Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
shikamooo ,mzee 1985 primary ..dah !!! hatar sana jf wakongwe wengiMimi nakumbuka gwaride la kutuingiza darasani, adhabu za kuchimba visiki na kufyatua matofali na yule mshikaji aliyekuwa anatukusanya kila jumatatu na kutuimbia nyimbo mpya kutoka kwenye kipindi cha misakato. Hiyo ni azimio primary school Mbeya mwaka 1979 hadi 1985
Marahaba kijana.shikamooo ,mzee 1985 primary ..dah !!! hatar sana jf wakongwe wengi
pamojaaMimi kwakweli nakumbuka kuwekea watu vioo chini ili niwachungulie,pia nakumbuka siku ya usafi likuwa ni J3 na Alhamisi nilikuwa nafua leso ili kucha zing'ae.
Hahaha aya mkuuuNiliwahi kukojoa darasani baada ya mwalimu kunizua kwenda chooni. Daaah Mwanafunzi mmoja akausoma mchezo weeee akatibua kwa ticha nilichapwa njiti R.I.P madam wangu wa darasa la kwanza
Na Wa kwanza lazima atoke MwengeBinafsi nimesoma Shule ya msingi Jamhuri mjini Moshi, nilikuwa naishi Police line.Mambo nayoyakumbuka nilipokuwa nasoma Primary:
1.Kupigana siku ya kufunga shule.
2.Kutoroka darasani kwa kupitia dirishani Mwl wa Hisabati anapofundisha.
3.Kwenda Uzunguni kuangua maembe na kuchuma zambarau.
4.Kutoka Police line hadi Kwa Fonga TPC kuchukua miwa.
5.Kwenda CCP na karandinga la Polisi kuangalia michezo mbalimbali iliyokuwa inajumuisha Polisi wa Mikoa yote Bara na Visiwani.
6.Nawakumbuka baadhi ya wachezaji wa Polisi waliokuwa na mashuti makali kama Mohamed Ndutu,Brown Mwaitegete, Pius aliyekuwa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wengine wengi.
6.Kutoroka darasani kwenda kusaka kware.
7.Mechi ya mpira kati watoto wa Police line na wale watoto wa ng'ambo Police Dog Section, kila tukicheza nao lazima tuwafunge na ngumi lazima zipigwe.
8.Kushindanishwa shule kitaaluma Korongoni, Muungano,Mwenge, Jamhuri na Mawenzi, shule yetu kila tukishindanishwa tunakamata nafasi ya pili, licha ya kuwa na watoto watukutu wa line.
Wewe unakumbuka nini enzi ukisoma Primary?
Duniani milima haikutani....mapinduzi