Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Mimi nakumbuka gwaride la kutuingiza darasani, adhabu za kuchimba visiki na kufyatua matofali na yule mshikaji aliyekuwa anatukusanya kila jumatatu na kutuimbia nyimbo mpya kutoka kwenye kipindi cha misakato. Hiyo ni azimio primary school Mbeya mwaka 1979 hadi 1985
 
Mimi nakumbuka gwaride la kutuingiza darasani, adhabu za kuchimba visiki na kufyatua matofali na yule mshikaji aliyekuwa anatukusanya kila jumatatu na kutuimbia nyimbo mpya kutoka kwenye kipindi cha misakato. Hiyo ni azimio primary school Mbeya mwaka 1979 hadi 1985
shikamooo ,mzee 1985 primary ..dah !!! hatar sana jf wakongwe wengi
 
Niliwahi kukojoa darasani baada ya mwalimu kunizua kwenda chooni. Daaah Mwanafunzi mmoja akausoma mchezo weeee akatibua kwa ticha nilichapwa njiti R.I.P madam wangu wa darasa la kwanza
 
Kale ka Bendi ka Ukaguzi usafi kakianza nilikuwa nachukia sana. na kuwahi number?

But Ugonjwa wangu mkubwa ulikuwa niku watizama kwa matamanio, wanafunzi wasabato, TARIME SEC. na nguo zao nyeupe nachizika kinoma, nilkuwa nawaona km Malaika, hasa wakija kanisani kuimba kwa mbwembwe na kwaya yao maalumu! wakisindikizwa na gari lao maalum, pembeni limeandikwa MSAADA WA SIDA. neno SIDA. nikatafsiri mwandishi alikosea ilikuwa ni msaada wa shida.

kumbe sirka la SIDA lilikuwepo kitambo?
 
Tulikuwa wezi sana wa vitumbua , bagia na hela za wauzaji yaani kifupi tuliishi vizuri, kula na kushiba lkn kwa kutumia nguvu za giza, nilikuwa nawapanga rafiki zangu wezi kwa mstari kuelekea nyuma yangu, siku moja mke wa Askari Mpemba alileta visheti kuuza, km kawaida yetu tukatinga gengeni,... mida ya Break, ee! Bwana weee!!!... hee!

Mara mama mpemba si kapandisha mashetani ghafla bin vuu! akatamka ''huyu mtoto mbaya sana huyuuu'' kwa kurudia rudia, huku anakuja mbio kunikamata, huku akiweka tenge lake sawa kiunoni, mimi mbio!... chenga mbili tatu, mama kaangukia uso kwenye Minyaa! mimacho kodo utadhani tochi!! mimi huyooo nduki!!! ..nikatokomelea mbali na kujichanganya na wanafunzi, rafiki zangu Wambura Chacha! alikimbia kivyake. sijawahi kumuona huyo mama tena maishani! jioni nikamwambia bibi...

sijui km bibi alifanya yake sikumbuki wala sikuulizia ...
 
HABARI.....?..
wanahitajika madalali tufanye biashara ya magodoro moja kwa moja kutoka kiwandani ,,na mchakato wao mkubwa utakuwa ni kuleta wateja wa jumla na reja reja,,, na watapata malipo kama kawaida punde wanapoleta mteja...
kwa mawasiliano zaidi 0692449416
 
Shule ya msingi mgulani, opposite na Chuo cha DUCE. Yaani ni mwendo wa dumu na mfagio, kuna siku mnaweza kwenda shule mkaishia kwenda keko kutafuta majani ya UKOKA siku nzima bila kusoma yaani.
 
Binafsi nakumbuka kipindi cha tosamaganga boys home, pindi naanza shule darasa la tano nilikuwa bonge sana ndani ya miezi sita tu nilikata ringi hatari, muhula wa pili nilichojifunza ni kufungua kufuli la kila aina kama ndiyo elimu niliyo kwenda kujifunza...
 
Jmn mm unakumbuk ck moja nikiwa darasa la 6 nilikutwa na MWALIMU wa darasa nikiwa na fanya mapenz na mwanafunzi mwenxangu choon ,nilichapwa fimbo za kutosha . Kwahiy hiyo story cwez kusahau Kayoka maisha yangu yote
 
Kubana mzinga hasa kama nimechelewa shule mpaka mwalimu wa somo la kwanza achomoke ndo nazama darasani kupitia kwenye dirisha lililokatwa nyavu za kashata.
 
Maza alikuwa Mwalimu Mkuu asee nilikuwa mkorofi nachezea kipigo mpaka unaelewa shoo akikukuta kwenye kundi la wasumbufu unachezea fimbo mara mbili.... Malezi yako naona manufaa yake now kipenzi changu. I LOVE YOU MAMA[emoji3531][emoji817]
 
Binafsi nimesoma Shule ya msingi Jamhuri mjini Moshi, nilikuwa naishi Police line.Mambo nayoyakumbuka nilipokuwa nasoma Primary:
1.Kupigana siku ya kufunga shule.
2.Kutoroka darasani kwa kupitia dirishani Mwl wa Hisabati anapofundisha.
3.Kwenda Uzunguni kuangua maembe na kuchuma zambarau.
4.Kutoka Police line hadi Kwa Fonga TPC kuchukua miwa.
5.Kwenda CCP na karandinga la Polisi kuangalia michezo mbalimbali iliyokuwa inajumuisha Polisi wa Mikoa yote Bara na Visiwani.
6.Nawakumbuka baadhi ya wachezaji wa Polisi waliokuwa na mashuti makali kama Mohamed Ndutu,Brown Mwaitegete, Pius aliyekuwa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wengine wengi.
6.Kutoroka darasani kwenda kusaka kware.
7.Mechi ya mpira kati watoto wa Police line na wale watoto wa ng'ambo Police Dog Section, kila tukicheza nao lazima tuwafunge na ngumi lazima zipigwe.
8.Kushindanishwa shule kitaaluma Korongoni, Muungano,Mwenge, Jamhuri na Mawenzi, shule yetu kila tukishindanishwa tunakamata nafasi ya pili, licha ya kuwa na watoto watukutu wa line.
Wewe unakumbuka nini enzi ukisoma Primary?
Na Wa kwanza lazima atoke Mwenge
 
•Nani anaijua mifuko ya sport?
•Nani anajua njumu za Cossovo?
•Ni nani anafahamu kalamu za umbo la zamani?
•Na he ni nani kati yenu kuna watoto shule walikuwa hawachapwi viboko kosa kwao ni wachawi?
•Unamwambia nini sasa HEDI GERO NA HEDI BOYI?
•ELOWAYI AKUMBUKWE JUMA UREDI
•Ukienda chooni usikute watu wameandika kwa kinyesi tena kilichoandikwa ni matusi basi jua wewe umesoma ST. MSTARAABU.

#MKOLANI GEITA
 
Back
Top Bottom