Jumapili, Februari 9, 2025
WAKULIMA WAPEWA UJUZI KUINGIA MASOKO YA NJE
View: https://m.youtube.com/watch?v=g4lX5ji0qBQ
Ukosefu wa maarifa na ujuzi miongoni mwa Watanzania, hususan wale walioko katika mnyororo wa kilimo, umetajwa kuwa sababu kuu inayowakwamisha kufikia masoko ya kimataifa.
Hayo yameelezwa leo Jumapili, Februari 9, 2025, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Timoth Mmbaga, wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa kilimo nchini, iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Italia.“
Watanzania wengi tunakabiliwa na changamoto ya kushindwa kuuza bidhaa zetu nje ya nchi kwa sababu ya ukosefu wa maarifa, ujuzi na taarifa sahihi za namna ya kuingia katika masoko hayo.
Ndiyo maana tumeandaa mafunzo haya kwa kushirikiana na Ubalozi wa Italia ili kuwasaidia wakulima wetu, hususan katika matumizi ya teknolojia,” amesema Mmbaga.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni ya awali na yataendelea kutolewa katika mikoa mingine ili kuwajengea uwezo wakulima na wadau wa kilimo, kwa lengo la kuboresha uzalishaji na kufanikisha upatikanaji wa masoko ya kimataifa.
source: mwananchi digital