Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Enzi zile duh........raha,

Kwenye mchakamchaka ni saa kumi usiku...... kuwahi namba, Hakuna kupiga kelele darasani, mambo ya table (hesabu za kuzidisha za kushtukizwa na teacher)....kumi na mbili mara sitaaaaaa mwl anakulamba fimbo mpaka utoe jibu.

Gwaride kwa filimbi:

Baba paka aliyesema.....
sisi hapa, ni watoto wadogo, twajifunza siasi ya ujamaaa, mwalimu wetu katfundisha adabu na heshima mbele ya wazaia wetu!.......
Oh, vijana, vijaaaana, vijana,vijana tayari, ..kulitumikia, taifa, taifa Tanzania, oh Walimu.......
Nyerere yupo ukiona kundi la siasa, Nyerere yupo,...Kawawa yupo......nk
Sisi tunataka kuwasha mwenge, tunataka kuwasha mwenge,
Naapana naahidi mbele ya chama,
Naipenda sana shule yetu
shule yetu imejengwa kilimani
Azimio la Iringa, lasema siasa ni kilimo, wananchi tushike majembe tukalime, tupate mazao bora.
Tumeuona mpilipili na maua yake ......
Ahaa, chama cahetu cha mapinduzi cha jenga nchi, Nyerere ahaaaa, Karume cha jenga nchi...

Nyimbo za mchakamcha, darasani na kuhamasishana

Iddi Amiri akifa, mimi siwezi kulia,ntamtupa kagera awe chakula cha mamba.
Mwenge huo mwenge.....mbio mbio
twende tukawinde leeeeo, tukawindeee vipepeo
Hasiependa shule ni mjinga kabisa
Kikojozi na nguo twaichoma moto!
Baba yake Juma ametia vilaka matakoni mwake vinauluzana umekuja lini....

Kwaya:

Karibu sana shuleni kwetu mtukufu Mkuu wetu wa Mkoa,

Ngonjera:

Hodi hodi uwanjani,

Vitabu:

Juma na Roza
Kalumekenge
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
siku ya gulio Katelelo
Kibanga ampiga Mkoloni
Brown ashika tama
Safari yenye mkosi
Nondo mla watu

Maarifa

Barua za mapenzi zinachorwa Mkuki na moyo, unaanza na "Kwako Dada Mpendwa..."
Barua za mapenzi zinafichwa kwenye mikebe
Barua za mapenzi zikipatikana zinasomwa mstarini.
kumbebea mwalimu maembe
kumpelekea mwalimu misigo yake kwa demu
Kuchunguliwa wanafunzi wa kike wakiwa ****** au kwa vioo

Kazi za nje

Kumwagilia Busatan za shule
Kufyatua tofari
Kuja na nyasi shuleni
kuleta maji kumwagia viunga vya shule kuondoa vumbi
kulima mashamba ya Mwalimu, DRDD, Mkuu wa Wilaya nk.

Kutoka shule

sasa, sasa saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheri tutaonana keshoooooo!

duh mkuu nimekukubsali kweli wewe wa enzi zile hivi siku hizi kuna nyimbo za shule kweli
 
Duh miaka ya 80 -90 kaka, mimi nilikuwa time keeper, sasa rafiki zangu walikuwa wananiambia nigonge kengere kabla ya muda ili tuwahi kucheza mpira - mpira wa makaratasi.

Darasa la tano namkumbuka mwalimu mmoja wa sayansi, akija darasani lazima aje na fimbo kama 10 hivi, anaanza kukumbushia somo la mwisho, anayeshindwa anapita mbele... anangoja super six....aisee kweli shule ilikuwa chungu kipindi chake kikifika.

Kuwahi number saa moja pia ilikuwa tatizo kwangu, ukicheliwa tu unakuta inakuwa imekula kwako.....moja...mbili.....tatu....nne etc

Mkaguo wa mwili ilikuwa soo, Kwa wale wamesoma vijijini ilikuwa hatari kukutwa na chawa, nguo hujafua, magaga ya miguu etc. Mimi nilikuwa ktk bendi ya shule nakumbuka wimbo wa mkaguo ulikuwa unaitwa kwa filimbi na bendi .... as Baba pakaa akasemaa twendeni tukawinde.....

Mwalimu Mkuu alikuwa mzee anaitwa Bebenya.... sasa lazima muimbe kumsifika kila siku asubuhi na jioni kabla hamjaenda nyumbani - tuliimba twampenda bembenya twampenda bembenya twampenda bebenyaaa eeeee aiyelele twampenda bebenyaaaa - tukae kwa amani tukae kwa amani tukae kwa amani eeee.....

