Wakuu huyu 'Mama Ntilie' anapataje faida? Naona kama nimefaidi zaidi Ugali mboga 7

Wakuu huyu 'Mama Ntilie' anapataje faida? Naona kama nimefaidi zaidi Ugali mboga 7

Mwache mdogo wangu kalala kwenye lindo. Ni hivi unapewa bamia moja, mchicha kidogo, samaki kibua wanatoa feri wanajua jinsi wanavyo bargain, ugali wanakupa umeshapigiwa mahesabu. Mimi nina mama ntilie pale kwangu. Nyama minofu miwili, mchicha au mboga yoyote kidogo, maharagwe na mchuzi kidogo. At the end of the day kama wateja wamekuja anapata faida elfu 3 tu baada ya kunilipa mimi za pango na kulipa alipokopa kuanza biashara asubuhi. Upo. Akirudi nyumbani mme kanuna wakati yeye kabeba mandoo na mtoto mgongoni. Kesho yale yale halafu mnakuja humu mnatunanga wanawake hamjui maisha tunayoishi. Mnawaangalia hao mabishoo lakini mnasahau mama na dada zenu wanaoteseka kusomesha wadogo zenu bila msaada wa waume zao wanaolewa na kujidundika madawa.
Kwa uliyoandika hapa ina maana mama na dada ntilie ndio wanaendesha familia huku waume/ bwana zao wakibembea tu. Sasa wanaweka nyumbani watu wa aina hiyo wa kazi gani, si waachane nao? Wanajibebesha mizigo ya kujitakia!
 
Walikuibia nadhani walikuona ni wa kutoka shamba. Pale sisi masela kwa huo msosi huwa tunakula kwa jero tu na glass kubwa ya juice tunapewa.kwa tsh 500/tu. Wewe wanakuuzia 1500 sababu wanajua mgeni.
 
Hiyo bei ni sawa kabisa
Unga anasaga mwenyewe
Dagaa wa mwanza bei chee
Samaki kibua wa kichina kipande bei chee
Bamia (mlenda) ndo usiseme sokoni ni kama unapewa bure
Matembere analima mwenyewe kwenye mtaro wa maji ya choo uswahilini
Maharage dukani si bei kubwa yakivimba kwa amila uhh full kushiba
 
mwaka 2017 baada ya kuitendea haki hela yote ya kujikimu, katika ku survive pale keko ndani ndani mule niliwahi kula ugali una nyama na mbg km sita hv kwa sh 300, kuna jamaa yang alikua na kiherere here akaniiga tukaenda wote, tulimrudisha geto kwa torori, siku mbili alivaa pempasi sijui ndio pedi zile m sijui huko, ilikua ukikaa nae karbu ukisikiliza huko tumboni n kama yale magari ya kuchanganya zege, huko chini kibiti nako ni mwendo wa kubadilisha honi na krach tuu,
Jamani we unachekeshaga sana na wewe nimecheka mpaka basi
 
mwaka 2017 baada ya kuitendea haki hela yote ya kujikimu, katika ku survive pale keko ndani ndani mule niliwahi kula ugali una nyama na mbg km sita hv kwa sh 300, kuna jamaa yang alikua na kiherere here akaniiga tukaenda wote, tulimrudisha geto kwa torori, siku mbili alivaa pempasi sijui ndio pedi zile m sijui huko, ilikua ukikaa nae karbu ukisikiliza huko tumboni n kama yale magari ya kuchanganya zege, huko chini kibiti nako ni mwendo wa kubadilisha honi na krach tuu,
Sema ilikuwa ni wewe acha kusingizia jamaa.

Wagerasi bana!
 
Ni ukweli usio na mashaka kuwa yatendwayo katika migahawa mingi ya mtaani, masokoni na mashuleni ni mambo ya kukifu,yakuongofya na kutetemesha sana japo inatulazimu kutumia vyakula hivyo vya magengeni hasa muda was asubuhi na mchana kulingana na muda(kuenda nyumbani na kurudi kibaruani au kazini) ama umbali wa mahala pa kazi na unapoishi pamoja na kipato chetu..
Yote ya yote,Mwenyezi Mungu ni Mwingi was kudra na hekima zake hazichunguziki kibiadamu amekuwa began nasi katika kutunusuru na mazira yote...maana mama genge wengi wanatumia rejects/ second option kuanzia nishati,sufuria,sahani,nafaka,mboga na ha viungo kwa ujumla pamoja na maji.
Pia wale was imani zao nao wanafanya yao biashara iwe amshamsha vigezo na masharti ya mtaalamu kuzingatiwa lakini Mungu kwa huruma bado anasimama nasi tunaishia kutibu typhoid na U.T.I tu
Nawatakieni mchana mwema wanazengo
 
Ugali+amira kibao.
Matembere sokoni mengi tu yakuokota, gharama yako maji ya kusafishia na sasa hivi mitaro imejaa.
Dagaa wapo waliolowa na mvua hawafai kusafirisha, nikuwasafisha sana.
Nyama ndaza hizi bongebonge kilo elfumbili.
Kuku hii siri tangu, piga ua sikuambii.
Sentensi ya mwisho mkuu ni kama marehemu kuku /vibudu waliojifia mabandani
 
Kuna siku nilisogea kiure chole huko uzaramuni nikaulizia msosi nikaambiwa wali kuku 1500/=, kuku wa kienyeji nikaghairi kula, siwezi kunywa hizi juice za vibandani hata kwenye ki mghahawa changu siweki wanazoita fresh juice, unaweza kuua mtu kwa magonjwa
 
Vibanda vya juice zile clear disposable wanaziosha wanarudisha kwenye mzunguko
Kipi Bora? Kunywa soda yenye sumu za viwandani?
au kunywa juice yenye hatihati ya kuwa na matatizo lakini ndani yake pia kuna virutubisho muhimu.
 
Back
Top Bottom