Wakurugenzi wapya walioteuliwa watakiwa kuripoti TAMISEMI wakiwa na CV pamoja na vyeti vyao

Wakurugenzi wapya walioteuliwa watakiwa kuripoti TAMISEMI wakiwa na CV pamoja na vyeti vyao

Only in Tanzania Unateua Mtendaji DED, Hauna CV yake ila unajua tu ya Kwamba ni MwanaCCM. Hatutakaa Tukafika " Kujenga Nchi Kwanza si Kazi Rahisi Kivile. Hawa ndio Watasimamia Wilaya Zetu ktk Allocation and monitoring of our scarce resources. Daaa!
Yale maandamano ya kesho kadi za UCHADEMA tunaonyesha na kujisajiri wapi?
 
Mkuu hiyo ya ualimu ni first appointment, vilevile ni taaluma. DED ni cheo ambacho mtu anakuwa promoted kutoka cheo chake cha chini
Sawa tunataka aje na vyeti vyake original huku tunazo copy tuu. Sasa ubaya uko wapi? au nyie mnadhani original inatunzwa na serikali
 
First appointment unakuwa DED? nimeona vibinti vibichi kabisa inawezekana ni first appointment from uvccm...
Mkuu ndio maana nikasema kwa cheo cha DED kuajiriwa kama first appointment ndio makosa ama umimi. Matokeo ya umimi ni kukwana tu hamna namna
Sawa tunataka aje na vyeti vyake original huku tunazo copy tuu. Sasa ubaya uko wapi? au nyie mnadhani original inatunzwa na serikali
Sawa Mkuu, lakini kama ni hivyo wangetangaza kuwa TAMISEMI or whatever wanatangaza nafasi za DED kwa wafuatao na wanatakiwa waje na vyeti vyao na VCs zao, sio watu hao WAMETEULIWA KUWA MA-DED hivyo waje hizo particulars. HAIPENDEZI KATIKA UTUMISHI WA UMAA
 
Ina maana waliteuliwa bila kufanyiwa vetting?

View attachment 1878462
Awamu ya hovyo hii,kuna wengine wameteuliwa kisarawe elimu haieleweki,bidada mmoja mashalah
Screenshot_20210803-205344_Twitter.jpeg
 
Mwenye CV ya aliyekuwa afisa tarafa wa kinondoni ambaye amaepelekwa kisarawe aliyechukua nafasi ya Mussa Gama aiweke hapa tafadhali. Maana online ipo ya kusema ni System Administrator na Data entry phoneshack Ltd.

Mkurugenzi yahitaji uwe senior civil servant with at least A degree in Accounting, Economics or Business Administration kama sio masters. Kidogo hii inaonesha mapungufu kwa mteauaji.
 
Hawa hawaendi kuwa DEDs hawa ni makala wa uchaguzi kuhakikisha ccm inashinda.
Kwa aina hii ya maDED wa kutoka uvccm, wakuu wa idara watakuwa wanajiongoza.....hakuna DED hapo, labda mhudhuriaji wa ofisini.
 
Wastutoe Road kujadili ujinga wao
TUKO PAMOJA NA FREEMAN EIKAEL MBOWE
 
ummy nae kiherehere, ameshindwa nini kumwambia ntejengwa awapigie simu kuwaita ofisini kwake.
 
Mwenye CV ya aliyekuwa afisa tarafa wa kinondoni ambaye amaepelekwa kisarawe aliyechukua nafasi ya Mussa Gama aiweke hapa tafadhali. Maana online ipo ya kusema ni System Administrator na Data entry phoneshack Ltd.

Mkurugenzi yahitaji uwe senior civil servant with at least A degree in Accounting, Economics or Business Administration kama sio masters. Kidogo hii inaonesha mapungufu kwa mteauaji.
Huyu dada elimu yake ya hapa na pale nadhani
 
Mbona hata ukipata ajira ya ualimu ni lazima unapoenda kuripoti lazima uende na vyeti sasa unashangaa nn wakurugenzi kwenda na cv

Sent from my VFD 600 using JamiiForums mobile app
Hoja yako ni ya kijinga sana na inaonesha hujui lolote kuhusu utumishi wa umma , huwezi fananisha ajira za ualimu na uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri.
 
Huyu dada elimu yake ya hapa na pale nadhani
Mama samia nikimuangalia alivyo anza vizuri na vituko anavyo vileta sasa namshangaa tu, wakurugenzi gani hawa kawateua awamu hii.
 
Katiba mpya ndio suluhu pekee
Only in Tanzania Unateua Mtendaji DED, Hauna CV yake ila unajua tu ya Kwamba ni MwanaCCM. Hatutakaa Tukafika " Kujenga Nchi Kwanza si Kazi Rahisi Kivile. Hawa ndio Watasimamia Wilaya Zetu ktk Allocation and monitoring of our scarce resources. Daaa!
 
Neno vetting linakera sana, ila wabongo hamuishi kulitumia kama vile lina mantiki yoyote kubwa.
Dada yangu (si mama kwangu), Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema "Rais huwa hakosei". Kwa usemi huo tu tayari alikuwa kakosea maana hakuna mtu asiyekosea, hayupo na hatakuwepo!

Ndio maana unahitajika upitiaji makini (keen vetting) katika kusoma, kuchambua na kuamua kabla ya kutandika mkeka wowote ule hadharani. Atakuja kuteua aliyekufa au mfungwa!

Sasa ona ambavyo kila uteuzi analazimika kurudiarudia na kurekebisha, hususan baada ya kukosa kutangulia uhakiki makini. Hata bunge la bajeti alilikosea mara kadhaa kwa kuliita bunge la katiba. Akasema: "sijui nina maradhi gani na katiba." Ni maradhi ya kukosea mara kwa mara kwa kukosa umakini!

Si maradhi ya katiba tu, bali hata maradhi ya wizara (mathalani kateua waziri wa tozo kandamizi badala ya waziri wa uchumi na mipango endelevu na yenye tija), maradhi ya mikoa, maradhi ya wilaya na sasa maradhi ya wakurugenzi wa halmashauri. Mkurugenzi mmoja anataka aongoze halmashauri mbili kwa wakati mmoja. Mara paap, kajikuta kakosea tena!

Je, atawezaje (au wasaidizi wake), kusoma na kuchambua kwa makini mikataba mikubwa yenye kurasa zaidi ya 800??!!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom