Wakulima wa mbaazi wilayani Kiteto wanalalamikia Viongozi wa Wilaya kuwa Madalali na kuwasababishia hasara

Wakulima wa mbaazi wilayani Kiteto wanalalamikia Viongozi wa Wilaya kuwa Madalali na kuwasababishia hasara

Joined
Sep 14, 2023
Posts
82
Reaction score
74
Wakulima wa mbaazi wa hapa mjini Kibaya wanalalamikia kuwa viongozi wa Wilaya wameshindwa kulinda maslahi ya wakulima wa mbaazi Wilayani Kiteto na wao kugeuka ndio madalali wa zao hilo.

Wakulima wamepima mbaazi zao toka wiki Moja iliyopita na bado hela hawajalipwa.

Kibaya zaidi wao mbaazi yao imepakiwa kupelekwa kuuzwa kwenye Soko la Dar es Salaam wao wakijua kuwa huo ni mnada kumbe watu wameamua kuingia kuwa madalali, na hili limeleta mgongano wa kimaslahi.

Watu wanatumia nguvu na walazimisha wakulima kupeleka mbaazi ghalani. Bei ambayo wao wamechukulia hizo mbaazi kwa wakulima ni Tsh. 2100/ hadi 2150/ kwa kg na wao wanauza soko la Dar es Salaam Kwa Tsh. 2400/ na zaidi, je mnufaika ni nani hapo?

Mkulima unakutana anakosa Tsh. 100/ Kwa kg ukizidisha mara ujazo wa Gunia ambalo ni kg 120 100=12000/- mara Tani 100 ambazo ni kg 10000?

Hapo mkulima anasafiwa au anakandamizwa?
 
Kuna CCM watakuja kukwambia mama kafungua soko nje.

Dawa CCM kuondoka tushachoka CCM movie [emoji897]
 
Katika Hali ya kushangaza wakulima wa Zao la Mbazi. Waliopeleka na kuchukuliwa mbazi zao Kwa Nguvu na Viongozi wilayani Kiteto Mbazi zao zimepelekwa kuuzwa kwenye Soko la Dar es salaam , MBAZU hizo zilisafirishwa na magari karibu matatu na kukabidhiwa kundi la Madalali wa Kiteto huku nao wakizipeleka Kwa Madalali wa Dar es salaam, hao wakulima wa Mbazi wakati wanasubiri MNADA kumbe mbazi zimeshasafirishwa muda mrefu na wao kuambulia Bei ya ahadi baada ya kulalamika wengine wakiambuwa Bei 2050 sababu mbazi Zina ukijani, wengine wakipewa 2080,2100, 2130. Huku wao wameuza Kwa Bei kati ya 2390 Hadi 2450/ hapo wakulima wanashanga huu udalali wa Viongozi wa Wilaya kusafirisha Mbazi kupeleka soko la Dar es salaam umeanza lini? Nani wapi walikubaliana na wakulima kuwa Mbazi za itaoelekwa Dar es salaam Kwa Madalali wa Dar?
jee. Muongozo wa Minada ya serikali inasemaje na utaratibu wake upojee?
jee tukisema wakulima wa Mbazi Kiteto wamepigwa Kwa Kutumia. Kivuli Cha Uongozi na mamlaka ya viongozi wa Wilaya Kwa kupelekwa polisi na kutishiwa na kuwekwa ndani itakuwa ni sahihi?
jee mkuu wa Wilaya anaweza kujitoa kwenye Hii kashifaa?
 
Back
Top Bottom