Kwa bajeti ya 1.5M unaweza kupata HP Brand New, ila cha msingi ni kuangalia specifications kuliko kuangalia brand pekee.
Kwa matumizi yako ya programming, internet na movies, ningekushauri ulenge angalau Core i5, RAM 8GB na SSD ya 512GB. Ukipata RAM 16GB itakuwa vizuri zaidi kwa programming. Kuhusu storage, SSD ni bora kwa speed kuliko HDD.
Ila kuwa makini na matangazo ya Core i7 kwa bei rahisi sana, kwa sababu generation ya processor ni muhimu kuliko jina la i5 au i7 pekee.
Ushauri wangu: nunua yenye warranty ya uhakika na hakikisha ni Brand New kweli, si refurbished iliyopakwa maneno ya kibiashara. Kwa 1.5M, specs unazopata ndizo zitakazoamua kama ni dili au umepoteza pesa.