pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 18,406
- 14,643
Kwa viapo vyao kwa Mola na matendo yao maovu laana itaambatana nao na uzao wao, asema Bwana wa majeshi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio wanaanza kuvunja viapo? Mzee Kibao ameuawa na wanasikia majina ya wahusika yanatajwa, vijana kina Soka wametekwa..waliohusika wanatajwa, wao wako kimya..kuna mengine yapi mabaya zaidi ya haya na wameshindwa kuchukua hatua, wakati familia zinalia???Umezuka mchezo nchini wa watawala kutoheshimu haki za raia, kutoheshimu viapo vyao. Na hii yote ni kwa sababu ya Kibri cha madaraka. Kibri cha kujiona "wakubwa" na kwamba ni untouchable.
Kwa kiburi hicho, hawa wenye dhamana huvunja viapo vyao walivyoapa kwa kushika Qur'an na Biblia halafu wakamalizia maneo ya "Ee Mwenyezi Mungu nisaidie"
Mafundisho ya Mwenyezi Mungu ni kutaka wale wenye mamlaka miongoni mwa watu wawe waadilifu. Ila nchini mwetu hilo jambo la uadilifu sasa limegeuka historia. Wanadhulumu chaguzi za wananchi kwa hila, na kibri kikubwa mno.
Sasa mimi niwakumbushe tu, Mungu amesema katiks vitabu wanavyoapa navyo kuwa "Hawapendi Madhalimu".
Nawakumbusha pamoja na kuikumbusha nafsi yangu kuwa ADHABU YA MWENYEZI MUNGU NI KALI, KIBOKO CHAKE NI KIKALI. Pale wanapokuwa wanajidhani wamemaliza kila kitu na ni invincible ndipo Fimbo ya Mungu inaporindima.
Kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu halafu ukavunja kiapo kwa ushabiki tu, uroho wa madaraka na kibri ni kujitafutia matatizo makubwa sana.
Wapeni Watanzania haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka, nsifanye dhulma!
Mkikaidi Shauri yenu, Umri wa mwanadamu ni mfupi, mtakuja kuwa accountable kwa dhulma ya kuvunja viapo vyenu mbele ya Mola
C.C. Samia
C.C Mchengerwa
C.C Majaliwa