Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,710
- 2,587
Jana nimeona Mechi ya Azam na Ruvu, kiukweli pasi na shaka Azam na wao wameshakata shauri liwalo na liwe kama wakubwa wengine, kwa udi na uvumba na wao wanataka matokeo sasa. Najua kama ilivyo desturi mtataka ushahidi lakini angalieni hizi mechi zinavyochezeshwa yaani mpaka Refa anayo matokeo mfukoni.
Juzi alicheza Simba, Refa alikuwa mpaka na yeye anashirikiana kushambulia Ihefu, mpaka akatoa tuta ambalo mwenyewe alijishtukia na kulifuta. Yanga wao tayari wameshapata goli Mwanza, la Refa kufunika. Vijana kweli wameshika hatamu lakini lazima tutazame tena.
Tunao TAKUKURU lakini wakiingia kuchunguza hili, mimi nimekaa pale mniite mbwa! Majibu ya kugushi ndiyo huko tunapoenda kushindana kweli tunaanza tena kuweka figisu. Wacheza kamari, wauza madawa ndiyo wanashikilia soka letu na wameweka mikono yao michafu, sasa mpaka tuliyokuwa tunawaona wasafi na wao wanaanza kuchafuka.
Tunajua wenye mamlaka ya soka walivyowabishi na kuna mengi ya dhahiri hawayataki kuyakubali, waamuzi mpaka mmewavilisha 'gadgets' basi wasaidieni kuondosha hizi aibu manake kuna mengine wanafanya wao aibu tunaona sie huku.