Wakurugenzi wa Makampuni ya Mafuta ya PUMA, Oryx, TOTAL na Lake Oil wakamatwa na Polisi kwa kuvuruga mfumo wa usambazaji!

Sasa si ndo biashara?,mfano mwaka huu watu wamestock mpunga kisha baadae kuuza kwa bei juu,
Hapa mi naona hii biashara ya mafuta ifanywe na serikali,hawa jamaa wafanye kazi za gereji kurepair magari,etc
We upo nchi gani, hiyo ni kinyume na sheria za nchi yetu, ni ujumu uchumi,yani unataka kupata super profit ununue kwa bei nafuu uje uuze kwa bei ya juu, pia unafanya bidhaa inaadimika sokoni, vijana mnataka kuongoza nchi ila vitu vya msingi hamvijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bei za mafuta huamuliwa na soko la dunia sio wao ewura wao wanatoa miongozo tu
 
Washtakiwe na wapewe kesi ya uhujumu uchumi na wapelekwe Segerea wakae hata mwaka. Walikuwa na kikao cha nini?. Kikao cha kutulangua?. Hawakufurahi bei ilipoteremshwa siku za karibuni. Ni nani hao katika nchi hii?.
 

You real said brother unaijua industry ya Mafuta vizuri within no time tutaanza kulia!!na kama ilivyo sema aerikali haiagizi hata lira moja ya mafuta so haina Uwezo wa kusambaza Mafuta hata kwa siku inchi nzima!tuache comedies jamani
 
Kwanini wasiwasikilize halafu mkawapinga kwa hoja na sheria? Kwani hao ni ACT mseme wanapanga maandamano?
 

serikali inapaswa kuchukua biashara ya mafuta ijenge vituo vyake kila mkoa itapiga mabilioni yanayokwenda nje kila siku biashara hii itawezekana kwa kuwa Mkulu hataniwi ni pesa chap chap na inalipa sana then tupungize kodi na ushuru kwenye maduka ya walalahoi!manake biashara nyingi za wapiga kura wa Mkulu zimeangushwa na kodi kubwa

hiki ni chanzo kipya cha mapato makubwa ya serikali wakichangamkie haraka tupate pesa ya kujenga SGR na kuwakomesha mabeberu, hili wazo lapaswa kutua mezani kwa Mkulu haraka! na amteu mwanajeshi mstaafu asimamie huo mradi mfano mkuu wa majeshi mstaafu nk na kila kituo kilindwe na mwanajeshi mwenye silaha ili staff waogope kuiba na kuwe na supervisor wanaokagua hesabu daily!
 
Kwanini wasiwasikilize halafu mkawapinga kwa hoja na sheria? Kwani hao ni ACT mseme wanapanga maandamano?

Mromboo, mimi sifahamu kwa nini wamekamatwa,nimetoa maoni yangu tu kufuatana na bei ya mafuta ilivyo shuka kutokana na Covid-19. Hilo ni punguzo la zaidi ya 50%. Suala la wao kukaa vikao sifahamu, tatajua kesho au mtondogoo kama jeshi la Polisi watatoa ufafanuzi (lakini uzi hapo juu umeandika wanavuruga mfumo wa usambazaji). Jeshi la Polisi ndio lenye mamlaka ya kumkamata mtu yeyote wanapokuwa na taarifa za uhalifu kwa kukusudia au kupanga njama. Ndio wenye mamlaka kikatiba, wanaweza kukusweka ndani then kesho yake wanakuachia na huwezi kuwashitaki popote.
 
Aiwezekani makampuni yote hayo yafanye collusion, tukisikiliza upande wa pili lazima tatizo litakuwa upande wa EWURA au TPDC.

Juzi kati TPDC walidai wao peke yao watakuwa na uhalali wa kuagiza nusu ya mafuta yanayoingia nchini kitu ambacho ukiangalia tu hili linaweza kuwa tatizo strategically kwa wengine.

Sasa sijui wanataka kuwalangua retailers wengine au kuna sababu zingine lakini nina imani tukisikia sakata lote tatizo litakuwa upande wa serikali.

Hizi ndio sababu watanzania wengi wanaonaga serikali isifanye biashara, tatizo mara nyingi utakuta sio ushiriki wao bali wanaingiaga bila ya strategy ya ushindani kupitia mamlaka yao wanavuruga kila kitu.

Nimpongeze Hussein Bashe juzi kati kwenye interview yake kasema ata hawa wazalishaji sukari wa ndani bei zao ni kweli faida yake ni ndogo kutokana na production costs zao au wanatumia tu oligopoly kuweka margin yenye ya faida juu sana. Kwa ivyo wameanza mchakato wa kuangalia cost zao kujua kama kweli mtanzania adhulumiwi kwa kuwekewa bei za juu. Wataendelea kuwalinda wazalishaji wa ndani lakini serikali aiwezi kuwafumbia macho wazalishaji wa ndani kama wao wenyewe awapo fair kwenye bei zao.

Kuna watu serikalini wana namna zao za kufanya mambo kupitia mamlaka waliyo nayo, ulinzi wanaopewa kupitia cover ya uzalendo na kuwalinda watakuja na vitu ambavyo vinaishia vuruga utaratibu wa kila kitu. Yaani hapa kwenye mafuta tatizo litakuwa upande wa serikali tu tukisikia upande wa pili.
 
You real said brother unaijua industry ya Mafuta vizuri within no time tutaanza kulia!!na kama ilivyo sema aerikali haiagizi hata lira moja ya mafuta so haina Uwezo wa kusambaza Mafuta hata kwa siku inchi nzima!tuache comedies jamani

Kwani unafikiri nani anayenunua mafuta kutoka nje? Hizi sio zama za zamani, JPM hana mchezo kama wao walifikiria wanaweza kufanya wanavyotaka imekula kwao. Tanzania kuna Serikali.
 
Chadema njooni huku wakurugenzi wa mafuta wanaonewa....tehtehteh
 

makampuni yote yaondolewe serikali inunue na kuuza mafuta mbona kwenye ndege tumeweza huku hatushindwi pia Mkulu akiamua na kuagiza, kuna hela sana huku!!
 
HAWAJAMAAA WANAHITAJI KUFIKISHWA MAHKAMANI WAPEWE ILE NAMBA ZETU ZA KULIPIA WAKISHAONA ZILE SIFURI MBELE HAKI NA WENGINE WATAJIUZULU NAFASI ZAOO
 
Wajinga hawa wapewe kesi ya uhujumu Uchumi. Mungu ambariki Magufuli. Viva baba kwene hili umenikoshaa.
Hawezi hao ni MABEBERU!!! Thubutuuu, ila wangekuwa ni watz, kesho tungesikia mengineee, lakini, PUMA, ORXY, TOTAL!!!
 
Hizo ndio sheria zi kipumbafu dunia ya leo ukicheza dk ama saa chache tu unakuwa umepoteza biashara kubwa.

Leo polisi wanakuwa na mamlaka hata ikithibitika walichemsha inakuwa poa tu.

Kwa namna hii usitarajie ukawa na jeshi lenye weredi.

Wakipigwa za uso kwa kulipa fidia wanapokuwa wanakosea hutasikia ujingaujinga ukifanyika. Watakuwa makini katika kutimiza majukumu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…