SoC04 Wakurugenzi wa halimashauri wapatikane kwa mfumo wa ajira ili kuleta dhana ya utawala bora na uwajibikaji kwa wananchi na siyo kwa watawala

SoC04 Wakurugenzi wa halimashauri wapatikane kwa mfumo wa ajira ili kuleta dhana ya utawala bora na uwajibikaji kwa wananchi na siyo kwa watawala

Tanzania Tuitakayo competition threads

mackj

Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
84
Reaction score
98
UTANGULIZI.
Ni makala ya story of change ya jamii forum, inayochochea mjadala wa kitaifa juu ya masuala mbalimbali, nami nikiwa nimeangazia dhana ya utawala bora nchini Tanzania, ili kuipata “Tazania tuitakayo” jina langu ni Makiwa Jumanne

Ni hivi karibuni Taifa la Tanzania limetimiza miaka 63 tangu uhuru wake uliopatikana mnamo desemba 9, mwaka 1961, likiwa ni taifa moja wapo kati ya mataifa machache yaliyopata uhuru wake bila kumwaga damu barani afrika
Licha ya umri huo mkubwa kama taifa huru, lakini bado kumekuwa na changamoto ya ukoloni mambo leo kwa baadhi ya maeneo ya kiutawala, unaotekelezwa na watawala kwa kuchagizwa na mfumo wa kikatiba ambao hata hivyo, unaonesha wazi kuwa hata katiba hiyo ni chakavu kwani ilitungwa tangu mwaka 1977

Hii ni wazi kwamba haiwezi kuakisi uhalisia wa mahitaji ya sasa kama taifa, ukizingatia kwamba nchi imekuwa na idadi kubwa ya watu, uelewa wa watu wake pia umekua, kutokana na mwamko wa wazazi kupeleka watoto shule, na kiwango cha mahitaji ya watawaliwa wenyewe kimeongezeka katika nyanja mbalimbali, ikiwemo demokrasia, utawala wa sheria na sayansi na teknolojia

Licha ya wanasiasa na wananchi wa makundi mbalimbali kupiga kelele juu ya mabadiliko ya katiba lakini bado kumekuwepo na mkwamo wa agenda hiyo, hasa tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, na uchaguzi mkuu 2025.

Katika mfumo wa sasa wa kikatiba, Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ndiye aliye na mamlaka ya kuwateua mawaziri, manaibu waziri,makatibu wakuu, manaibu katibu wakuu, na wakurugenzi, hali ambayo inadhoofisha uwajibikaji na kudumisha dhana ya utawala Bora, mfano katika wizara ya TAMISEMI, wizara hii iko chini ya ofisi ya Rais, ambapo kwa mujibu wa sheria ya tume ya uchaguzi iliyopita, kabla ya sheria mpya ya tume ya uchaguzi ya 2024 kutungwa, Mkurugenzi wa Halimashauri iwe ya jiji,mji au manispaa ndiye aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi katika jimbo husika kitu ambacho kimuundo kilikuwa kinazua maswali mengi sana juu ya uwepo wa uchaguzi huru na wa haki kwa vyama vyote.

Ni miaka mingi kumekuwepo kilio cha wanasiasa juu ya wakurugenzi kutokusimamia na kuratibu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge, kwakuwa ni wateule wa Rais ambaye pia anakuwa ni mgombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi husika, na mwenyekiti wa chama kinachoshiriki uchaguzi, kwa madai kuwa mara nyingi wanaweza kuwa wanapokea maelekezo kutoka kwa wenyeviti wa wilaya na mikoa wa chama kinachounda dola, ili kutoa upendeleo wa namna fulani, kwakuwa wao na wakuu wa wilaya wanawajibika moja kwa moja ndani ya vikao vya maamuzi vya chama hicho, kama wateule wa mwenyekiti wa chama Taifa, hivyo kusababisha haki kutotendeka hata pale vyama pinzani vinapokuwa vimeshinda chaguzi.

