Ndoa ni suala la dini, wala sio mila kama watu wanavosema kwasbb ndoa hufungwa kanisani au msikitini, na hufungwa kwa sheria za dini (kwa waislam), upande wa wakristo sijui ila kwa vile inafungwa kanisani basi naamini hufungw kwa sheria z kikristo pia.
Linapokuja suala la kuvunja hii ndoa, inabidi ivunjwe kidini kama ambavyo ilifungwa.
Kwa waislam kuna process zake kama vikao vya wazazi pande zote mbili, talaka moja, talaka ya pili na ikishindikana kabosa, viongoz wa dini watashirikishwa(kumbuk ilofungw kidini) na wakishindwa kusuluhisha basi TALAKA INAPITA.(kuachana mazima)
Hata baada ya kuachana, sheria bado inaendelea kuongelea majukumu ya kila mmoja juu ya watoto waliopatikana na haki za mwanamke, mfano, m'ke ataondoka na mahari yake. Watoto kama ni chini ya balegh bas watakua chin ya uangaliz wa mama yao na baba yao atahusika 100% kuwahudumia, na watakapofika balegh kiakili bas watakua chini ya uangalizi wa baba mpk pale watakapotoka mikonon mwake kama ni m'ke, bas mpk pale atakapoolewa, hapo nd anatoka chin ya uangalizi wake.
Kama ndoa ni suala la dini basi kila kitu inabidi kimalizwe kidini, unless kama haikufungwa kwa misingi ya dini.
Kuishirikisha mahakama katika suala la kidini ni udhaifu (staki kusema udhaifu wa nini).