Wakulima wa nyanda za juu kusini wanasema Mama ametufikia na kutujaza matumaini, wanauliza nani hajafikiwa na mama?

Wakulima wa nyanda za juu kusini wanasema Mama ametufikia na kutujaza matumaini, wanauliza nani hajafikiwa na mama?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu huo ndio msemo mpya ulioibuka huku mtaani kwa kundi kubwa la wakulima ambao kwao kilimo ndio pumzi yao, wanasema hakika Mh. Rais Samia amewafikia kwa wakati na kuwajaza matumaini katika mioyo yao.

Hii imetokana na kuwasili kwa wakati kwa mbolea za ruzuku zinazouzwa kwa bei elekezi ya serikali yao, hii ni baada ya wiki chache kupita tangia tulipojiandikisha taarifa zetu katika mitaa na vitongoji vyetu na kupewa namba za siri tunazokwenda kuchukulia mbolea.

Hata maeneo ya vijijini sana ambako mawakala waliokuwa hawajafika kwa ajiri ya kukamilisha taratibu za uchukuaji wa alama za vidole tayari wameshawasili na kufanya zoezi hilo, ili watu waneemeke na juhudi hizi za Mh. Rais Samia kuwajari na kuwatazama kwa jicho la huruma wakulima.

Ndugu zangu hakika Mama Samia amewagusa sana wakulima na pongezi kubwa sana zinaendelea kutolewa kwa Mh. Rais. Ikumbukwe kuwa kundi kubwa sana la watanzania limejiajiri katika secta hii ya kilimo ambayo Mh. Rais ameibeba mikononi mwake kusaidia wakulima.

Ngugu zangu kinachokwenda kutokea ni mapinduzi ya kilimo na uchumi wa wakulima, sasa wakulima wanakwenda kuongeza uzalishaji na hivyo kukuza kipato katika familia zao, kwa kuwa pia kwa sasa bei ya mazao imekuwa nzuri sana tangia wakati wa mavuno.

Awali mkulima alikuwa anahenyeka juani na katika mvua kwa kuvuja jasho jingi, lakini jasho hilo lilikuwa linaliwa na waliokaa kimvulini, kwani bei ilikuwa chini sana wakati wa mavuno na kupelekea mkulima kuuza kwa bei ya hasara bila kujari gharama alizotumia na kuendelea kuelea katika kisima cha umasikini mwaka ahdi mwaka. Lakini sasa mkulima anafaidika na jasho lake kwa kuwa soko kwa sasa ni la uhakika na pembejeo sasa ni uhakika.

Hapa Mh. Rais amezifuta jasho kaya na familia na kundi kubwa lililo katika secta hii iliyo uti wetu wa mgongo. Usalama wa nchi ni chakula, chakula kinakwenda kuwepo cha kutosha na mkulima anakwenda kunufaika. Hakika Mama Samia ni kiongozi wakipekee sana katika mikakati yake ya kiuongozi katika kugusa maisha ya wananchi wake, uongozi wa Mh. Rais ni wakuacha alama njema, Rais Samia ni zawadi kwetu watanzania.

Wakulima wanasema Mama ametufikia tulipo. Wanauliza nani hajafikiwa na kuguswa na utumishi uliotukuka wa Mh. Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassani?
 
Back
Top Bottom