Haraiki ya zile nyimbo za utaifa tumeziimba sana, hawa walimu waliokuwa wametoka JKT wakati huo walikuja na vinyimbo kibao walikuwa wanatufundisha - Nakumbuka wimbo mfupi mmoja siku ya kumaliza darasa la saba picknic , tulichapishiwa vyeti kila mmoja aliitwa mbele kuchukua cheti kwa mgeni rasmi mratibu tarafa..huku shule nzima ikiimba wimbo huu

Ndugu... ( anatajwa mhitimu darasa la saba)
Simama ukachukue cheti chakooo

kiitikio - Ukachukue Cheti, Ukalijenge taifa, taifa lakungoja ukatende uliyoangizwaa ..

Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana, best student wa mwaka pia tulikuwepo wazee wa mizawadi.

aisee acha tu, siku ya mkesha wa x-mas miaka hiyo, majibu yanakuja kijijini sita tumefaulu - mimi Moshi tech, Mengine Tabora Boys, Girls, na Mazengo

acha bwana, mkuu unaturudisha enzi za utaifa kwa kweli kakaa - tumetoka mbali wengine.

Mfunyukuzi kweli unafukunyua.


Sina kawaida ya kusoma post ndefu kama hii mpaka iwe imenivutia. Imekaa vizuri mkuu, umenikumbusha mbali sana!
 
ha ha ha, mi nakumbuka vilikuja vitoto toka mjini viwili vinavaa safi uniform smart, tatizo havikuwa na akili sasa navionyesha hesabu na sayansi, asubuhi vinaniletea maadazi- saa 4 vinanipe hela kila siku. aaaa kile cha kiume kwa nini kisiwe ki shemeji - akili ikanisaidia nikavuta mzigo fastaa - hapo darasa la tatu.

Hahahaha! Hao sio sisi!
 
aaaa kile cha kiume kwa nini kisiwe ki shemeji - akili ikanisaidia nikavuta mzigo fastaa - hapo darasa la tatu.

darasa la tatu ndugu yangu? mimi wakati huo nilikuwa ndogo sana nilikuwa mshikilia mapembe tu wakati ng'ombe akikamuliwa mpeleka barua, kuangalia usalama kama mwl haji mwisho nanunuliwa muwa.
 
kuna kamwalimu ka hesabati kalikuwa kananambia nikapenyezee bange, hako kamwalimu kalikuwa kanavuta kuliko bobu male! kama hujakapenyezea bange kanakuloga wewe na familia yako! kakishavuta bange zake mpaka 1+1 utakaona kanatafuta kalkuleta.

Hahahahaha! Nimeshindwa kujizuia kucheka mbele za watu hapa ofisini, mpaka wananiuliza kulikoni. Hujatulia kabisa wewe klorokwini!
 
hii kali namkumbuka mbabe mmoja alikua anakaa nyuma kabisa ya darasa basi maticha waliofundisha masomo yakimbore anapanda dirisha live anasepa ticha anabaki kutingisha kichwa tu
 
Mabraza men wa enzi hizo walikuwa wakivaa taugh boot aina ya BENQ na raba za kina Ken Mkapa na suruali za LEGGS wakati kina FirstLady wa enzi hizo walikuwa wanatoka na raba za Leso na magauni yenye mikanda ya vipepeo bila kusahau sie wagumu tulikuwa tunatune Kung-fu shoez teh teh
umesahau cha cha cha,au zile raba za bora
 
Naona mabishoo wa Clouds wameiga hapa nao eti wamekuja na operation ya unakumbuka nini ulipokuwa shule, JF iko juu sana kumbe mambo mengi ya wanaojiita watoto wa mujini wanayavumbua humu...
 
nakumbuka kazi ya kuwahi namba kila asubuhi na ukichelewa ni fimbo kwa kwenda mbele
 
nilikuwa mvivu sana kuamuka asubuhi mama akiniamsha nilikuwa namdanganya leo tumeambiwa twende mchana, sikumoja nikakosea step nikamwambia shule imefungwa eebwanaa.. alinibeba kimsobesobe hadi shuleni nikakuta wenzangu wako mstarini mwl mkuu alikuwepo nililambwa mboko kwanza mama akaja mwl wa darasa akaja mwl wa zamu mwisho mkuu mwenyewe wiki nzima matak o yakawa yamevimba sikurudia tena.

uliweza kukaa darasani kweli mkuu....maana makalio yalikuwa yamevimba siyo?
 