Pamoja na kufutwa utaratibu huo kupitia sheria mpya ya tume ya uchaguzi, na ili kupata tanzania tuitakayo ni muhimu wakurugenzi wa halmashauri kupatikana kwa mfumo wa ajira na siyo kuteuliwa, jambo ambalo litapanua uwajibikaji na dhana ya utawala bora itaonekana, kwani watatimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma na utawala bora, na watatekeleza majukumu yao kikamilifu bila kuyumbishwa na mifumo ya kisiasa,

Hoja hii ni nyeti sana kwa ustawi wa nchi na watu wake, na wadau wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kupitia majukwaa mbalimbali juu ya mfumo huu wa kikoloni, lakini bado watawala wanaweka masikio pamba kwakuwa wamekuwa wanufaika wamfumo huu

Aidha wakurugenzi wa Halimashauri wameshuhudiwa wakifanya kazi bila ufanisi kupitia ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) na kupelekea serikali kupata hasara katika miradi mbalimbali kutokana na uwezo mdogo, maana huteuliwa kisiasa bila kuzingatia uwezo wao kiutendaji
Ifahamike kuwa serikali za mitaa ndiko msingi wa maendeleo ya taifa unakoanzia na ndiko huduma nyingi za jamii zinazomgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja ziliko, na ndiko pato la ndani la Taifa (GDP) linakotengenezwa kwa makusanyo ya ushuru na tozo mbalimbali, hivyo haipaswi kuwa na mchezo wa siasa, badala yake panahitajika watu makini na wanaoweza kuwajibika kwa wananchi, nasiyo kuwajibika kwa watawala na hili ni jambo linalowezekana kufanyika na kwa kufanya hivyo tutaipata tanzania tuitakayo.

Mpaka kufikia hapo nakuwa sina la ziada hadi wakati mwingine jina langu ni MAKIWA JUMANNE

Kwaheri.
 
Upvote 1
Pamoja na kufutwa utaratibu huo kupitia sheria mpya ya tume ya uchaguzi, na ili kupata tanzania tuitakayo ni muhimu wakurugenzi wa halmashauri kupatikana kwa mfumo wa ajira na siyo kuteuliwa, jambo ambalo litapanua uwajibikaji na dhana ya utawala bora itaonekana, kwani watatimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma na utawala bora, na watatekeleza majukumu yao kikamilifu bila kuyumbishwa na mifumo ya kisiasa,
Kumbe hilo limerekebishwa! Basi tunaenda vizuri😊.

hivyo haipaswi kuwa na mchezo wa siasa, badala yake panahitajika watu makini na wanaoweza kuwajibika kwa wananchi, nasiyo kuwajibika kwa watawala na hili ni jambo linalowezekana
Mtoa mada mbona ni kama unaiwekea mipaka dhana ya uwajibikaji maana hata huyo mtawala anapaswa kuwajibika kwa wananchi pia.

Nadhani ile akili ya kikoloni bado inatutafuna kudhani kuwa wananchi ni wa mkoloni wakati yee mkoloni ni mkoloni tu.🤔. Ndio tunahamishia kwenye watawala wa serikali.

Asema hivi kwa sababu hii sio asili yetu tangu na tangu. Hapo zamani mwanakabila alikuwa ni wa mtemi na mtemi alikuwa ni wa mwanakabila vivyohivyo. Yaani mwananchi aseme mtemi wangu, na mtemi aseme mwananchi wangu na kila mmoja ako na majukumu na haki zake. Ndio maana watemi kuingia front na jeshi lake ilikuwa ndiyo kawaida.

Sijui tumeisahaulia wapi hiii!!!
 
Kimsingi tayari huyu mtawala amekosekana wa kumuwajibisha kutoka kundi la wananchi ndio maana tunahitaji kuanza na chini ili mwisho wa siku tufike juu
 
Back
Top Bottom