi na kupunguza mapato ya serikali. Hapa uchumi wa nchi hushuka kwa namna mbili – namna ya kwanza ni kushusha mapato ya kodi na namna ya pili ni kupitia wizi wa sanaa za wanamuziki.

Kero ya mwisho kutokana na kelele, hasa maeneo ya uswahilini, ni vigogoro. Kuna mitaa ambayo kila wiki hukosi kusikia muziki wa kutisha kutoka kwenye maspika makubwa ya vigodoro. Unaambiwa kwamba hiyo ni never miss. Usiombe ukajenga au kupanga maeneo hayo. Hukawii kutelekeza nyumba yako uliyoijenga kwa mikono yako mwenyewe ukaenda kupanga mitaa ya mbali. Kelele za vigodoro ni kero zaidi hasa katika maeneo ya ukanda wa pwani na uswazi.

MAONI YANGU
Naunga mkono juhudi za NEMC kuwashughulikia wapiga kelele kwani kelele hizi, kama ilivyoainishwa hapo juu, zinasababisha ghasia kwa umma na kuvuruga uchumi wa taifa. Shime watanzania wote tushikane mikono kuhakikisha kwamba tunatoa ushirikiano wa kutosha kwa NEMC wakati wanapofanya juhudi za kuondoa kelele hizi kwenye mitaa yetu ili wananchi tuishi kwa amani na furaha.

Nawasilisha.
Pia soma:
Asante KKKT kwa kuonesha njia. Bado hii misikiti ya BAKWATA
 
Back
Top Bottom