Nilikuwa nasubiri wakati wa mapumziko kukunua bagia,mabumunda,visheti na ubuyu,na iskirim alafu unatemea mate ili usiombwe

halafu una-scream 'hakiombekiiiiiiii!',kudadadeki walai.life was so sweet,hamna kuwaza kulipa bili,kodi,mafuta garini,ada na........dah..hata yale 'mambo yetu' ilikua hamna kufaidi sana!
icon7.gif
 
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
Hii..." Saaa..imefikaaa..ya kwenda nyambani....mama amepikaaa...wali na nyama....Saa imefika ya kwenda nyumbani Mama amepikaaa wali na nyama.......Kwaheri mwalimu .....kwaheriii...tutaonana keshooooooooooo..."basi hapo ni Mbio mtindo mmoja madarasa ya udongo...basi wengine tunaruka madirishani.....hapo jumatatu lakini SHATI halitamaniki...daaaah...aiseee...nakumbuka mbali..mno....daaaah..
 
..........Nakumbuka nyimbo tu za darasa la kwanza, maana madarasa mengine sikusoma hapa bongo.
Mabata madogo madogo yanaogelea, yanaogelea ktk shamba nzuri la bustani.............
Hesabu mama ohhh hesabu, hesabu ninakupenda ahhhh hakika.....................
...........Vile vile nakumbuka kababu, ice cream, sambusa na uji wa mchele...........I wish enzi hizo zirudi.
 
Shule zetu nyingi tulizosoma zilikuwa hivi na akili zilikuwemo leo hii mazingira mazuri na facility kwenye shule nyingi hasa za mjini zipo ila mitoto bomu bomu sijui tatizo ninini hasa au ndio hivyo tena nchi imeharibika na haina mwenyewe kuanzia chini hadi kwa wenye nchi???
3583548_orig.jpg
Tatizo la kizazi cha sasa ni chipsi kuku, simu, kuangalia movie, series, kuangalia uchafu kwenye internate basi unafikiri akili zitatoka wapi sana sa wanachofikiria ni kuiba pepa tu ili wafaulu.

Enzi zetu Walimu walikuwa na ari ya kufundisha, hakukuwa na mambo ya movie, sijui series, sijui chips kuku weekend, sijui internate, simu n.k hivyo hata watoto kusoma ilikuwa ni kusoma kwelikweli hakuna kuibia najua shule ya msingi ilikuwa mwanafunzi ukiwa wa kwanza unapewa zawadi kwa hiyo ilikuwa inatia hamasa ya kila mtu kutaka awe wa kwanza darasani.

halafu vitu kama vitabu, madaftari, kalamu za risasi, rula ni vitu ambavyo vilikuwa vinapatikana shule na vya kutosha. mwanafunzi alikuwa akikosea lazima achapwe viboko vivyo watoto walikuwa na adabu sio utovu wa nidhamu kama watoto wa siku hizi. masomo ya sayansi kimu yalikuwa yanatusaidi kujua usafi na kupika sijui siku hizi kama bado yanafundishwa shule ya msingi maana siku hizi mtoto unamkuta ni wa kudekadeka tu.
 
Ahha umenikumbusha mbali sana,kuna mwalimu mmoja nadhani alitoka JKT ndo akaja kwenye shule niliyokuwa nasoma,mwalimu alikuwa anatembeza fimbo sijawahi kuona,sasa usiombe iwe zamu yake watu tulikuwa tunawahi shule kwa kuogopa fimbo,na kila nimwonapo huwa nakumbuka though sasa hivi amekuwa mchungaji kwa hiyo kila nikimwona nakumbuka enzi za shule za msingi.
 
Na mimi nakumbuka niliwahi kusoma shule moja Wilolesi iko Iringa kuna mwalimu mmoja alikuwa mkuu wa shule alikuwa anaitwa mwalimu Kajiba alikuwa hodari na shule ilikuwa inasifika kwa kuponda kokoto, tulikuwa wajasiria mali wa kuponda kokoto si mchezo kila wiki angalau kila mwanafunzi anakuwa na debe lake moja la kokoto. Nakukumbuka hapo shule kulikuwa na miti miwili mikubwa ina matunda ya mitoo nafikiri watu wa Iringa wanaijua basi wakati mwingine tukiwa darasani unasikia ubwabwa unanukia tunaambizana unasikia harufu hiyo ya ubwabwa hivyo majini yako yanapika juu ya hiyo miti yaani hata matunda yake tulikuwa tunaogopa kuyala kwa ajili ya hizo imani tulizokuwa tumejiaminisha kuwa kuna majini juu ya miti tehe tehe.
 
