Wakristo wengi huhofia mali kugawanywa pasu kwa pasu ndio maana hawaachani hata wakifumania wake zao

Wakristo wengi huhofia mali kugawanywa pasu kwa pasu ndio maana hawaachani hata wakifumania wake zao

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kwa waislam wengi mambo ya kuvunja ndoa yanamalizwa kimya kimya bila hata mahakama kuhusika, wapo wanawake wanaoenda mahakamani kudai haki za mali lakini ni wachache.

Kwenye ukristo shughuli ipo tofauti, ndoa hadi inavunjika hapo ni kwamba mahakama imehusika na imeshatoa hati ya ndoa kuvunjika, baada ya hapa kinachobaki huwa ni zoezi la mali kugawanywa ..hata kama ulimfumania mkeo analiwa, ndoa ikivunjwa lazima mgawane mali.

Yani hapa wanasheria wakishajua ndoa yenu imevunjika wanamuona mke wako ni mgodi, watamsaka wamsaidie kwa namna yoyote ili mali wapewe mgao wao wa uhakika.

Sheria ni kwamba mali za kugawana ni zile ambazo zilianza kuwepo baada ya ndoa lakini kiuhalisia huko mahakamani kama huna connection nzito jihesabie tu kwamba pasu kwa pasu, tena haraka tu.

Hapa si ajabu kusikia mtu kaua mke wake ili ayamalize hayo maumivu, ndio hizi kesi tunaona mtu alieua na jinsi alivyo tunapata mshangao, unakuta mwanaume mstaarabu kaua mke wake yani tukio alilofanya na jinsi alivyo haviendani kabisa.
 
Ni heri kwa waislam mtu anaweza kuvunja ndoa kimyya kimya na wakamalizana kimya kimya.

Kwenye ukristo shughuli ipo tofauti, ndoa ikivunjika basi na mahakama imehusika hapo, kile kitendo tu cha kutoa hati ya ndoa kuvunjika ni tiketi ya mali kugawanywa.

Wengi huihia kugawana mali pasu kwa pasu maana hawana elimu ya sheria na wale mahakimu nao huwa wanalazimisha hii pasu kwa pasu ili mgao wao uongezeke, ila hata ukiwa unazijua sheria bado kuna mgao na hili ndilo huumiza wengi.
Biblia imesema Mungu anachukia kuachana Kwa hyo ni maandiko si bla bla unazoleta hapa hakuna kuachana hata iweje Kwa mkristo...
 
Kwa waislam wengi mambo ya kuvunja ndoa yanamalizwa kimya kimya, wanawake wanaoenda mahakamani kudai haki za mali wapo lakini huwa ni wachache

Kwenye ukristo shughuli ipo tofauti, ndoa hadi inavunjika hapo ni kwamba mahakama imehusika na imeshatoa hati ya ndoa kuvunjika, baada ya hapa kinachobaki huwa ni zoezi la mali kugawanywa.

Yani hapa wanasheria wakishajua ndoa yenu imevunjika watamsaka mwanamke wamsaidie kwa namna yoyote ile mali zigawaywe nao wapewe chao,

Wengi huishia kugawana mali pasu kwa pasu maana hawana elimu ya sheria, yani kule mahakamani kumshinda mwanamke ni ngumu sana maana anaonekana ni mnyonge na sheria zinampendelea sana kiasi kwamba hata kama alikuwa hajishughulishi basi anapewa asimilia 30 za mali.

Hapa si ajabu kusikia mtu kaua mke wake ili ayamalize hayo maumivu, ndio hizi kesi tunaona mtu alieua na jinsi alivyo tunapata mshangao, unakuta mwanaume mstaarabu kaua mke wake yani tukio alilofanya na jinsi alivyo haviendani kabisa.
Tatizo ni dini ya watu yani inafuata matamanio ya watu lkn sio Muumba kasema nini
 
Sio kweli.. mali huwa inagawanyishwa kwa ushahidi wa mchango wako.

