Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

mzee ELOWAI huwa ni mbaya kwa lediiz!

mara nyingi ndizo siku wanazivunjiwa vikombe vyao!......

Geoff hebu tuliza mzuka wako ..Primary unavunja kikombe labda miaka hii ya 2000 binamu
 
Umenikumbusha tulipoambiwa tuende na majembe shuleni wakati nyumbani hakuna jembe, ukimwambia hivyo mwalimu anakuona kama bishoo na anatangaza mboko dhidi yako. Hivyo busara ya umri inakuagiza kusepa, ukishasepa leo ina maana msala unahamia kesho, inabidi na kesho usepe. Mwishowe unaanza kujilaumu kwanini usingekubali mboko na mambo yangeisha kitambo, inakuwa majuto mjukuu.

Kingine ni yale mambo yetu ya mwaka wa mwisho yaani LY, hapa tulikuwa tunajiona wajanja balaa hata mwalimu unamuona kama mwenzio vile. Wakati huo bana we acha tu, kama kungekuwa reverse mie ningeweka!!
 
Firstlady vipi siku ya picnic ya darasa la saba ulivaa nini wakati huo - vipi disco lilikuwaje?

nakumbuka nilifungua mziki na mwalimu mmoja wa kike - mwalimu Agwene na wimbo wa -----

Siwezi kuuuwa mtu mamaaa dhambi kwa mungu mamaeee, shauri yakooo, shauri yako eeee...... sijui kama watu wanaujua

nilikuwa na rafiki mmoja mmama kweli wakati huo alikuwa ananipenda sana aliniazima nguo ya njano na heleni kuuubwa za njano ..nitascan vipicha vyangu nikutumie tunatoka mbali uone hiyo nguo ya kuazima miaka hiyo...
 
Nakumbuka tulikuwa wakakamavu sana. Hebu fikiria, tulikuwa tuna kamchezo kahatari sana kakutumia matairi ya magari(used), unajikunja kwenye tairi,unasukumwa kwenye kamamteremko hivi,halafu tairi ikianza kuongeza mwendo,unachomoka nje kishujaa. Ole wako ukosee taiming ya kuchomoka. Just imagine kitakachotokea. It was a very risk game but we enjoyed it.
 
Mchezo wenu afadhari, wetu ilikuwa tunapanda wenye jiwe kilimani, tunaweka box tunakaa then tunaseleleka hadi chini kama mita 50 mapka 80 hivi. sasa kasheshe box lichanike sasa huo msuguano kaptula yote inachanika ngozi ya **** nyekunduu ukifika chini..... duh hamu yate ishakuisha
 
nilikuwa na rafiki mmoja mmama kweli wakati huo alikuwa ananipenda sana aliniazima nguo ya njano na heleni kuuubwa za njano ..nitascan vipicha vyangu nikutumie tunatoka mbali uone hiyo nguo ya kuazima miaka hiyo...

naisubiria kwa hamu...
 
naisubiria kwa hamu...
HEHEHE!mzee unaona kama ''milango imefunguliwa''......mkw wa n'tu huyo..SHAURILO!..MPIGIE SIMU LEMA AKWAMBIE YALIYOMKUTA...!festiledi nae ni ''mtoa roho''
 
duh nimecheka sana na mmenikumbusha mbaaali sana atiiii, sasa mbona mwaharibu mwelekeo wa thread semeni basi mmesoma shule zipi za mguu mmoja
 
HEHEHE!mzee unaona kama ''milango imefunguliwa''......mkw wa n'tu huyo..SHAURILO!..MPIGIE SIMU LEMA AKWAMBIE YALIYOMKUTA...!festiledi nae ni ''mtoa roho''

ha ha haaa duh - mbona unaniogopesha Geoff, picha tu za utotoni kakaaa- very funy.

Unanikumbusha tena tulivyokuwa tunatembea na vioo vidogo mfukoni, wakati wa ukaguzi msitarini unakiangusha unakisuma kwa miguu hadi kati ya miguu ya dem....then unacheki pichaa --LIVE

Sooo ukikamatwaaa bwaana......

Nyumbani mama anagomba mbona vioo vyake vinapotea kumbe sisi tulikuwa na mpango mkakati..... ( Strategic plan ya kideo cha bure shuleni)
 
HEHEHEHE!
hili la kioo had leox-pin analipraktisi kazini kwake
 
Mabraza men wa enzi hizo walikuwa wakivaa taugh boot aina ya BENQ na raba za kina Ken Mkapa na suruali za LEGGS wakati kina FirstLady wa enzi hizo walikuwa wanatoka na raba za Leso na magauni yenye mikanda ya vipepeo bila kusahau sie wagumu tulikuwa tunatune Kung-fu shoez teh teh
 
HEHEHEHE!
hili la kioo had leox-pin analipraktisi kazini kwake

ila siku hizi anatumia naked eyes wala si kioo!!! (p.i.m.p) afu anawaambia laivu...oyaaa sista eeeh umekaa vibaya naniii yako ya kijani inaonekana!!!
 
Mabraza men wa enzi hizo walikuwa wakivaa taugh boot aina ya BENQ na raba za kina Ken Mkapa na suruali za LEGGS wakati kina FirstLady wa enzi hizo walikuwa wanatoka na raba za Leso na magauni yenye mikanda ya vipepeo bila kusahau sie wagumu tulikuwa tunatune Kung-fu shoez teh teh

raba za loso na mikanda ya vipepeo imerudi siku hizi!!!!!!!!!!!

in new names ''all stars'' sijui zile raba zinaitwa!!!! na kina dada mamikanda yanajaa kiuno lol!!!
 
nilikuwa mvivu sana kuamuka asubuhi mama akiniamsha nilikuwa namdanganya leo tumeambiwa twende mchana, sikumoja nikakosea step nikamwambia shule imefungwa eebwanaa.. alinibeba kimsobesobe hadi shuleni nikakuta wenzangu wako mstarini mwl mkuu alikuwepo nililambwa mboko kwanza mama akaja mwl wa darasa akaja mwl wa zamu mwisho mkuu mwenyewe wiki nzima matak o yakawa yamevimba sikurudia tena.
 
kwenye darasa langu mimi tu ndiye nilikuwa na kandambili wengine pekupeku, wakati wa kwenda nyumbani nazibeba mikononi zisichafuke matope.

Duh! Hiyo kiboko. Kuna shule moja ya msingi niliwahi kusoma kwa muda kijijini alikokuwa anaishi bibi yangu. Huko wasichana walikuwa wanakuja wamejifunga migolole (sio khanga). Yaani unakuta mwanafunzi ana nguo moja tu, hiyo hiyo ni ya shule na hiyo hiyo ya nyumbani. Hakuna unifomu.

Mimi na dada yangu tulikwenda kwenye ile shule tukiwa na unifomu na viatu. Dada yangu akapewa u-dada mkuu kwa kuwa alikuwa madarasa ya juu...mimi darasani kwetu (la pili) nikapewa u-monita!
 
ha ha ha, mi nakumbuka vilikuja vitoto toka mjini viwili vinavaa safi uniform smart, tatizo havikuwa na akili sasa navionyesha hesabu na sayansi, asubuhi vinaniletea maadazi- saa 4 vinanipe hela kila siku. aaaa kile cha kiume kwa nini kisiwe ki shemeji - akili ikanisaidia nikavuta mzigo fastaa - hapo darasa la tatu.
 
mabraza men wa enzi hizo walikuwa wakivaa taugh boot aina ya benq na raba za kina ken mkapa na suruali za leggs wakati kina firstlady wa enzi hizo walikuwa wanatoka na raba za leso na magauni yenye mikanda ya vipepeo bila kusahau sie wagumu tulikuwa tunatune kung-fu shoez teh teh

hiyo ya kweli mikanda ya vipepeo nimeikumbuka hahahahahaha
 
Back
Top Bottom