Siku hizi ni tofauti.. Kwanza uteuzi kisha ndio vetting .. Usishangae baada ya wiki wengine wakatenguliwa
Dada yangu (si mama kwangu), Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema "Rais huwa hakosei". Kwa usemi huo tu tayari alikuwa kakosea maana hakuna mtu asiyekosea, hayupo na hatakuwepo!
Ndio maana unahitajika upitiaji makini (keen vetting) katika kusoma, kuchambua na kuamua kabla ya kutandika mkeka wowote ule hadharani. Atakuja kuteua aliyekufa au mfungwa!
Sasa ona ambavyo kila uteuzi analazimika kurudiarudia na kurekebisha, hususan baada ya kukosa kutangulia uhakiki makini. Hata bunge la bajeti alilikosea mara kadhaa kwa kuliita bunge la katiba. Akasema: "sijui nina maradhi gani na katiba." Ni maradhi ya kukosea mara kwa mara kwa kukosa umakini!
Si maradhi ya katiba tu, bali hata maradhi ya wizara (mathalani kateua waziri wa tozo kandamizi badala ya waziri wa uchumi na mipango endelevu na yenye tija), maradhi ya mikoa, maradhi ya wilaya na sasa maradhi ya wakurugenzi wa halmashauri. Mkurugenzi mmoja anataka aongoze halmashauri mbili kwa wakati mmoja. Mara paap, kajikuta kakosea tena!
Je, atawezaje (au wasaidizi wake), kusoma na kuchambua kwa makini mikataba mikubwa yenye kurasa zaidi ya 800??!!
Sent from my TECNO LC6 using
JamiiForums mobile app