Mke awe wa kikristo ama awe wa kiislamu sheria ya ndoa kwenye kugawanya mali ni moja
Watanzania wengi wamekaririshwa mali zinagawanywa pasu kwa pasu.

Wanaingia mahakamani wanaonekana hawajui kitu, wale jamaa wanaomtetea mke nao wana gawio lao inabidi wafosi kingi iwe pasu kwa pasu.

Kwa wale walioelimika ndio huwa wanaweza kujitetea kwamba mali zinazogawanywa ni zile ambazo zipo baada ya ndoa zisizohusisha urithi ama zawadi,
 
Biblia imesema Mungu anachukia kuachana Kwa hyo ni maandiko si bla bla unazoleta hapa hakuna kuachana hata iweje Kwa mkristo...
Mh,

Mathayo 19:9"Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, anazini"
 
Kwa wale walioelimika ndio huwa wanaweza kujitetea kwamba mali zinazogawanywa ni zile ambazo zipo baada ya ndoa zisizohusisha urithi ama zawadi,
Labda kama kulikuwa na makubaliano kabla ya ndoa (prenuptial agreement)
 
Labda kama kulikuwa na makubaliano kabla ya ndoa (prenuptual agreement)
Sheria ipo wazi kwamba mali za kugawana ni zile baada ya ndoa lakini huko mahakamani kama huna coonection hesabia tu kwamba ni pasu kwa pasu
 
Kwenye ndoa waislam wapo vizuri Sana. Shida wana ubinafsi sana, wabaguzi hawataki bint zao waolewe..

Huku kwa wakristo mambo ya ndoa Ni kifungoni.

et hadi kifo kiwatenganishe hapo mwanamke akilwa nje atajua anaenda kwa kushauriwa na viongozi badae mambo yanakaa sawa..happy lazima mauaji yatokee.

Hakuna mwanamke mwenye dharau na kiburi Kama msaliti.
 
Kuna mambo yakotokea mfano umemfumania mwanamke,mwanamke kakutoroka,kazaa njee ya ndoa
Mwanamke hapati Mali

Ova
 
Kwenye ndoa waislam wapo vizuri Sana. Shida wana ubinafsi sana, wabaguzi hawataki bint zao waolewe..

Huku kwa wakristo mambo ya ndoa Ni kifungoni.

et hadi kifo kiwatenganishe hapo mwanamke akilwa nje atajua anaenda kwa kushauriwa na viongozi badae mambo yanakaa sawa..happy lazima mauaji yatokee.

Hakuna mwanamke mwenye dharau na kiburi Kama msaliti.
Kwamba waislamu hawataki watoto wao waolewe ? Ebu fafanua vizuri hii kauli yako
 
Biblia imesema Mungu anachukia kuachana Kwa hyo ni maandiko si bla bla unazoleta hapa hakuna kuachana hata iweje Kwa mkristo...
Mathayo 5:32
Lakini ninawaambia kuwa, kila atakayemtaliki mkewe kutokana na sababu isiyohusiana na uzinzi, anamfanya mke wake kuwa mzinzi. Na kila atakayemwoa mwanamke aliyetalikiwa, atakuwa anazini.

HUWA MNAPATA NINI KUYASINGIZIA MAANDIKO?.
 
Mh,

Mathayo 19:9"Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, anazini"
Mtu anakurupuka na KUYASINGIZIA maandiko!Ni watu wa kuonea huruma tu.
 
Hayo makanisa yanayoruhusu ndoa za jinisia moja ndiyo yanafuata qoran? Hebu kuwa na heshima kijana
sasa umeshaambiwa hakuna kitu kama hicho ktk bible umekomaa.bible ni ile ile shida ni akili mbovu kama za hao wanaof1rana hata huko uarabuni au zenj.
 
Back
Top Bottom