Mi nakumbuka siku ambayo nyumbani walikuwa wachinje mbuzi hivyo sikuweza kuhudhuria shule ili niweze kukishiriki kisusio kikiwa cha moto. Kesho yake mwalimu wa darasa alikuwa akiita majina na ulikuwa unapaswa uitike jana na leo mwaalimu. Mimi kwa hofu ya kufupisha sentensi nikaitika juzi na leo mwaalimu, maana jana yake sikuwepo. Ndio mwalimu kanitoa mbele ya darasa kutaka kujua kulikoni, pamoja na kujitetea kuwa jana yake sikuweza kuhudhuria kwa sababu nyumbani tulichinja haikusaidia. Mwalimu alinipeleka kwenye ofisi ya staff waalimu waliokuwepo wakanigombania kama mpira wa kona kwa mboko.
 
Enzi zile duh........raha,

Kwenye mchakamchaka ni saa kumi usiku...... kuwahi namba, Hakuna kupiga kelele darasani, mambo ya table (hesabu za kuzidisha za kushtukizwa na teacher)....kumi na mbili mara sitaaaaaa mwl anakulamba fimbo mpaka utoe jibu.

Gwaride kwa filimbi:

Baba paka aliyesema.....
sisi hapa, ni watoto wadogo, twajifunza siasi ya ujamaaa, mwalimu wetu katfundisha adabu na heshima mbele ya wazaia wetu!.......
Oh, vijana, vijaaaana, vijana,vijana tayari, ..kulitumikia, taifa, taifa Tanzania, oh Walimu.......
Nyerere yupo ukiona kundi la siasa, Nyerere yupo,...Kawawa yupo......nk
Sisi tunataka kuwasha mwenge, tunataka kuwasha mwenge,
Naapana naahidi mbele ya chama,
Naipenda sana shule yetu
shule yetu imejengwa kilimani
Azimio la Iringa, lasema siasa ni kilimo, wananchi tushike majembe tukalime, tupate mazao bora.
Tumeuona mpilipili na maua yake ......
Ahaa, chama cahetu cha mapinduzi cha jenga nchi, Nyerere ahaaaa, Karume cha jenga nchi...

Nyimbo za mchakamcha, darasani na kuhamasishana

Iddi Amiri akifa, mimi siwezi kulia,ntamtupa kagera awe chakula cha mamba.
Mwenge huo mwenge.....mbio mbio
twende tukawinde leeeeo, tukawindeee vipepeo
Hasiependa shule ni mjinga kabisa
Kikojozi na nguo twaichoma moto!
Baba yake Juma ametia vilaka matakoni mwake vinauluzana umekuja lini....

Kwaya:

Karibu sana shuleni kwetu mtukufu Mkuu wetu wa Mkoa,

Ngonjera:

Hodi hodi uwanjani,

Vitabu:

Juma na Roza
Kalumekenge
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
siku ya gulio Katelelo
Kibanga ampiga Mkoloni
Brown ashika tama
Safari yenye mkosi
Nondo mla watu

Maarifa

Barua za mapenzi zinachorwa Mkuki na moyo, unaanza na "Kwako Dada Mpendwa..."
Barua za mapenzi zinafichwa kwenye mikebe
Barua za mapenzi zikipatikana zinasomwa mstarini.
kumbebea mwalimu maembe
kumpelekea mwalimu misigo yake kwa demu
Kuchunguliwa wanafunzi wa kike wakiwa ****** au kwa vioo

Kazi za nje

Kumwagilia Busatan za shule
Kufyatua tofari
Kuja na nyasi shuleni
kuleta maji kumwagia viunga vya shule kuondoa vumbi
kulima mashamba ya Mwalimu, DRDD, Mkuu wa Wilaya nk.

Kutoka shule

sasa, sasa saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheri tutaonana keshoooooo!

zingine ni
Sikiri mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini......

Kofia nyekundu tarabushi inanipendeza mama..........
Nalalia kulia leo...................... Bibi tarabushi. nakwambia hapo ndio darasa la tatu nafikiri.


Asiyependa shule ni mjinga kabisa, barua ikija aitembeza kote....


Karudi baba mmoja,
Toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja ili kumtaka hali............


halafu pia enzi hizo watu wa mazingaombwe wanakuja kutuletea mazingaombwe yao mara unatolewa shati jipya la shule, mara hela do!

Azimio, Azimio, Azimio la Arusha, lilitangazwa tano mbili sitini na saba Azimio la Arusha.

Kaka yangu sikiliza
nataka kukuambia,
Azimio la Arusha,
lilizaliwa Arusha.............


halafu mambo ya kucheza rede, uki, mdako, kujipikilisha, kiboleni, hahahaaaa we acha tu...
 
Back
Top Bottom