Wakristo wanatoa sana kwa wachungaji kuzidi kwa wahitaji, Waislamu wanatoa sana kwa wahitaji kuzidi kwa mashehe

Wakristo wanatoa sana kwa wachungaji kuzidi kwa wahitaji, Waislamu wanatoa sana kwa wahitaji kuzidi kwa mashehe

Naomba nitoe elimu kidogo: Kuna wakristo wasio wakristo, hawa hawaujui ukristo kwa maana ya kwamba hawana uhusiano binafsi na KRISTO. Wakristo wasio wakristo wanapotoa sadaka wanaamini wanampa/wanamfadhili mchungaji!! Wakristo walio WAKRISTO (waliookoka) wanapotoa sadaka wanajua wanamtolea Mungu na ndivyo ilivyo!! Wakristo wasio wakristo wamezaliwa na wazazi wakriso ambao pia wanaweza kuwa ni wakristo wasio wakristo pia!! Mkristo wa kweli ni yule aliyeokoka.
umeokoka vipi
tupe andiko
mi nasema hakuna mtu aliye okoka
 
Kwani hizo hospital na shule ni bure? Kibaya zaidi hizo shule zina ada kubwa kuliko shule nyingi za binafsi. Wanachofanya wakristo ni ubepari.

Fanyeni kazini Acheni kulalamika cha bure unakipata kwa Mungu peke yake tu
 
Makanisani wakristo wengi wakishatoa sadaka kanisani ndio shughuli imeishia hapo. Ni rahisi sana kuwakuta wachungaji mabilionea wanaotajirika kwa sadaka za waumini lakini kuna waumini wana changamoto zinazoweza kutatulika kwa milioni 10 ila wanaombewa badala ya kusaidiwa, ni kweli makanisa yanajenga shule mpaka huko vijijini ila sihesabii kama msaada maana ni miradi ya kifaida, shule za kiristo ni kawaida sana kukuta ada ni milioni 3, vyuo navyo vipo vingi ni gharama kuzidi vya serikali.

Licha ya kwamba waislamu wengi ni maskini ukilinganisha na wakristo, Nimegundua waislamu hawatoi sana sadaka misikitini lakini huwa wanasaidia sana huku nje.

Nimewahi kupata shida ya maji na niliweza kuchota maji bure kabisa msikitini wiki nzima, kanisa waweza kukuta lina mabomba ya kutosha ila ni kwajili ya matumizi ya kikanisa tu.

Niliwahi kufikia sehemu sina pa kulala nilienda kanisani nikiwa muumini wa kanisa tangu mtoto lakini nilikataliwa kabisa, sehemu iliyonitunza ni msikiti,

Mwezi wa Ramadhani ule mwezi mzima ni kawaida sana kuwakuta waislam wanasaidia vyakula watu wenye shida.


Pamoja na mazuri haya kilichonitatiza kuhamia uislam ni dini ambayo ina baadhi ya sheria zenye mirengo mikali sana, hakuna free will uhuru wa kiimani kwamba unaweza kuchagua dini nyingine, kukariri koran na kuomba kwa lugha usiyoijua, mistari yenye kuchochoea chuki dhidi ya wasio waislam, n.k.
Hao wanaotumia mkate na kugawa silesi Moja Moja kwa waombaji siku ya ijumaa? Wenzako wanajenga shule na hospitali ili kulenga mahitaji halisi ya jamii. Kuna madhirika kama carnitas yanatoa msaada halisi kwa maskini
 
well
 

Attachments

  • %E8%B6%85%E7%BA%A7%E6%88%AA%E5%B1%8F_20240202_160719.jpg
    %E8%B6%85%E7%BA%A7%E6%88%AA%E5%B1%8F_20240202_160719.jpg
    42.9 KB · Views: 5
Hii imeenda, hata hospitali wodi za wazazi wamama wa kiislam wanapita kugawa maziwa na uji kwa wakina mama waliojifungua

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Ni kheri kumsaidia mtu mwenye uhitaji kuliko kwenda kutoa sadaka yako sijui kwa mchungaji,kwanza ni ujinga sana,mtoa mada uko sahihi kabisa nakuunga mkono mimi niko kwenye haya makanisa nayaona mengi sana
 
Ni kheri kumsaidia mtu mwenye uhitaji kuliko kwenda kutoa sadaka yako sijui kwa mchungaji,kwanza ni ujinga sana,mtoa mada uko sahihi kabisa nakuunga mkono mimi niko kwenye haya makanisa nayaona mengi sana
Mkuu ikiwa wewe ni Mkristo kweli nafikiri kuna kitu hukijui.

Biblia imetoa mqongozo wa sadaka.

Kumpa mchuñgaji pesa ni hiari ma sio lazima.

1. Kuna sqdaka ya hiari, hii kila mtu hutoa jinsi moyo wake wapenda kutoa

2. Kuna sadaka inaitwa ZAKA.. hii ni 10% ya mapato yako, mwanzilishi ni Ibrahim alimtolea kuhani mkuu aitwaye Melkizedeki, ikaelezewa Kitabu cha Malaki 3:7

3. Kuna sadaka ya limbuko ya mazqo na wanyama, hii kabla hujaanza kivuna unatoa mazao ya kwanza, haina kiwango ni moyo wako.

4. Pia kwenda kuwasaidia Wajane, Yatima na wagonjwa.

Hapa sio kutoa pesa au vitu tu hata kutoa muda kwenda kuwatembelea ni sadaka.

Hii imewlezwa vyema na Yakobo, tena akasema dini iliyonjema ni kwenda kuwaona Wajane na yatima.

Note: Hii ya kumtolea mchungaji sadaka ipo kwa makanisa ya mfukoni zaidi, kila wiki wanabuni ufunuo mpya wa kuvuna pesa.

Nami nasema acha watu wavunwe tu kwa ujinga wao
 
Kuokoka na nini
Kuokoka toka dhambini. Hivyo kuepushwa na hukumu ya Mungu dhidi ya wenye dhambi ambapo watatupwa katika jehanamu ya moto. Huko watateseka milele maana na hiyo ndiyo huitwa mauti ya pili. Ukiokoka unazaliwa mara ya pili na hivyo kuwa na nguvu ya kukataa dhambi.
 
umeokoka vipi
tupe andiko
mi nasema hakuna mtu aliye okoka
Warumi 10:9-12. "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. ............."

Zab 16:3​

Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Hiyo hapo juu ni kanuni ya wokovu. Yeyote akiifanyia kazi kwa moyo wake wote anaokoka
 
Umeyatoa wapi hayo maneno?
Warumi 10:9-10. Hapo kuna kanuni ya kuokoka! Ukristo wa mtu unaanzia kwa mtu kumkubali Yesu awe Bwana na Mwokozi wake kwa kufuata m.,aelekezo kwenye mistari hiyo, hauanzii kwa kuzaliwa na wakristo.
 
Kuokoka toka dhambini.
Umewahi soma baibo?
Matayo 19:25.

25 Wanafunzi wake waliposikia haya walishangaa sana, wakamwuliza, “Ni nani basi anaweza kuokoka?”

🙄🙄🙄
Matayo 19: 26 .
Lakini Yesu akawatazama akawaambia, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani,
 
Back
Top Bottom