Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

ukichokozana na mwenzako unamwambia tutapigana saakumi
nakulikuwa na sehemu ya kupigania

Mkuu umenikumbusha habari ya kupigana, kuna jamaa yetu alidundwa siku 1 akabaki anatambia mkwe Wa nyumbani kwao (Dada yao alikuwa ameolewa kama ana wiki 1 hivi). Eti nitaenda nikaliambie li-mkwe la nyumbani kwetu! Msingi miaka hiyo ilikuwa raha sana!! Jamaa yalikuwa yakiamua kupiga mkono ilikuwa hatari sana na ukizingatia kulikuwa na mibaba imeacha wake nyumbani, zilikuwa zinapigwa ngumi za kiutu uzima!
 
Mi nakumbuka kipindi kile simu za mkononi zilikua hamna tuliteuliwa vijana wawili wakakamavu kupeleka barua shule ya jirani iliyopo kilometa 5
 
mi nakumbuka uketo, yaan ikua lazima kila siku nikaange mahindi na kuyaloweka kama msosi saa nne.
 
pia nakumbuka tulivyotandikwa mifimbo darasa la saba wote tulipofeli mitihan ya kata yaan kila mwalimu lazima fimbo moja moja yan sitosahau.
 
Dah nimecheka sana. Mnakumbuka mambo ya kupinga? Siku nzima mkono makalioni ukitoa Tu Boonge la buti linakuhusu... Basi kutwa nzima unashikilia kalio kama unazuia mavi...
 
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???

Mkuu hivi mwaka 1986 rais wa Tanzania alikuwa ni nyerere .acha fix mkuu
 
mi nakumbuka uketo, yaan ikua lazima kila siku nikaange mahindi na kuyaloweka kama msosi saa nne.
Kulikuwa kuna kitu inaitwa bong'oa,ukiinama tu mzee teke la adabu litakuhusu then kulikuwa na kupinga kuhusu vitu vya kula kula ukishika vibaya tu wamepokonya na unaachiwa masikitiko tu
 
Minakumbuka ishu kubwa ilikuwa ni kuimba table mwalimu wahesabu akifika niushuzi tuu. Na English kutamka the ilikuwa ni ze kwakwenda mbele stick sake usiombe binafsi matako yalikuwa yasha palalaiz kwa viboko at a upige 50 kwangu ilikuwa kazi bure.na kale kawimbo "watolo wapite mbelembele"ujue hapo nimkong'oto Wa adabu.
 
Salama:ccm inaamini kwamba binadamu wote ni sawa shikamoo mwalimu.sitasahau
 
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
Aisee mimi mchezo ulinitawala sana kufua nguo ilikua ni JUmapuli SAA moja usiku nakausha navpasi
 
Nakumbuka kukalishwa benchi moja na mtoto wa kike afu nahama nilikua naona ujinga ila saivi nikiona picha za huyo binti naumia mno roho, kumbe mwalimu wangu alikua na nia njema

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mm kuanzia darasa la tano hadi la saba nilikuwa napangiwa mwanafunzi wa kike, hafu mwalimu alikumshenzi anampanga ambaye uwezo wake darsani upo chini ili nimsaidie, ila yule binti hakufaulu ingawa aliolewa hadi Leo anakijana wake yupo Chuo kikuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom