Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Enzi zile duh........raha,

Kwenye mchakamchaka ni saa kumi usiku...... kuwahi namba, Hakuna kupiga kelele darasani, mambo ya table (hesabu za kuzidisha za kushtukizwa na teacher)....kumi na mbili mara sitaaaaaa mwl anakulamba fimbo mpaka utoe jibu.

Gwaride kwa filimbi:

Baba paka aliyesema.....
sisi hapa, ni watoto wadogo, twajifunza siasi ya ujamaaa, mwalimu wetu katfundisha adabu na heshima mbele ya wazaia wetu!.......
Oh, vijana, vijaaaana, vijana,vijana tayari, ..kulitumikia, taifa, taifa Tanzania, oh Walimu.......
Nyerere yupo ukiona kundi la siasa, Nyerere yupo,...Kawawa yupo......nk
Sisi tunataka kuwasha mwenge, tunataka kuwasha mwenge,
Naapana naahidi mbele ya chama,
Naipenda sana shule yetu
shule yetu imejengwa kilimani
Azimio la Iringa, lasema siasa ni kilimo, wananchi tushike majembe tukalime, tupate mazao bora.
Tumeuona mpilipili na maua yake ......
Ahaa, chama cahetu cha mapinduzi cha jenga nchi, Nyerere ahaaaa, Karume cha jenga nchi...

Nyimbo za mchakamcha, darasani na kuhamasishana

Iddi Amiri akifa, mimi siwezi kulia,ntamtupa kagera awe chakula cha mamba.
Mwenge huo mwenge.....mbio mbio
twende tukawinde leeeeo, tukawindeee vipepeo
Hasiependa shule ni mjinga kabisa
Kikojozi na nguo twaichoma moto!
Baba yake Juma ametia vilaka matakoni mwake vinauluzana umekuja lini....

Kwaya:

Karibu sana shuleni kwetu mtukufu Mkuu wetu wa Mkoa,

Ngonjera:

Hodi hodi uwanjani,

Vitabu:

Juma na Roza
Kalumekenge
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
siku ya gulio Katelelo
Kibanga ampiga Mkoloni
Brown ashika tama
Safari yenye mkosi
Nondo mla watu

Maarifa

Barua za mapenzi zinachorwa Mkuki na moyo, unaanza na "Kwako Dada Mpendwa..."
Barua za mapenzi zinafichwa kwenye mikebe
Barua za mapenzi zikipatikana zinasomwa mstarini.
kumbebea mwalimu maembe
kumpelekea mwalimu misigo yake kwa demu
Kuchunguliwa wanafunzi wa kike wakiwa ****** au kwa vioo

Kazi za nje

Kumwagilia Busatan za shule
Kufyatua tofari
Kuja na nyasi shuleni
kuleta maji kumwagia viunga vya shule kuondoa vumbi
kulima mashamba ya Mwalimu, DRDD, Mkuu wa Wilaya nk.

Kutoka shule

sasa, sasa saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheri tutaonana keshoooooo!
 
kwenye darasa langu mimi tu ndiye nilikuwa na kandambili wengine pekupeku, wakati wa kwenda nyumbani nazibeba mikononi zisichafuke matope.
 
kwenye darasa langu mimi tu ndiye nilikuwa na kandambili wengine pekupeku, wakati wa kwenda nyumbani nazibeba mikononi zisichafuke matope.
hehehehehe!
Interestingi
 
niliwahi kukutwa na mama mzazi NAFANYA MATUCI NA HAUSIGELI!..halafu yeye alikuwa mkubwa sana kwangu.mimi nilikuwa darasa la tatu
Mh! Wewe hukuungua na huyo mdada mkubwa?!!....
 
Nakumbuka mwaka 1978 wakati wa vita tuliambiwa tuchimbe mahandaki shuleni, nilikuwa mtoro sana siku moja mwl akatubamba tumejificha humo siku nzima na wasichana.

hee mwenzetu umekula chumvi nyingi hongera
 
Nilivyokuwa shule yamsingi tulitumwa panga na jembe
pia kuni na maji na nilikuwa na go peku ka ng'ombe
Mwalimu wetu alikuwa mcheshi sn na alikuwa chapombe
Alinisihi mara nyingi nisiwe ***** ka Mgombea Ubunge
Maana ninaweza angamiza JF na letu tukufu Bunge.

Alieendelea kusema kuna waut wanajiita akili kichwani
Ukiitazama kwa undani wa posti zao utakuta iko *** chini,
Ukitaka kuaamini anakwepa hata vimichango na kuhoji kwa nini,
Hata mwenye nyumba /forum akimuuliza anadai utani do nini,
 
deh deh deh ukiridi bitwini ze lainz ,utagundua kwamba meseji senti
 
kwenye darasa langu mimi tu ndiye nilikuwa na kandambili wengine pekupeku, wakati wa kwenda nyumbani nazibeba mikononi zisichafuke matope.

I love this!!!!!!!!!
 
mie sitasahu LY yangu ilivyokuwa jamani kweli tunatoka mbali sana ..
 
Duh miaka ya 80 -90 kaka, mimi nilikuwa time keeper, sasa rafiki zangu walikuwa wananiambia nigonge kengere kabla ya muda ili tuwahi kucheza mpira - mpira wa makaratasi.

Darasa la tano namkumbuka mwalimu mmoja wa sayansi, akija darasani lazima aje na fimbo kama 10 hivi, anaanza kukumbushia somo la mwisho, anayeshindwa anapita mbele... anangoja super six....aisee kweli shule ilikuwa chungu kipindi chake kikifika.

Kuwahi number saa moja pia ilikuwa tatizo kwangu, ukicheliwa tu unakuta inakuwa imekula kwako.....moja...mbili.....tatu....nne etc

Mkaguo wa mwili ilikuwa soo, Kwa wale wamesoma vijijini ilikuwa hatari kukutwa na chawa, nguo hujafua, magaga ya miguu etc. Mimi nilikuwa ktk bendi ya shule nakumbuka wimbo wa mkaguo ulikuwa unaitwa kwa filimbi na bendi .... as Baba pakaa akasemaa twendeni tukawinde.....

Mwalimu Mkuu alikuwa mzee anaitwa Bebenya.... sasa lazima muimbe kumsifika kila siku asubuhi na jioni kabla hamjaenda nyumbani - tuliimba twampenda bembenya twampenda bembenya twampenda bebenyaaa eeeee aiyelele twampenda bebenyaaaa - tukae kwa amani tukae kwa amani tukae kwa amani eeee.....

Haraiki ya zile nyimbo za utaifa tumeziimba sana, hawa walimu waliokuwa wametoka JKT wakati huo walikuja na vinyimbo kibao walikuwa wanatufundisha - Nakumbuka wimbo mfupi mmoja siku ya kumaliza darasa la saba picknic , tulichapishiwa vyeti kila mmoja aliitwa mbele kuchukua cheti kwa mgeni rasmi mratibu tarafa..huku shule nzima ikiimba wimbo huu

Ndugu... ( anatajwa mhitimu darasa la saba)
Simama ukachukue cheti chakooo

kiitikio - Ukachukue Cheti, Ukalijenge taifa, taifa lakungoja ukatende uliyoangizwaa ..

Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana, best student wa mwaka pia tulikuwepo wazee wa mizawadi.

aisee acha tu, siku ya mkesha wa x-mas miaka hiyo, majibu yanakuja kijijini sita tumefaulu - mimi Moshi tech, Mengine Tabora Boys, Girls, na Mazengo

acha bwana, mkuu unaturudisha enzi za utaifa kwa kweli kakaa - tumetoka mbali wengine.

Mfunyukuzi kweli unafukunyua.
 
mie sitasahu LY yangu ilivyokuwa jamani kweli tunatoka mbali sana ..

Firstlady vipi siku ya picnic ya darasa la saba ulivaa nini wakati huo - vipi disco lilikuwaje?

nakumbuka nilifungua mziki na mwalimu mmoja wa kike - mwalimu Agwene na wimbo wa -----

Siwezi kuuuwa mtu mamaaa dhambi kwa mungu mamaeee, shauri yakooo, shauri yako eeee...... sijui kama watu wanaujua
 
FESTILEDI mtoto wa juzi tu....alikuwa hajazaliwa
 
ilikuwa tukimaliza masomo ya siku,ilikuwa ni darasa la pili miaka ya 80 tunapitia mashambani kwa watu kuiba machungwa ndizi etc, sasa tunalazimisha wasichana wakwee juu ili tuwachungulie chup** zao, mmoja wao one day akavua chu**pi akaiweka ndani ya mkoba ndo akakwea, huku anatamba mtangoja sana nyie!! mnataka mnichungulie chpi yangu leo hamuioni, kaacha duka wazi nasisi wala hatukuwa na hamu ya kuendelea kuchungulia kwani chpi ishavuliwa. daaahhh enzi za mwalimu bwana!
 
Back
Top Bottom